Nimepigwa chabo na mama mwenye nyumba leo asubuhi

Kitoabu

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
10,658
11,604
Katika hali nisiyoitarajia leo nimegongana uso kwa uso na mama mwenye nyumba wangu akiwa dirishani kwangu, bila shaka alikua akinipiga chabo.

Tukio hilo limenitokea mchana huu muda mchache niandikapo hapa.

Nilikua nimetoka kuoga tayari kwa kwenda kutembelea familia

Nikiwa katikati ya kupaka lotion nikiwa uchi kama nilivyo zaliwa ghafla niliona kivuli kikizama chini upande wa dirishani kwangu sikuwa na wasi kwa kuwa hapa home hakuna tabia ya wizi, lakini nivyokuwa naendelea na zoezi la kuchana nywele (nikiwa bado uchi) nilimshuhudia mama mwenye nyumba kupitia kwenye kioo akiwa kajibanza dirishani akinila chabo.

Nimefedheheka sana kwa kuwa nina imani kanichambua mwili wote hajaacha kitu.

Cha ajabu huyu mama ni mtu mwenye heshima na maadili mema hata watoto wake wana tabia nzuri sana.

Isitoshe ni mlokole mzuri tu.

Hapa nilipo niko chumbani hata kutoka nje naona aibu.

Nafikiria kwenda kwa mjumbe kumpelekea malalamiko yangu lakini tatizo nikiamuliwa nihame itakuwaje?

Kuhama hama majumba nimechoka naona nawatajirisha madalali tu.

Dah! Aibu gani hii?
 
Back
Top Bottom