Ndugu zanguni wanajukwaa la jamiiforum, Salaam.
Ni masikitiko yangu makubwa sana kwamba Mtanzania yoyote akipoteza cheti chochote kiwe cha kidato cha nne au cha sita au chochote kinachotolewa na baraza la mitahani (NECTA) eti huna fursa ya kupata nakala ya cheti husika.
Imenishangaza pale wanapokuwambia ukatangaze kwenye gazeti la serikali kwa maana ya kwamba ukishatangaza unapewa a dublicate copy kama polisi wanavyotoa leseni mara inapopotez!!
Sasa najiuliza, ni watanzania wangapi wanakosa fursa ya kuajiriwa kwa sababu tu ya sera za serikali yetu kuwa mbovu. Ni kikwazo gani kinachofanya mtanzania asiwe na haki ya kupata nakala ya cheti chake ili aendelee kuchangamkia fursa za ajira zinazotoka kuliko kuwekewa kikwazo tena na serikali yake isiyo na ajira za kutosha.
Mbaya zaidi ata kama una transcript TUME YA AJIRA hawaiitaji kwa ajili ya kukupa ajira maana wanatangaza kabisa kuwa hawakubali transcript kama huna cheti husika.
Watanzania wengi wako njia panda ndugu zanguni na si mimi peke yangu naomba nipatiwe mwarobaini wa hili swala kama maandamano nielewe, na kama ni kuuwa pia nijue. Kama si vyote hivi basi naomba Wizara na Waziri husika aangalie hili swala kwa undani kwa sababu ukienda baraza la mitahani wanasema wizara ndiyo inahusika na sera kwa hiyo wanafuata taratibu zilizowekwa na wizara. Jamani wiraza na watu na baraza la mitahani ni watu pi siyo majengo useme hayawezi kufanya mabadiliko, tunapata shida viongozi wetu tunaomba mtusaidie, siyo sisi tumetaka vyeti kupotea. Chonde chonde waheshimiwa warekebisha sera naomba mliangalie hili kwa undani vinginevyo kunaongeza kundi la wasio na ajira bila sababu za msingi kabisa.
Naomba msaada wenu wana jukwaa nimwone nani anisaidie??