mkada
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 1,200
- 908
Nimebahatika kuwa na mke mzuri sana,ni mchanganyiko wa mnyamwezi na muhaya,ni mzuri na ana tabia nzuri sana,tumebahatika watoto wawili,na ndoa yetu ina miaka sita sasa,nina kazi nzuri na nakaa nyumba ya kupanga ya nyumba vitatu Changanyikeni.Kwa kifupi nampenda mke wangu.Kinachoniuma ni kuwa kila nikitoka nje,barabarani,au sehemu za starehe siishi kutamani wanawake wengine na mara kadhaa wale wanaonikubalia nimelala nao guest,achilia mbali gharama ninazotumia kwenye starehe,mke wangu ananipenda sana,na mimi nampenda pia,sipo tayari kumuacha na niko tayari kuilinda ndoa yetu kwa gharama yeyote ile
.huwa najuta sana kumsaliti kwani hastahili haya niyayomfanyia,kinachonisikitisha ni kuwa siwezi acha kuendelea kumsaliti.Najiuliza huu ni upepo tu utapita au ni nn?au ndo madhara ya kuwa bookish shule mpaka nikasahau starehe...naomba msaada.

