Tarehe 30 May 2022 mida ya saa nne asubuhi ulifanyika uzinduzi mdogo wa barabara ya juu kwenye makutano ya Kawawa/Chang'ombe na Nyerere road.
Kimsingi ni daraja moja ndo limefunguliwa Kati ya mawili ya mradi huo.
Mimi nilikuwa miongoni mwa watumiaji wa mwanzoni kabisa wa daraja Hilo.
Kilichonishtua ni kiwango duni Cha lami ilobandikwa hapo...ukiiangalia hata kwa macho yasio ya kitaalamu lami hiyo haifananui kuwekwa hapo, barabara haijatulia huko juu, ukifika juu karibu na katikati kuna kama kituta, lazima ushtuke.
Ukikaribia mwisho unashtushwa Tena na kituta. Yaani imagine Hadi mistari ile ya katikati ya barabara imepinda, hivi nyie watu mko serious kweli?
Magufuli angekuwepo ofisini mngefanya haya madudu?
==========

Uliza kwanza! Iliyowekwa kitaalam inaitwa Primer coat! Hiyo siyo lami Bali ni gundi ya kushikanisha kokoto zilizopo!
Wameaiacha hivyo kwasababu mradi haujakamilika, mkandarasi kakubali kuruhusu magari ili kupunguza foleni ingawa pia kapewa bonus katika ujenzi wa project hiyo! Fairly play!
Hivyo akikaribia kumaliza mradi atamalizia kuweka lami kurahisisha traffic flow!
Kwasasa tunywe mtori nyama zinakuja baadae: foleni ilikuwa kubwa mno!