Nimepona tena baada ya kuweka mkono na kukemea ugonjwa!

Nimepona tena baada ya kuweka mkono na kukemea ugonjwa!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Kama kawa, nimekuwa nikiwaletea habari za kweli kabisa, bila kuchanganya hata tone la uongo. Leo tena napenda kuwahabarisha kuwa jana, ghafla tu, nilipata maumivu makali sana katika sikio langu la kushoto. Ni maumivu makali yaliyoenea mpaka upande wa juu wa kichwa changu. Kama hiyo haitoshi, nilihisi pia maumivu makali hata wakati wa kutafuna na kumeza chakula.

Dalili za ugonjwa huo zinafanana na za ugonjwa wa Otitis interna (inner ear infection / labyrinthitis).

Mimi, nikiugua, kimbilio langu la kwanza ni Yesu, kwakuwa uponyaji wa Yesu ni free of charge na mara nyingi ni instant healing. Mtu akikuambia utoe pesa kwanza ndio akuombee, mkimbie haraka, huyo ni tapeli mkubwa.

Hivyo nilifanya kama Yesu alivyoagiza: niliweka mkono wangu sehemu inayouma, nikakemea ugonjwa huo na kuuamuru utoke kwa Jina la Yesu. Niliendelea kumuomba Mungu aniponye na kuahidi kwamba nikipona, nitawashuhudia watu muujiza huo mkubwa.

Hivi ninavyoandika uzi huu, sisikii hata chembe ya maumivu. Hakika kuokoka na kuishi na Yesu ni kutamu.
 
Mk 16:17-18
Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
 
Mambo ma mchungaji
 
Mtu akikuambia utoe pesa kwanza ndio akuombee, mkimbie haraka, huyo ni tapeli mkubwa.
Wale wanaosema utoe sadaka ya kujikataa ili wakuombee, wakisikia hiyo kauli itakuwaje
 
Kwanini walokole wengi siyo wazima kichwani?
Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulubiwa? (Wagalatia 3:1-14)
 
Uende muhimbili mochwari ukafufue maiti pasta..!!
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulubiwa? (Wagalatia 3:1-14)
Ndugu zako wakuwahi na wakusimamie umeze dozi unaweza kupona hawajachelewa sana
 
So kitaalamu sibitali zote zifungwe?
Zitafungwaje zote wakati humu kuna rundo la watu kama kina Lucha wasioamini miujiza.
Acha sisi tuendelee ku-save pesa za matibabu. Wenye mapesa waache tu waende hata huko AIIMS, New Delhi
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Uende muhimbili mochwari ukafufue maiti pasta..!!
Waliokufa katika dhambi hawawezi kufufuka sasa, mpaka siku ya hukumu. Ukiishaingia kuzimu, hutoki humo. Kasome habari ya Tajiri na Lazaro. (Luka 16:23; Waebrania 9:27)
 
Ndugu zako wakuwahi na wakusimamie umeze dozi unaweza kupona hawajachelewa sana
Expert member tangu 2018 huwezi kuandika hata paragraph moja yenye hoja zilizoenda shule. Una-copy na ku-paste kauli zilezile. Duh
 
Kwani wewe utaishi milele? Anza kuzihesabu siku zako zilizobaki za kuishi duniani. Sio nyingi. Sekunde ya kwanza tu baada ya kukata moto, ndio utatambua kwamba mada zangu hazikuwa porojo. For in that infinitesimal interstice between temporal cessation and eternal adjudication, the so-called trivialities you disdain metamorphose into transcendental verities of ineluctable consequence. Your derision today shall be eclipsed by an incontrovertible realization, that divine truth is neither frivolous nor negotiable.
 
Expert member tangu 2018 huwezi kuandika hata paragraph moja yenye hoja zilizoenda shule. Una-copy na ku-paste kauli zilezile. Duh
Wakikuwahi utapona ila wanavyochelewa utafungiwa mirembe
 
Wakikuwahi utapona ila wanavyochelewa utafungiwa mirembe
Huu uzi unakuhusu. Usome kwa makini
 
Kwani wewe utaishi milele? Anza kuzihesabu siku zako zilizobaki za kuishi duniani. Sio nyingi. Sekunde ya kwanza tu baada ya kukata moto, ndio utatambua kwamba mada zangu hazikuwa porojo. For in that infinitesimal interstice between temporal cessation and eternal adjudication, the so-called trivialities you disdain metamorphose into transcendental verities of ineluctable consequence. Your derision today shall be eclipsed by an incontrovertible realization, that divine truth is neither frivolous nor negotiable.
Kufa nitakufa hata leo. Lakini nasema hiviii hizo ni porojo kama nyingine.
 
Back
Top Bottom