Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Uwekezaji wa thamani kubwa kwenye miundombinu ya daraja la juu la Mfugale jijini Ilala mkoani DSM umepoteza dhima yake na thamani ya fedha iliyowekezwa pale kutokana na kwamba mradi umepunguza foleni kwa asilimia ndogo tu ambayo haiwezi kuakisika kwenye uhalisia wa maisha ya watu.
Mradi ulilenga kuwahisha viongozi kwenda na kutoka uwanja wa ndege. Barabara ya Mandela tokea Ubungo inaliingizia taifa fedha nyingi kuliko ya Nyerere kipande cha kutokea mjini hadi darajani.
Kosa hilo limerudiwa tena kwenye daraja la juu la makutano ya Nyerere na Kawawa eneo la Chang'ombe, daraja limelenga kusafirisha viongozi kwenda uwanja wa ndege. Huenda miradi kama hiyo kwa maeneo yaliyosalia ya Morocco, Mwenge, Magomeni na Uhasibu ujenzi ukafanyika kisiasa.
Kuna janga la foleni kwenye barabara ya Mandela hususan Mwananchi kuja Mfugale na Uhasibu kuja Mfugale.
Nini kifanyike Mfugale:
1. Nadhani makosa yasahihishwe kwa kuondoa taa za kuongozea magari chini ya daraja na kujenga mzunguko (roundabout) ili kupunguza foleni zinazosababishwa na taa kupitisha magari kwa zamu.
2. Ijengwe barabara ya njia mbili ya chini ya ardhi baada ya kupita njia ya reli kuvuka daraja hadi kuibukia usawa wa TBC ili gari za Ubungo - Bandarini zipite chini kwa chini.
3. Kama namba mbili hapo juu haiwezekani basi zijengwe barabara double za pembezoni mwa daraja ili kwamba gari za kwenda kulia na kushoto kwa daraja zisilazimike kupindukia katikati ya barabara ya chini ya daraja (kwenye taa) na kwamba barabara hiyo ya chini itabaki maalum kwa gari za Bandarini, Temeke nk na pia gari za Ubungo nk.
Tukizingatia ushauri huu hakutakuwa na haja ya kujenga bypass (mchepuko) ya kuondoa foleni ya Buguruni mataa.
Tujadili.