Nimeshtushwa na idadi ya watoto wanaosoma shule binafsi kurudishwa shule za Serikali

Mkuu tofautisha lugha na ujuzi, kujua kuendesha gari ni ujuzi, kujua kingereza sio ujuzi.

Kama kujua kingereza kungekua na faida, wa south Afrika wote wangekua wameajiriwa ama wanigeria ama hata wakenya.

Nachosema, kwa ulimwengu wa sasa, lugha haihawahi kua kikwazo cha mtu kufanikiwa na pia isiwe kigezo cha kumpeleka mtoto shule, kuwe na additional skills ambayo mtoto ataipata hata bila kujua kingereza hiyo itakua na value kubwa sana kwenye maisha yake kuliko kujua kingereza.

Leo ukienda gereji, gari nyingi zinatengenezwa na vijana ambao hawakumaliza hata form 4, hawajui kingereza ila wana ujuzi. Vijana wanakuja kutoka st Patrick wanajua kingereza ila hata ujuzi tu wa kubadilisha taa ya umeme imeungua hawana, hii ni hasara.
Ndio shida iliopo hii, kupenda ku force watu wafanane..

Tufanye bas mtoto katoka kwenye bas la njano kaemda gereji, na mwingine katoka alikotoka kaenda gereji. Haya lete maneno hapo!!.

I think la muhim sana ni kiwafunza watoto ku discover their purpose and talents.

Na sis kama wazaz tuwatengenezee mazingira ku favour klle wanacho taman kufanya wakiwa wakubwa.

Ukilijua hil wala hutakaa kubishanamijadala hii.
Maisha si mashindano
 
Kutumia simu janja ndo kipimo cha kujua Kiingereza? unajua ni mara ngapi watanzania tumekosa fursa ndogondogo tu kwasababu kiingereza kinatupiga chenga?
Usilete hoja nyepesi kwenye mambo mazito. Huko maofisini muda wa presentation ukifika unatamani uingie chini ya meza maana ni aibu.
Huo ulikua mfano tu mdogo.

Fursa ndogondogo zipi umekosa kwa sababu ya kingereza?

Presentation maana yake nini, kwani lazima u present kingereza? Ili iweje? Kwamba changamoto ya uchafu jiji la dar es salaam nayo unatakiwa ui present kwa kingereza?
Unaleta hoja nyepesi kwenye hoja nzito. Jenga hoja nzito tafadhali.
 
Umeandika nini hiki?🙄
 
Jikuneni pale mikono yenu inaweza fika..
Msiumie watu wanapotumia hela zao kwa watoto wao. Hata kama shule hazima ubora ndio hivyo tena wameamua kuzitumia pesa zao vinaya, wengine mnaumia nin?
Kama mtu anaweza tumia 1m kwa ajil ya starehe tu zisizo na maana ,kuna shida gan mtu akaamua kupoteza hiyo pesa kwa namna nyingine!!!
Barikiwa sana Kwa ushauri mzuri
 
Kutumia simu janja ndo kipimo cha kujua Kiingereza? unajua ni mara ngapi watanzania tumekosa fursa ndogondogo tu kwasababu kiingereza kinatupiga chenga?
Usilete hoja nyepesi kwenye mambo mazito. Huko maofisini muda wa presentation ukifika unatamani uingie chini ya meza maana ni aibu.
Na kama uwezo wa kupata ada upo, tusiruhusu watoto wetu wakakutana na hii AIBU,....Huwa ni fedheha
 
Private saa hivi ghali sana, wa kwangu yupo nursery bado lakini ada ya mwaka ni ada ya mara mbili niliyokua nalipa chuo.... Usafiri tu nalipa 1.1M kwa mwaka, hapo bado ada, stationary,hela ya mitihani, uniform na takataka kibao...

Huyu mwingine bado hajaanza shule, sasa kama una watoto wanne aisee hapo Kuna kutoboa kweli

Private nyingi ukiweka na usafiri ada ni kama 2M kwa mwaka
Haya........
 
Kutumia simu janja ndo kipimo cha kujua Kiingereza? unajua ni mara ngapi watanzania tumekosa fursa ndogondogo tu kwasababu kiingereza kinatupiga chenga?
Usilete hoja nyepesi kwenye mambo mazito. Huko maofisini muda wa presentation ukifika unatamani uingie chini ya meza maana ni aibu.
Hehehehehe kwakweli ni kiingereza tu ndo kinatufanya tuzipende English medium manake kwa dunia ya Leo Kuna ugumu sana usipojua English hasa sehem mbali mbali kwenye ulimwengu wa kwanza na fursa zake.....mim nashukuru primary nilisoma English medium na imenisaidia sana kwenye mambo mbalimbali ila kiuhalisia ukitoa English hatuna utofauti na waliosoma kayumba & hii ni kutokana na structure ya syllabus ya elimu yetu ...
 
Huo ulikua mfano tu mdogo.

Fursa ndogondogo zipi umekosa kwa sababu ya kingereza?

Presentation maana yake nini, kwani lazima u present kingereza? Ili iweje? Kwamba changamoto ya uchafu jiji la dar es salaam nayo unatakiwa ui present kwa kingereza?
Unaleta hoja nyepesi kwenye hoja nzito. Jenga hoja nzito tafadhali.

Kuna mawili
Aidha hujawahi kuajiriwa
Au unakaza tu ubongo uonekane wa tofauti sana (katika ujinga)

All in all jikune mkono wako unapoweza kufika. Mwisho wa siku ipo tofauti ya ELIMU BORA na BORA ELIMU.

Kujua kiingereza ni muhimu sana.
 
Hehehehehe kwakweli ni kiingereza tu ndo kinatufanya tuzipende English medium manake kwa dunia ya Leo Kuna ugumu sana usipojua English hasa sehem mbali mbali kwenye ulimwengu wa kwanza na fursa zake.....mim nashukuru primary nilisoma English medium na imenisaidia sana kwenye mambo mbalimbali ila kiuhalisia ukitoa English hatuna utofauti na waliosoma kayumba & hii ni kutokana na structure ya syllabus ya elimu yetu ...

Labda English Medium za mchongo kaka. Ila English Medium zenye ubora kuna mengi sana watoto hujifunza apart from kujua kiingereza pekee.
 
Hv unaweza kuwa na pesa ukampeleka mtoto wako serikalini...?ww kama hela huna tulia...usijitekenye na kucheka mwenyewe
 
Average ya ada kwa mtoto mmoja private ni 3.5m kwa mwaka pamoja na mazagazaga yake yote. Sasa ndugu kama una watoto 3 ama 4 unaona kazi ilivyo pevu - kukusanya 14m kwa ada tu utasogea kweli.

Bara kujisalimisha kayumba.
 
Huo ulikua mfano tu mdogo.

Fursa ndogondogo zipi umekosa kwa sababu ya kingereza?

Presentation maana yake nini, kwani lazima u present kingereza? Ili iweje? Kwamba changamoto ya uchafu jiji la dar es salaam nayo unatakiwa ui present kwa kingereza?
Unaleta hoja nyepesi kwenye hoja nzito. Jenga hoja nzito tafadhali.

For instance, nimewahi kuhudhuria Seminar na mtu anayefanya kazi UN. Anaeleza linapokuja suala la kufanya kazi na East Africa kule Headquarters, Kenya wanatupiga gape na wanapewa kipaumbele zaidi kwasababu they are Fluent in English na wana exposure zaidi kuliko watanzania.

Hilo ni shirika moja tu. Yapo mashirika mengi sana yana hiyo kasumba. Endelea kua mzalendo na st kayumba zako na kiswahili chako wakati hata mzalendo namba moja Mwl. Nyerere alikua anauchapa ung’eng’e ule wa Malkia kabisa.

Acheni kukaza ubongo kwenye Upuuzi.
 
Hehehehehe kwakweli ni kiingereza tu ndo kinatufanya tuzipende English medium manake kwa dunia ya Leo Kuna ugumu sana usipojua English hasa sehem mbali mbali kwenye ulimwengu wa kwanza na fursa zake.....mim nashukuru primary nilisoma English medium na imenisaidia sana kwenye mambo mbalimbali ila kiuhalisia ukitoa English hatuna utofauti na waliosoma kayumba & hii ni kutokana na structure ya syllabus ya elimu yetu ...
Joannah
 
For instance, nimewahi kuhudhuria Seminar na mtu anayefanya kazi UN. Anaeleza linapokuja suala la kufanya kazi na East Africa kule Headquarters, Kenya wanatupiga gape na wanapewa kipaumbele zaidi kwasababu they are Fluent in English na wana exposure zaidi kuliko watanzania.

Hilo ni shirika moja tu. Yapo mashirika mengi sana yana hiyo kasumba. Endelea kua mzalendo na st kayumba zako na kiswahili chako wakati hata mzalendo namba moja Mwl. Nyerere alikua anauchapa ung’eng’e ule wa Malkia kabisa.

Acheni kukaza ubongo kwenye Upuuzi.
For instance, nimewahi kuhudhuria Seminar na mtu anayefanya kazi UN.
Mtaje huyo mtu so that we know ur not talking about a ghost
 
Back
Top Bottom