Moja ya Mbinu wanayotumia watu kufanya Biashara Kariakoo

United ya Ferguson

JF-Expert Member
Oct 29, 2021
2,779
5,460
Kuna msemo mmoja unasema kama unasubiri uje upate milioni mia ndio uje uaze kufanya Biashara fahamu kabisa kichwani mwako kuna uwezekano mkubwa sana Maisha yako yote ukashindwa kuja kufanya Biashara.

Mtu aliyezaliwa kufanya biashara huwa anatafuta wapi anaweza kuanzia bila kusubiri mamilioni ya mtaji kuanza kufanya Biashara. Leo ngoja nieleze mbinu Moja tu wanayotumia watu kufanya biashara kwenye soko la Kariakoo ili mtu anayehangaika aaze vipi kufanya Biashara apate mwanga kidogo wapi anaweza kuanzia.

Dalali Ndani ya Biashara unayofanya, una mtaji wa kulipa fremu au Goli na mtaji kidogo tu kwaajili ya kununua mzigo mfano unataka kuuza bidhaa za electronic zenye uhitaji wa milioni hata mia Huko ila umejitafuta umepata Hela ya Fremu na kununua Tv kama pisi kumi tu.

Usiache ingia kwenye gemu anzaa na pisi hizo hizo kumi weka dukani ikitokea mfano umepata mteja anataka Hisense nch 43 na wewe huna unakimbia kwa wafanyabiashara wengine unachukua Mali unakuja unauza unapeleka pesa ya watu, umepata mteja wa Freezer na wewe ukutani una Tv unakimbia kwa wauza freezer unamletea mteja unauza unaweka faida yako mfukoni unapeleka pesa ya watu, unataka kuuza nguo za Ndani una mtaji wa Taiti dozeni mbili tu amekuja mteja anataka dozeni kumi unakimbia kwa wauzaji wengine unachukua unampa mteja unauza unavuta faida yako unapeleka pesa ya watu.

Unataka kuuza simu za i phone una mtaji wa simu tatu tu za I phone X aza na hizo tatu ukipata mteja wa 11 pro unakimbia kwa wauzaji wengine unachukua unamuzia mteja unaweka faida yako unapeleka pesa ya watu. Kitu Cha muhimu zaidi kwenye hii Mbinu lazima uwe na ukaribu sana na wafanyabiashara wanaofanya biashara kama yako hasa wale wakubwa pia uwe muaminifu sana pia duka lako lisiwe mbali na wafanyabiashara wazeko ili uweze kusave mda wa mteja akili kichwani mwako.

Nihitimishe kwa kusema hiyo ni mbinu Moja wapo tu ila Mbinu zipo Nyingi sana ambapo mtu mwenyewe uhitaji anaweza kuingia kkoo akajifunza mwenyewe nakupata ujuzi zaidi Na zaidi.
 
Mfano mzuri sana

Kuna siku nilipita pale uhuru nikataka nunua kamba za viatu za rangi fulani hivi jamaa akawa Hana.

Akaniambia tulia akazama kati huko akaja niletea kamba nazotaka.

Naamini zile kamba alizipata kwa Bei ya chini huko kati Mimi aianiuzia kwa kwa Bei yake
 
Back
Top Bottom