Nimeshindwa kununua TV ninayoihitaji Kariakoo

monotheist

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
720
943
Wiki iliyopita nilienda kkoo kwa lengo la kununua tv hasa hisense smart 43 inch na nilizunguka maduka mengi ya pale kkoo ila na huwa napenda kuuliza maswali ya kutosha kabla sijanunua bidhaa husika lakini majibu niliyokutana nayo kutoka kwa wauzaji yanashangaza.

Kutokana na maswali niliyokuwa nawauliza wauzaji wengi wao hawakunishauri ninunue hisense wanadai kwamba tutakuja kusumbuana kwenye warranty kwani nyingi ni copy na pia si imara wakanambia original zinapatikana posta zinakuwa na maandishi meusi na sema gharama yao ni kubwa mno.

Nilionyeshwa tv mbalimbali kama alitop, solamax, rising, goodvision ambazo unaweza kupata smart 43 inch kwa tsh 450,000 wanadai zinaweza kudumu kuliko hata hizo hisense ambazo copy zimejaa Kariakoo.

Je, mnanishauri nini kuhusu tv bajet ni 630k sasa hapo kama nikichukua solamax au nyingine zinazofanana na hizo si pesa nyingi inabaki.
 
Ongeza mapene kanunua hizo og, kuna faida nyingi kama unajipend tafuta kitu Og hata million na ushee ...Hayo ya kichini hayana mzuka picha zitaanza kupauka kabisa Tv utaona nyeupe kwa mwali hata mtu mweusi unaona mweupe .
 
Wiki iliyopita nilienda kkoo kwa lengo la kununua tv hasa hisense smart 43 inch na nilizunguka maduka mengi ya pale kkoo ila na huwa napenda kuuliza maswali ya kutosha...
Una shingapi? Kuna TCL 43, 4k. Ina miezi miwili na nusu hutojutia
 
Back
Top Bottom