Ugonjwa wa kuhara damu

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,575
44,807
Huu ni ugonjwa unaotokana na mchafuko wa tumbo ambao unasababisha kuharisha kinyesi chenye damu au kamasi au vyote kwa pamoja. Ugonjwa huu usipotibika haraka unaweza kusababisha kifo kutokana na mwili kupoteza maji, virutubisho na madini kwa wingi.

Dalili zake

1. Kuhara kinyesi chenye damu au kamasi

2. Kutapika damu

3. Mwili kuchoka sana

4. Kutokuwa na hamu ya kula

5. Maumivu ya tumbo

Visababishi vya ugonjwa huu

Vimelea vya bakteria, prozotoa, minyoo, kemikali au virusi ndio visababishi vikuu vya huu ugonjwa.

Kuhara kunakosababishwa na bakteria bacillus kunaitwa bacillary dysentery, na kule kwa amiba kunaitwa amoebic dysentery.

Tiba yake

Ugonjwa huu unasababisha mwili kupoteza maji, virutubisho na madini kwa wingi, hivyo;

1. Kunywa maji mengi yenye mchanganyiko wa kiwango kidogo sana cha chumvi pamoja na sukari ili kurudisha maji, virutubisho na madini vilivyopotea mwilini.

2. Nenda kituo cha afya au Maabara iliyo karibu ili kupata vipimo.

3. Kama itabainika ni ugonjwa kwa kuhara wa kawaida basi dawa zinazofaa kuutibu ni Ciprofloxacin kwa bakteria au Flagyl(Metronidazole) au Nor-T ambayo ni mseto wa dawa mbili (Norfloxacin na Tinidazole) kwa amiba na bakteria kwa muda wa siku tano hadi kumi.

ANGALIZO: SIYO KILA MTU MZIMA ANAYEPATA HIZO DALILI HAPO JUU NI DYSENTERY (MCHAFUKO WA TUMBO), PIA ZINAWEZA KUWA DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO. NI VYEMA UKAPATA USHAURI KABLA YA KUTUMIA DAWA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom