Nimepeleka zawadi: Mume kaichoma moto! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimepeleka zawadi: Mume kaichoma moto!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ndyoko, Feb 12, 2012.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Jamani hiki ni kisa cha kweli kimetokea masaa 48 yalopita. Ishu yenyewe iko hivi:-

  Nilikuwa naishi kwenye nyumba pamoja na mpangaji mwenzangu huko mkoani manyara wilaya ya kiteto. Kwa bahati nzuri nikahama kwenda kuishi kwa nyumba ya ofisi. wakati nahama, mke wa mpangaji mwenzangu alikuwa mjamzito na mwezi ulopita kajifungua mtoto.

  Sasa nilipopata taarifa za huyo mke wa mpangaji mwenzangu kupata mtoto nikaona sio mbaya niende kumpongeza-nikiamini ni jambo jema kadiri ya mila zetu waafrika, si mnajua tena. Kwa bahati nzuri nilienda muda ambao na mume wa huyo mzazi alikuwepo. Nikapiga stori na baadae nikaamua kumpa mzazi nguo-niliona nimpe zawadi ya kitenge kwa ajili ya kukafunika kachanga-na nikaondoka zangu.

  Kumbe baada ya mimi kuondoka, huko nyuma nikaacha kivumbi. Mume akahoji iweje niende pale na kutoa zawadi? Kwa nini nilifika kwake badala ya kwenda kwa mwenye nyumba? Mwanaume akaamua kuchukua hicho kitenge na kukichoma moto. Wakati zogo linaendelea mwenye nyumba aliwasikia na akaamua kupata full details. Na leo hii, tarehe 12/02/2012 saa 6 mchana huu, akaamua anitaarifu kuhusu issue hii yote akihofia kwa isije nikaenda pale kumbe jamaa ana 'machungu' na mimi.

  Binafsi nimefadhaika sana na suala hili ukizingatia nilikaa nao kwa miaka miwili na nusu, hivyo kwangu walikuwa kama ndugu, maana kuna siku, kabla sijahama, mke aliwahi kupata complications za ujauzito, walikuwa wakiwasiliana nami kumuangalia mtoto wao kwanza aliyekuwa amelala usiku wakati wao walienda hospitali.

  Jamani naomba mnieleweshe nilikosea wapi ktk mchakato wote niloulezea hapo juu. na nahisi huyu jamaa iko siku anaweza hata akaniwekea sumu kwa hisia chafu alizopata ktk stori hii yote.


   
 2. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Sio wanaume wote wenye uelewa na zawadi ila ulichokosea ni kumpa zawadi bila kupitia kwa mmewe. Hata ingekuwa ni mimi haiwezekani ukamletea zawadi mke wangu baada ya kujifungua bila mimi kunishirikisha.
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa wewe nawe kama hamkua karibu ulikua unawataka nini hao wanandoa? Wakati mwingine unatakiwa uangalie mahusiano yako na mtu mwingine ni ya karibu kiasi gani ili kuelewa limitations zako.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Mwanamke akijifungua wewe kama rafiki yake unatakiwa umpongeze mumewe (mpelekee mvinyo ama msokoto wa bhange) ama upeleke zawadi ya mtoto. Kumnunulia nguo na chakula (usije ukapeleka mchele ama nyama) ni jukumu la mumewe
  Wazo la pembeni: ama kitenge ulichonunua kilikuwa sub-standard ama kimezidi sana std yake hata mume akasirike.
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  kama ni ukaribu ulikuwa mkubwa sana ndo maana nashangaa huyo mtu ambaye tulikuwa tunakaa hata ndani kwake kuangalia mpira, ktk hili ka-behave kikengekenge
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  jumapili yangu imekamilika kikwelikweli, mweeeeeeeeee!
   
 7. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2012
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  sioni kosa ulilofanya hapo
   
 8. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Labda kwa mila zao ulikosea,bora ungenunua hata nguo za mtoto unamnunulia kitenge yeye jamaa kwa akilizake finyu kajua umemuhonga mkewe...
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  wanamme hawapendi wake zao wakizawadiwa na wanamme wemgine wanapojifungua.

  Anahisi labda na wewe ulishiriki kumuongezea maskio mtoto. Usufanye kosa hili hata siku moja.
   
 10. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  jamaa nimemdharau sana kwani tulikuwa tukishirikiana ktk mengi. nakumbuka alishawahi kuja kuomba unga, sukari na mambo mengine ya ujirani kama wapangaji. Hivyo mie wala sikuwa na wazo lolote baya ndo maana nikapeleka zawadi, na uzuri niliitoa mbele yake. Umeongelea suala la mila, hebu tuwekane wazi hapa na pengine hii ni nafasi kwa wapare kuliongelea hilo.

  Kwa kuwa jamaa ni mpare labda wapare mtueleze, kwa mila zenu mke anapojifungua ni zawadi gani apewe mke na zipi apewe mume? Nimeuliza hivi kwa sababu huyo mwanaume ni mpare na mkewe ni mnguuu!
   
 11. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Asante sana kwa ushauri wako!
   
 12. M

  MORIA JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndyoko ndugu ulikosea kidogo.. mimi siyo mpare...huna mke? ingependeza mkeo au dada yako abebe hiyo zawadi...mila na desturi zetu jamaa alitakiwa akualike yeye kwanza..sasa wewe kujitia wa kwanza uelewekaje au umekua shangazi ya mtoto 'mkaguzi'..tena umebeba waxii kabisa(mwanaume) ina maana ulijipanga/pania kabisa...siku nyingine UKIALIKWA ukipewa mtoto basi unajipapasa chochote unampa mzazi kwa niaba ya mtoto...
   
 13. k

  kajunju JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Ndyoko ulichemka.kwanza ukitaka toa zawad kwa mama wakti amejifungu lazma umtaarifu mme.ukienda na zawadi bas wote wawepo.huna mke?ungeenda na mkeo basi ndiye anayepeleka zawad nepi,vitenge na vyakula lain.yawezekana licha ya kukaa nao nyumba moja,wewe ulijenga mazoea meng na mkewe.mme tayari anakusukia kumpenda mkewe. Kuna msemo mmoja kuwa mme au mke anayemuonea wivu mwenzie anampenda sana!kumbuka ulienda kwao bila mawasliano nao na ghafla mme akakukuta.usirudie
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  well, i can now confirm kwamba ule mzigo wa malawi ulifika na uliuanika kabla ya kuutumia:rant:
   
 15. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  hauna point hapa si usinge comment.
   
 16. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #16
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  kasema ya mtoto unataka nini tena??????
   
 17. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #17
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  Kasema zawadi ya mtoto au hamjasoma????

  Kama mume akuwepo kuna shida gani na wao lazima wanatumia vitenge kutunza watoto wao?

  Huu ulikuwa ni wivu wa kijinga wa mume, ameona umehama na amefikiria mengi labda hiyo siku alikuwa amechacha sana na akaona weye unajifanya unapesa

  wewe usiwe na wasi chamuhimu wasahau hata ukikutana nao barabarani wapite, hiyo atajiuliza why na atajua umeambiwa.

  Achana nao hao, zawadi ya mtoto ameikataa akalle mbele.
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Feb 12, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa mkasa huo. Mimi sioni kosa lolote hapo!
   
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  Feb 12, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  pole sana. Mbona sijaona kosa lako hapo? Zaidi nionacho 1. Wivu wa kijinga wa mume au 2. Mume alikua akikuchekea kijino pembe, hakuwa akipenda uwepo wako ila afanyaje nyumba ya kupanga.

  Dawa ni kuyapuuzia,songa mbele
   
 20. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #20
  Feb 12, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  pole sana ndugu:unajua kila mtu na uuelewa wake...kwa kupunguza hasia na mawazo fanya km ulitoa sadaka mana mungu mwenyewe ndo wa kukuhukumu kwa ulichokifanya km ni kosa au sahihi.......ubinadam kaz ndugu yangu...sio wote wanajua kuishi na mtu.:A S embarassed:
   
Loading...