Simulizi: Nilinusurika kuchomwa moto

Apr 19, 2023
77
123
NILINUSURIKA KUCHOMWA MOTO 1
IMG_7704.jpg

Nilikuwa nimekaa zangu sina hili wala lile, mara simu ikaingia kutoka kwa rafik yangu, akanimbia leo unaonaje tukachek mechi pale uwanjani? Nikamwambia sina uhakika kama nitapata ticket, akaniambia hilo ndo tatizo la ushamba wako. Tickets tutapata, kwanza leo hatuchezi na timu kubwa kwamba hayo mambo yataleta shida, nikamwambia sawa basi tutaingia.

Alikuwa shabiki wa timu ambayo na mimi nilikuwa shabiki wa timu hiyo hiyo, hivyo tukakubaliana kwenda kuicheki hiyo mechi. Nilijiandaa mida ilipofika, na kwa sababu umbali kutoka ninapokaa mpaka uwanja wa mpira ulipo sio mkubwa, niliamua tu kutembea kwa mguu wakati huo nikiwa nimekubaliana na rafiki yangu Johnson kukutana pale pale uwanjani.

Nilifika sehemu fulani ambapo nilikuta watu wengi wakiwa wamekusanyika, kuna mtu alikuwa amekamwatwa pale
Alikuwa amepigwa vibaya sanaaa, na watu wengi wamemzunguka, wakiwa wamemfunga kamba za miguu na mikono.

Nikajaribu kuwauliza watu ni nini kinaendelea, mtu mmoja akanieleza

kuwa huyu amekamatwa akiiba betri ya gari ambayo ilikuwa imewekwa juu ya gari lile, sasa plan ilichorwa kuanzia kwa wenzake halafu yeye anapokea na kupeleka sehemu nyingine,
Ikiwa na maana kuwa aliyetoa Betri pale sio yeye, ni mtu mwingine ambaye aliivusha na kumpa mwingine

Huyo mwingine ndo akampa yeye, na yeye kuna mtu alikuwa anaenda kumpa, ndivyo wezi wanavyofanya huku, unakuta kwenye line wapo kama watano, sasa ili iwe vigumu kukamata kitu chako, wanachokifanya ni kupokezana tu, ili ukimshtukia mmoja ukija kumsearch usipate kitu, na hao wote

watano kwa pamoja hutaweza kuwajua. Ndio maana huku ukishaibiwa kitu sahau kuhusu kukipata.
Lakini za mwizi siku zote huwa ni Arobaini, katika line ya hawa leo huyu ndo kapatikana. Kuna mzee mmoja ni kama kaushtukia mchezo akajitoa mwanga kupiga kelele na kumrukia ndo watu

wote hawa tukafika na kuanza kumshughulikia. Huyu mzee kajitoa mwanga kwa sababu ukiwaharibia hivi baadaye wanaanza kukuwinda, wanaweza kukuchoma visu mpaka kukuua, ndio maana wengi wakiona wananyamaza, hawasemi kitu wala kufanya kitu.
Lakini tutakachomfanyia huyu itakuwa funzo

kwa wenzake wanaotutaabisha usiku na mchana. Walimpiga vibaya sana, kila mmoja anapiga anapoona
Akajitokeza baba mmoja akasema ole wa mtu yeyote hapa aite polisi, ukigundulika na wewe tunakujumlisha naye, maana nyie mtakuwa wamoja.
Hawa wajinga ukiwapeleka polisi kesho wametoka

Na wanaendelea na uhalifu wao, sisi ndio tutawashughulikia wenyewe.
Muda huo anaongea watu wanaendelea kumpa kipondo jamaa, wengine hata hawakusikiliza anasema nini, japo alikuwa akitumia sauti ya juu. Ila wengi walisapport hakuna kuita polisi hakuna kuita polisi

Kipigo kiliendelea na jamaa alikuwa hatamaniki. Alipigwa mpaka ungetamani umuondoe pale hata kama ni mwizi mkubwa kiasi gani. Ila sasa wananchi wenye hasira kali huwezi kuwaeleza chochote hapo.

Yule baba aliyekuwa anasema mtu yeyote asiite polisi alikuwa ana hasira sanaa na hao jamaa (wezi) yaani alikuwa anakaza apigwe apigwe!

Sasa akapata wazo akasema, huyu jamaa tumchome moto, mimi natoa petroli kwa gharama yangu leteni mipira tumchome moto,
Yule mwizi alibembelezaa

Japo ndo hivo maneno yalikuwa hayawezi hata kutoka vizuri lakini alibembeleza sana wasimchome na wakati huo wameshamvunja hadi miguu
Yule baba akasema kama unataka kusalimika tuambie uliyekuwa unaenda kumpasia betri ni nani na uliipokea kutoka kwa nani?
Jamaa hawezi hata kuongea

Wakamuuliza, tuambie ulikuwa unampasia nani? Leo lazima tuwapate wote. Usiposema tunakuchoma moto unakufa unawaacha.

Alikuwa hawezi hata kuongea,
Alinyoosha kidole kuelekea upande niliokuwepo mimi akasema huyo halafu akawa hawezi kuongea tena.
Sasa mimi nilikuwa mtu ambaye sijarusha hata jiwe moja kwa huyo mwizi kwa sababu hata siwezi yaani. Na hilo ndo likawa kosa kubwa
Watu waligeuka

wote wakasema kumbe ni wewe, kuna kama wawili walikuwa wanatetea ambao waliniona nikija plus yule aliyenisimulia kinachoendelea,

Lakini wapiii, watu wote hasira zao zikaamia kwangu maana mtu mwingine aliyekuwa pembeni yangu alikuwa ni yule aliyeibiwa na wengine walikuwa ni akina mama na wengine sikumbuki, Nilivutwa na kuingizwa kati,
Watu wanapiga kelele, wachomeni wote wachomeni wote wachomeni wote,

Nikawa napambana kuwaambia mimi simjui huyu mtu, mimi ni mpita njia nimekuta mwizi anapigwa nikasimama…wakati huo wapo wanaonitetea pia ila ni wachache sanaaa, wengine hata hawaelewi chochote ila wamekazia apigwe achomwe moto

Eeh bhana ile siku sitakaa niisahau,
ila kukutoa tu wasiwasi, ni kuwa bado niko hai ndo maana nipo hapa nakusimulia,
Sasa nini kilitokea? Na niliponaje?!

Tukutane sehemu ya mwisho inayofuata nikumalizie kisa hiki
 
NILINUSURIKA KUCHOMWA MOTO 1
View attachment 2593018

NILINUSURIKA KUCHOMWA MOTO 2

IMG_7722.jpg

Kelele za watu wakiongea kwa nguvu apigwe! Apigwe! Apigwe! zilizidi. Wakati huo napambana sanaa kujitetea kuwa huyu mwizi mimi simjui, na sielewi kwanini amenitaja. Sikukubali kukalishwa chini kizembe, maana walikuwa wanasema kaa chini kaa chini! Nilijetetea kwa nguvu na kuongea kwa sauti kubwa, kwa nini mnamuamini huyu bila sababu? Mm simjui kabisaa, ana sababu zake za kunitaja anajua mwenyewe lakini mimi hapa nilikuwa mpita njia tu, kwanza naelekea kuangalia mechi pale uwanja wa CCM
Sasa wakati watu wanaendelea kunivutavuta wanipige maana kinachochelewesha zoezi hilo la mimi kuanza kupigwa kama yule mwizi baada ya kunitaja kuwa nashirikiana naye wakati mimi simjui, aliulizwa tu ulikuwa unaenda kumpasia nani mzigo aufikishe sehemu nyingine yeye akanyoosha kidole kuelekea kwangu mimi nilipokuwa nimesimama nikishangaa tu watu wanavomchezeshea kipigo (kama tulivyoona sehemu ya kwanza)
Sasa mimi kwangu kipigo bado hakijaanza kwa sababu kuna wengine wananitetea ambao waliniona nikija pale wakiongozwa na yule aliyekuwa akinisimulia
kilichotokea kuhusu huyo mwizi, ila sasa point zao zinakosa mashiko kwa sababu hawana uthibitisho kuwa sio mimi, maana hata mwizi ni kawaida kufanya hivo, anakuibia halafu anakuja kukuuliza vipi nini kinaendelea? Umeibiwa? Inabidi huyo mwizi tumsake! Na wakati huo mwizi ndo yeye
Sasa katikati ya hizo purukushani, kumbe wakati watu wanapiga mwizi na wanataka kunipiga mimi kwa sababu ya hayo mashtaka ya kushirikiana na mwizi, na wao wanaiba hapo hapo, Maana kwenye hizo purukushani simu yangu nilichomolewa bila kujua, wallet pia wakapita nayo.
Mimi niko bize na kupambana na kuokoa uhai wangu, maana maamuzi wanayotaka kuyafanya ni kutuchoma wote moto kwamba ni wezi. Na kumbe na wao wakapita na hivyo vitu vyangu,
Sasa kwa sababu nilikuwa nikitumia nguvu sanaa kujitetea, maana kweli sio mwizi, hivyo ile aibu sina, Niliwaambia
nilikuwa naenda kukutana na rafiki yangu uwanja wa CCM tukacheki mechi leo kuna mpira wa timu fulani. Wakaniambia basi mpigie simu tumuulize sisi wenyewe hapa hapa, ole wako akikukana tunakuchoma moto
Sasa si nikaingiza mkono mfukoni nitoe simu tumpigie, kumbe simu sina,
nikawaambia simu yangu aisee nimechomolewa, Aloooh kile kipigo nilikula siku hiyo sitokaa nisahau kwenye maisha yangu, waliona nawaletea mzaha Nilipigwaa, nilipigwa vibaya mnooo, mpaka nikapoteza fahamu kabisaa
Nilikuja kupata fahamu baada ya siku mbili nipo hospitali.

Na kumbe yule ndugu aliyekuwa akinitetea kuwa mimi sio mwizi maana aliniona nikija na akanisimulia kinachoendelea, baada ya kuona hawa watu wako serious wataniua, maana aliona yule mwizi halisi ameshakufa tayari kwa
kipigo japo ni alikuwa amepoteza fahamu tu, alijua na mimi hawa watu wataniua vile vile, na sasa nauawa bila sababu
Aliamua kuondoka na kwenda upande wa pili huko umbali kidogo na kupiga simu polisi, akawasistiza wawahi maana hawa watu wameshaua mtu mmoja na wa pili watamuua pia
kama polisi mtachelewa.
Japo kumbe pia na yeye hakuwa wa kwanza kupiga simu polisi kumbe na watu wengine walikuwa wameshapiga, polisi ndo akamwambia tunakuja tumeshapata taarifa.
Polisi hawakuwahi kiivo lakini wakati wanakuja walikuta nimepigwa mpaka nimepoteza fahamu huku raia
wao wakijua nimekufa kama mwenzangu, polisi walifika raia wote baada ya kuona polisi hakuna aliyebaki, wakatukagua na kugundua tupo hai wakatupeleka hospital fulani chini ya uangalizi wao Hayo alinisimulia huyo ndugu aliyenisaidia kuwapigia polisi na kwa sababu roho yake
ilimuuma sana kwa kitendo nilichofanyiwa aliamua kufuatilia Usalama wangu mpaka mwisho na baada ya kupona yeye ndo alinichukua polisi. Mungu ambariki sanaa
Yule mwizi halisi nilikuwa naye kwenye wodi moja, ni vile tu nilikuwa siwezi kuamka na kumshughulikia
Nilimlaumu sanaa kila siku nilikuwa nikimwagia matusi ya kila aina kwa ukatili alionifanyia, nilitamani nipate hata bunduki nimuwashe risasi hapo alipo, polisi walipogundua kinachoendelea waliomba tubadilishwe wodi tusikae wodi moja.
Hiyo ndo ilikuwa ponea yake maana nilikuwa
nawaza kuwa nitakuja kumfanya huyo jamaa kitu kibaya mnoo kama vipi tufe wote.
Lakini yote yaliisha nilirudi nyumbani pamoja na yule ndugu aliyekuwa akishirikiana na familia yangu kuhusiana na hali yangu.
Na sasa naendelea na maisha yangu na kwa kweli sitokuja kuisahau hiyo siku

Hii story ni tafsiri tosha ya wengi walioko magerezani na cells. Wapo wengi ambao wameingia hivi hivi, hana kosa hata robo kasingiziwa mwanzo mwisho.
Tuna kitu cha kujifunza hapaa
Eeh bhana mm sina la ziada zaidi ya kukukaribisha kwa ajili ya story nyingine kali kama hii.
 
Inanikumbusha mbali sana, nilishakamatwaga maeneo ya fukwe za ziwa huku Mwanza, mwenyewe nilikuwa nabarizi huku nna binocular (darubini) yangu nikiwa nacheki maeneo ya ziwa kwa utaratiibu huku napunguza stress zangu za ujobless, nakuja kushtuka nimezungukwa na hawa sumajkt wanadai eti wana wasiwasi na mimi kisa nina darubini eti huenda mimi ni al shabab aisee walinichukua na kunipeleka huko kambini kwao, walinikagua hawakuona cha maana, walinipiga sana wakaita polisi nikawekwa sero nilichezea kichapo cha kutosha.
Mungu saidia ilikuwa ni usiku wa mwaka mpya na agizo na jiwe lilikuwa haitakiwi kujaza mahabusu bila sababu na kwa siku hiyo ilikuwa lazima walete watu wapya usiku huo. Ndio ponapona yangu nikatoka bila kutoa hata sh 100.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom