Nimeshuhudia muujiza wa ajabu nchini Germany!

Nimeshuhudia muujiza wa ajabu nchini Germany!

Mkuu inaonekana wewe ni mwanafalsafa sana. Maajabu kwangu ni katika namna rahisi ya usemi wa kila siku wa mtaani ambao hata babu yangu kule kijijini ataelewa; jambo ambalo si rahisi kuelewa au kufafanua ni jinsi gani linatokea. Na pia hii ni katika context ya ufahamu wangu na wengi wa waliokuwa nami siku hiyo - pengine mwingine au wengine wanaona au waliona si maajabu.

Kuruka na kukaa hewani kwa ndege kama Airbus 380 yenye uzito wa maelfu ya tani ni maajabu kwa wengi - lakini si kwa watu wanaoelewa kanuni za aeronautics. Au hata jinsi unavyoweza kupata picha live kwenye TV, ni maajabu kwa wengi. Kumbuka kwamba hata kitendo cha Yesu kutembea juu ya maji, au kupasuliwa kwa bahari ili wa-Israeli wapite toka Egypt, ni maajabu kwa kuwa ubongo wa mwanadamu kwa sasa si makini kuweza kujua science iliyo nyuma ya matendo hayo. Kumbuka tunatumia asilimia 10% ya uwezo wa ubongo wetu.

Ndio maana nikauliza - "Kuna mtu anaelewa hili?" Kama kuna mtu anaelewa basi atatufafanulia na kwa tutakaomwelewa haitakuwa maajabu tena.

Kwanza kabisa hatujui kama hii ni optical illusion ama la. Tutajuaje kama si optical illusion?

"Magician's" tricks nyingi ni optical illusions tu.

Tutajuaje kwamba hii si moja ya hizo?
 
Kwanza kabisa hatujui kama hii ni optical illusion ama la. Tutajuaje kama si optical illusion?

"Magician's" tricks nyingi ni optical illusions tu.

Tutajuaje kwamba hii si moja ya hizo?

Sasa Mkuu unaanza ubishi. Nilishasema nilikuwapo hapo niliona kwamba hao ni watu halisi. Sasa hili suala la optical illusion unalitoa wapi? Ona kwamba Mimi mwenyewe nimepiga hizi picha sio kwamba nimezipata kwenye mtandao. Kama uko makini utaona nimepiga picha toka angles mbalimbali ili kukupa 3D context. Optical illussion gani unaongelea wakati unaona kuna 3D context na picha zilipigwa kukiwa na objects (including live objects) kwenye foreground na background?
 
Sasa Mkuu unaanza ubishi. Nilishasema nilikuwapo hapo niliona kwamba hao ni watu halisi.

Optical illusion inawezekana kwa sababu umesema umeona kwamba ni watu halisi. Umeona.

Hata karata tatu pale Manzese unaona zinavyochanganya, but it is nothing but a sleight of hand.

Sasa hili suala la optical illusion unalitoa wapi?

Kwa sababu umeweka imani kubwa sana katika unachokiona bila kujua kwamba inawezekana umewekewa mtu wa maboksi, au mtu ni wa kweli lakini ana kilo ishirini.

Ona kwamba Mimi mwenyewe nimepiga hizi picha sio kwamba nimezipata kwenye mtandao.

Bado unaongelea picha. Unaweza kwenda in the middle of the Sahara sehemu ambayo haina maji, ukaona kuna dimbwi la maji kutokana na mirage, ukilisogelea nalo linazidi kuendelea kuwa umbali ule ule, mwisho linapotea. Mirage.

How do you know this was not a mirage?

Kama uko makini utaona nimepiga picha toka angles mbalimbali ili kukupa 3D context.

3D is not enough when there is 4D. Moreover, you cannot represent 3D on a 2D media, especially because you are not even covering the event from three planes. Unajua utosini kwa huyo aliyebebwa kuna nini?

Optical illussion gani unaongelea wakati unaona kuna 3D context na picha zilipigwa kukiwa na objects (including live objects) kwenye foreground na background?

As long as unaishia kuongelea picha tu, an optical illusion is very possible.

Moreover, you have not defined "muujiza wa ajabu" ni kitu gani? Kitu inabidi kiweje ili kuweza kuitwa "muujiza wa ajabu"?

Kwa sababu kuna mtu anaweza kukwambia kuuliza kwa nini hao watu wamejifunika miguo guo yote hiyo? Wameficha mashine gani kwenye hiyo miguo?

Isije kuwa mtu kakaa kwenye kiti cha chuma kimeunganishwa kwa uficho mpaka chini, wewe unaona muujiza wa ajabu!
 
I see that the Turk is back as an Arab 🙂

turk-hidden-1-4.gif
 
Huu sio uchawi wala sio mazingaombwe, hao ni waturuki kunavyuma wanaweka kuwasapoti ndio maana wanavaa grovu na mashati ya mikono mirefu kuficha, ukitembelea miji mingine ya germany kama Berlin, Leipzig, Koln etc utawakuta. hakuna uchwai hapo ni sanaa tu za kituruki.
 
Huu sio uchawi wala sio mazingaombwe, hao ni waturuki kunavyuma wanaweka kuwasapoti ndio maana wanavaa grovu na mashati ya mikono mirefu kuficha, ukitembelea miji mingine ya germany kama Berlin, Leipzig, Koln etc utawakuta. hakuna uchwai hapo ni sanaa tu za kituruki.

Afadhali wewe Mkuu Alles umesema na kutupa sababu ya kisayansi kuliko Mkuu Kiranga hapo juu ambae naona analipeleka hili mbali sana, optical illusions, do!!! Maelezo hayo ni sawa na ya mwanasheria aliyekufa miaka 100 iliyopita afufuliwe leo na kuona Airbus 380 inaruka angani!

Mie pia nilidhani kuna frame ya chuma ambayo in atensile strngth kubwa ambayo imepindishwa kwa namna ya helufi "S" kufuta mavazi na kuwekewa namna ya seat ili yule wa juu akae bila kuchoka kwa muda mrefu. Kwa namna hiyo support ya weight ya mtu aliye juu sio mkono na goti la huyu aliye chini bali base ya ile frame. Mtu wa chini anachotoa ni "stabilizing force" ambayo haibebi uzito wa yule aliyeko juu.
 
huo ni ubunifu wa hali juu wa kujilia pesa kiulaini
 
sumbawanga wale wataalamu wanatundika koti hewani na kofia
 
hakuna maajabu , kuna chuma kigumu mithili ya nondo, kimekunjwa kwa weledi kikitokea chini alipokaa jamaa kikipitia kwenye manguoa yao kufuata mkono , na kisha hiko chuma ndio kilichooundwa mithili ya kiti ambayo jamaa wa juu kakalia.

balance ya mtu mwa juu inategemea zuzo wa mtu wa chini ambae pia amekaa kwenye kitu kilichoundwa mithili ya stand za kuwekea maua.
hata mie naweza....kumbe naweza kula vichwa vya waTz nikirudi

Kwani upo wapi mkuu, naona unasema ukirudi?
 
Wana JF, hivi karibuni nikiwa katika matembezi katika mitaa ya jiji la Frankfurt nchini Germany, nimekutana na muujiza ambao hadi leo nashindwa kuelewa ni nini kilichokuwa kinatendeka. Niliwakuta watu wawili wa asili ya kiarabu wakiwa wamebebana kwa njia ya ajabu kama inavyoonekana katika picha. Walikuwa wamekaa hivyo kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili ya kuchoka au kutumia nguvu. Niliweza kuhakikisha wote wawili walikuwa ni bnadamu hai na sio picha wala sanamu. Walifanya hivi ili kujipatia chochote toka kwa watu.

Kuna mtu anaelewa hili?

Duh!Hii kali,uliwaona wakati huyo wa juu anapanda huko alitumia njia gani?
 
Wee ndio pekee uliojaribu kung'amua mtego wao, kumbe ni ujanja tu, Wengine humu ndani ni porojo tu. Na inawezekana sio Waarabu bali wamejifunga maguo hivyo kuficha uhalisia wa jambo hilo
hakuna maajabu , kuna chuma kigumu mithili ya nondo, kimekunjwa kwa weledi kikitokea chini alipokaa jamaa kikipitia kwenye manguoa yao kufuata mkono , na kisha hiko chuma ndio kilichooundwa mithili ya kiti ambayo jamaa wa juu kakalia.

balance ya mtu mwa juu inategemea zuzo wa mtu wa chini ambae pia amekaa kwenye kitu kilichoundwa mithili ya stand za kuwekea maua.
hata mie naweza....kumbe naweza kula vichwa vya waTz nikirudi
 
Mmmmhhhh!!!!!!! kwa kweli ni zaidi ya maajabu, ndo gymnastics hzo
 
Mnashangaa nini? Kuna babu kule Loliondo anatibu kisukari, ukimwi, shinikizo la moyo, na magonjwa mengine mengi tu kwa miujiza.
 
Back
Top Bottom