ndyoko
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,971
- 1,650
- Thread starter
- #41
Mkuu kama umekaa na watu miaka miwili kwa ukaribu huu na hujaweza kuelewa kwamba zawadi ya kitenge kwa mama mtu itazua makubwa, basi wengine ambao hawakuwepo kwenye hiyo nyumba wakiuliza mahusiano yalikuwaje huwezi kuwalaumu kwa nini hawaelewi.
Shida yangu mimi ni unajuaje kuwa kama ningepeleka nepi asingezichoma? Kama ningepeleka hela, tuseme, 10,000 au 20,000, ambayo ni zaidi ya thamani ya kitenge unajuaje kuwa asingitupa hiyo hela? Mimi nadhani hapo ni tabia ya mtu tu.
Pengine labda niseme kitu ambacho sikupenda kukiongelea hapa. Kwamba jamaa ni mtu wa totoz tena kwa sana tu, nadhani hilo ndo linalomsumbua-huenda nahisi yale anayoyatenda huenda mkewe anatendewa pia.
Alishawahi kumzushia dada wa mwenye nyumba eti anatembea na shamba boy wa mwenye nyumba, lakini cha ajabu huyo dada wa mwenye nyumba alipoondoka, jamaa ameanza kumsalandia huyo dada wa mwenye nyumba. Sasa mwenye nyumba amejua kuwa jamaa ameshaimbisha dada yake.
Ni ujinga tu mkuu, utoe zawadi ya hela, nguo za mtoto au hata ukimnunulia yeye mume nguo bado atahoji tu na pengine kuzichoma tu moto.