Nimeponea chupuchupu kuuawa kwa mchepuko

Nimeponea chupuchupu kuuawa kwa mchepuko

Pole sana mpambanaji. Tatizo hamsomi alama za nyakati, wengi wenu mnakufa kizembe sana asee
 
Mtakufa siku si zenu asee. Hiki kingekuwa kifo cha kizembe kabisa
 
Jombaa baada ya wiki nitajua nifanye nini lakni kwa sasa bado nabawabu
 
Vp demu wako ameacha kukuonyesha mapsnzi mubashara mpaka uende kwa mchepuko!??
 
Aseee...tulia njia kuu mkuu,mimi mwenzio naona ubahili sana kuhudumia mwanamke wa nje aisee....wanafilisi na kuchelewesha maendeleo sana hao,Acha kupoteza muda nao,komaa na maisha tu.
Aisee umenena vema sana,ukitaka kujutia maisha yako wakati wa uzee basi kuwa mtu wa kuendekeza wanawake wengi,(michepuko,)wanatia umasikini uliotukuka!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba Jasmine siku nyingine usipende kushika shika simu ya mkeo kama umeshagundua kuwa hataki.
Lakini mkiwa katika hatua hiyo, ujue kabisa hakuna mapenzi tena kati yenu. Ni maslahi tu ya upande mmoja ndio yanawaweka pamoja.
 
Baba Jasmine siku nyingine usipende kushika shika simu ya mkeo kama umeshagundua kuwa hataki.
Lakini mkiwa katika hatua hiyo, ujue kabisa hakuna mapenzi tena kati yenu. Ni maslahi tu ya upande mmoja ndio yanawaweka pamoja.
mkuu kweli kabisa jana ndio nimeamini hilo
 
Salaam wadau

Naingia kwenye habari moja kwa moja nina mchepuko ambao nimepata naye mtoto mmoja wa kike sasa jana jioni kama kawaida lazima nipite na kuwajulia hali na kuwaachia chochote kitu cha wiki, sasa nilipofika nikakuta mama Jasmini amekwenda kuoga na pale ndani yupo mdogo wake na mtoto Jasmini.

Mara simu ikaanza kuita nikaishika na kuiangalia naona imeandikwa jina driver 1,
ikafanya kama missed call 3 ghafla nikaona sms nipo pale makutano place nikaiweka simu pale pale kitandani huku roho inakwenda mbio

Bibie akaingia akasalimia macho yake yakalenga kwenye simu ghafla namuona amebadilika sura...anauliza nani amegusa hii simu yule mdogo wake akasema shemeji..nani amekwambia ushike hii simu umeona nini haya nipe ujumbe uliyouona humu naona umeshasoma.

Nikaona huyu ananichezea nikamfuata..akaniambia ukinigusa tu nitakukata visu hapa sasa nikaona ni habari nyingine anaingia msikitini na viatu nikamwambia yule mdogo wake atoke nje

Nikamfunua moja kidevu, akapiga nduru ananiuaaaa nikafunika nikafungua mlango duuuh wapangaji washaanza kutoka, kutahamaki nyuma nasikia kimbia atakuua naangalia nyuma namuona ana kisu mkononi ikabidi nikimbie kosa kubwa mimi huwa naingia pale kwa siri akapiga kelele mwiziiiiii nilichokipata hata tabu kueleza mpaka wanafika kuamulia wale wapangaji nimepoteza kila kitu na nimevimba.

Kwa hasira amerudi kule nyumbani bodaboda yangu ameibonda na mawe wala haitamaniki nikaichukua na kumuachia mjumbe pale ili Jumatatu niipeleke kwa fundi na mimi nikaelekea polisi kuchukua karatasi kwenda hospital, nyumbani nishasema nimevamiwa na watu walionifananisha kama nimewaibia pikipiki.

Nilichoamua ni kusamehe mtoto na ubalozi nimeufunga rasmi
Mchepuko sio dili, ni kujiingiza kwenye chain mpya ya mapenzi hasa pale mchepuko unapo jua kua we uwezi kuuoa na unafamilia yako. Ungefanywa vibaya.
 
Back
Top Bottom