Nimeshuhudia moto Mkubwa uliotokana na jiko la gesi leo.

Wakuu nilikuwa napita kichochoro fulani hivi, Kuna mama alikuwa kwenye maandalizi ya kupika
ghafla nimeshuhudia moto mkubwa kutoka kwenye Lile jiko, Siku wahi kupiga picha
zaidi ya kukimbia na kumuokoa mtoto mdogo ambaye alikuwa karibu na jiko hilo.

Nimejaribu kuuliza nini kimesababisha tukio lile yule mama anatetemeka na kulia tu.
Sasa najiuliza tu, Lile jiko lingekuwa ndani nini kingetokea? Hivi vitu ni vizuri lakini
ni muhimu kuwa makini navyo.

View attachment 1183587

Kwanza ni makosa kutumia mtungi mdogo alafu ukawa unapikia nje kuna majiko maalum ya kupikia nje.
Mtungi mdogo unahitaji sehem ambayo hakuna upepo mkali.
Ukiwa unawasha moto wa gas kwanza hakikisha gas ilikua imefungwa(ilivyotumika mara ya mwisho) pili washa kwanza moto usogeze karibu na burner kisha ufungue gas hapo gas itakutana na moto kwa haraka kabla haijasambaa.
 
kosa jingne ni ile unaanza kwa kufungua gesi half ndio unapiga kiberiti.

Aloo acha hio tabia, siku utakuja kuungua mpk tumboni,

it seems imposible untill is done.
Hivi ndo tunavyofanya wengi mkuu, wengine tumeanza kumiliki hayo majiko kwa kununua
mikononi kwa wlioshindwa kulipa VICOBA
 
aisee kuna siku nilimkuta mzee mmoja anapigana na huu moto wa aina hii tena mtungi mkubwa.

kisa hakifahamiki,ila mpaka nafika mimi pale,ile pipe imeungua yote moto umeshika kwenye koki unafoka balaa watu wanauzima na mchanga,kwa vile shepu ya mtungi haisapoti hilo zoezi ikawa kazi bure.sasa hofu yangu ikawa ni kwenye mtungi kuburst sababu ya mtungi kupata moto sana,nikaumiza kichwa nikaona hapa ili kuuweza kwanza wacha niupige maji.nikachota maji kiasi flani nikafanya kama nauchapa na maji ule mtungi mdomoni kwa nguvu sana,ukazimika.sababu koki imeungua bado inakawa inaruhusu gesi kutoka.nikaipoza na maji kisha nkaitoa hapo zoezi likawa limefanikiwa.

haya mavitu wameyatengeza vizuri sana tatizo liko kwa watumiaji,tunakosa umakini tu na kufanya mazoea.mfano umemaliza kupika,unatakiwa ufunge(chomoa)koki ili hata ikitokea ajali ya moto,gesi isiwe sehemu ya kuikuza ajali hiyo.
 
wakati mwingine unaweza chukua kitu ka shuka ukalitia kwenye maji ukaja ukaufunika mtungi tena unaanza kuwa unajizuia na moto ukiwa unausogelea kwakutumia hilo shuka hasa sehemu za mbele
 
Aisee wapi Apo mbona pakavu Sana napafananisha na iramba ivi daah network sitatizo kweli uko
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom