Nimepeleka zawadi: Mume kaichoma moto!

Ndyoko sijaona kosa lolote lako hapo ni huyo mume kuwa tu insecure nothing else. Na uelewa finyu kama wengine walivyosema. Wala usijali ulienda kwa roho safi ushamaliza kazi. Atajijua yeye na roho yake na insecurity yake mwenyewe na jinsi ya kudeal nayo. Zawadi ni zawadi tena kwa mtoto chochote kinafaa.
 
Huna kosa lakini kitenge was a wrong choice man! labda na wewe ungekuwa umeoa una mke mngeenda wawili na kitenge chenu.

Otherwise ungenunua nguo ya mtoto
 
Kwa desturi zetu watanzania, kuna taratibu nyingi zinazotofautiana za kutoa zawadi baada ya mtoto kuzaliwa. Pamoja na kwamba tunaiga utamaduni wa wengine, ni vizuri kuzijua tamaduni zetu. Kwa baadhi ya makabila, mwanamume haruhusiwe kwenda ona mtoto aliyezaliwa au kutoa zawadi.

Maranyingi wanaume hupongezana wenyewe wakikutana nje ya nyumbani. Makabila mengi, wazazi hupongezwa siku ya kutolewa mtoto, (arobaini). Na makabila mengi ni marufuku mtoto kuonekana/kupewa zawadi kama bado hajatolewa nje ili aweze kuonwa na kila mtu baada ya kukatwa kitovu na kufanyiwa mila na desturi zao.

Wewe kuwa rafiki, haikuhalalishi kuwa kimbelembele kupeleka zawadi/kumuona mtoto bila kufuata taratibu zinazotumika na jamii ya rafiki yako. Kosa ulilofanya na kutojua taratibu/mila au desturi zao.
 
Kikawaida huwa ukimbeba mtoto mchanga kwa mara yako ya kwanza toka amezaliwa huwa tunajisachi mfukoni na kutoa chochote kisha unamshikisha mkononi au unamuwekea kwenye nguo zake. Full stop!
 
Ndyoko ulichemka.kwanza ukitaka toa zawad kwa mama wakti amejifungu lazma umtaarifu mme.ukienda na zawadi bas wote wawepo.huna mke?ungeenda na mkeo basi ndiye anayepeleka zawad nepi,vitenge na vyakula lain.yawezekana licha ya kukaa nao nyumba moja,wewe ulijenga mazoea meng na mkewe.mme tayari anakusukia kumpenda mkewe. Kuna msemo mmoja kuwa mme au mke anayemuonea wivu mwenzie anampenda sana!kumbuka ulienda kwao bila mawasliano nao na ghafla mme akakukuta.usirudie
tunaishi nyumba moja, sio kusema nilifunga kiguu na nyumba. of course my wife wangu hayupo na wakati natoa zawadi, wote wawili walikuwepo. Anyway nimejua ni aina gani ya mtu niliyekuwa naishi naye. Huenda jamaa hajiamini
 
Kuna watu wengine hata kuulizia ulizia tu "mama fulani hajambo" inakuwa issue. Sembuse kitenge.

Inabidi kuwajua watu kabla ya kujiingiza katika matatizo yasiyo kichwa wala mguu.
 
Elezea vizuri. Habari yako iko nusu. Elezea huo muda mliokaa nao mahusiano yalikuwaje

miaka miwili na nusu na sisi wawili ndiyo tulikuwa wapangaji wawili pekee. Tulikwa tunashirikiana ktk mengi. Kuna wakati nilivyokuwa naenda field vijijini alikuwa akinipa hela kumnunulia mkaa, alikuwa anaomba hata mahitaji ya ndani kwangu na mengine mengi tulikuwa tukishirikiana. Hivi inakuwaje watu wazima hamuelewi nnaposema jirani mpangaji mwenzangu, au mnaishi mwezini nini? Sioni ni nini usichoelewa hapa!
 
Ungenunua zawadi ya kitoto i.e. blanketi, diapers, toys, etc. na kuwapa wazazi wote kwa pamoja.

Kumpa mke kitenge si busara hata kama hukuwa na nia mbaya.
 
pole sana. Mbona sijaona kosa lako hapo? Zaidi nionacho 1. Wivu wa kijinga wa mume au 2. Mume alikua akikuchekea kijino pembe, hakuwa akipenda uwepo wako ila afanyaje nyumba ya kupanga.

Dawa ni kuyapuuzia,songa mbele

thanx madam!
 
miaka miwili na nusu na sisi wawili ndiyo tulikuwa wapangaji wawili pekee. Tulikwa tunashirikiana ktk mengi. Kuna wakati nilivyokuwa naenda field vijijini alikuwa akinipa hela kumnunulia mkaa, alikuwa anaomba hata mahitaji ya ndani kwangu na mengine mengi tulikuwa tukishirikiana. Hivi inakuwaje watu wazima hamuelewi nnaposema jirani mpangaji mwenzangu, au mnaishi mwezini nini? Sioni ni nini usichoelewa hapa!

Mkuu kama umekaa na watu miaka miwili kwa ukaribu huu na hujaweza kuelewa kwamba zawadi ya kitenge kwa mama mtu itazua makubwa, basi wengine ambao hawakuwepo kwenye hiyo nyumba wakiuliza mahusiano yalikuwaje huwezi kuwalaumu kwa nini hawaelewi.
 
Ungenunua zawadi ya kitoto i.e. blanketi, diapers, toys, etc. na kuwapa wazazi wote kwa pamoja.

Kumpa mke kitenge si busara hata kama hukuwa na nia mbaya.

Unadhani asingechoma moto hata hivyo. mi nadhani kwa akili hii, jamaa ni mjinga sana na nadhani hata hivyo angechoma tu moto. Ndo maana watu wengine huwa hawatoi lift kwa wake za watu maana unaweza ukawa umembeba mke wa mtu halafu mwenye mali anawaona mnampita huko kwao mume anaenda kuwasha moto. sema tu wanawake huwa hawasemi wanapokutwa na ujinga huu
 
Nenda kadai zawadi yako umpelekee mzazi wako!!!

Mhhhhhhhhhh! hapana kamanda, ili mradi nimejua aina ya mtu nilokuwa nikiishi naye, basi ila namuonea huruma sana, maana kwa ujinga kama huu ataishi maisha ya shakashaka sana ktk mapenzi yake!
 
miaka miwili na nusu na sisi wawili ndiyo tulikuwa wapangaji wawili pekee. Tulikwa tunashirikiana ktk mengi. Kuna wakati nilivyokuwa naenda field vijijini alikuwa akinipa hela kumnunulia mkaa, alikuwa anaomba hata mahitaji ya ndani kwangu na mengine mengi tulikuwa tukishirikiana. Hivi inakuwaje watu wazima hamuelewi nnaposema jirani mpangaji mwenzangu, au mnaishi mwezini nini? Sioni ni nini usichoelewa hapa!

Njoore ukumbire??
 
Unadhani asingechoma moto hata hivyo. mi nadhani kwa akili hii, jamaa ni mjinga sana na nadhani hata hivyo angechoma tu moto. Ndo maana watu wengine huwa hawatoi lift kwa wake za watu maana unaweza ukawa umembeba mke wa mtu halafu mwenye mali anawaona mnampita huko kwao mume anaenda kuwasha moto. sema tu wanawake huwa hawasemi wanapokutwa na ujinga huu

Kuna tofauti kubwa sana kati ya zawadi ya kitenge kwa mama mtoto na zawadi ya sipper cups, diapers, au toys za mtoto.

Common sense...common sense Ndyoko!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom