Nimepata maono dr. Slaa kashinda urais 2015

Nimepata maono dr. Slaa kashinda urais 2015

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Posts
1,334
Reaction score
1,466
Ukiwa uchaguzi wenye kila aina ya vituko, hatimaye Dr Slaa aliibuka mshindi kwa asilimia 70 ya kura zote.

Kwa ushirikiano wa karibu sana na vyama vya NCCR, CUF, CDM waliweza kushinda kwenye mikoa ya mwanza, tabora, kagera, shinyanga, mbeya, iringa, arusha, kilimanjaro, manyara, pemba, na kugawana kura vna wahasimu wao mikoa iliyobaki.

Vijana wengi walijitokeza kupiga kura na kuipeperusha bendera ya CDM chini ya mwamvuli wa ushirikiano na vyama tajwa.

Polisi na wanajeshi kama ilivyokawaida walitumika kutisha raia, mabomu mengi sana ya machozi yalipigwa ila wananchi walisema safiri hii haiwezekani.

Dr Slaa aapishwa uraisi 2015.
 
mkuu endelea kuota. Kwa 2015 upinzani kuchukua urais ni 'skendo tu' kazaneni mchukue majimbo mengi iwezekanavyo na wards za udiwani nyingi tu!
 
wacha masikhara weye, labda rais wa yanga
 
Kila nikiuungalia ule mwamba wa Kaskazini ukishikiana na mastermind Rosttamu kwa kweli kuna kivumbi 2015
 
Hayo maono atakuwa kakuotesha mzee mtei halafu slaa utakuwa umeota ameshinda urais wa twiga star au urais wa bawacha.
 
Wengine hamjui jinsi tunavyomkubali Dr Slaa....Ukweli wake.....Unyenyekevu....Utumishi.....Uadilifu......Ukali.....kutoogopa mijadala ya wazi......pia upeo mkubwa wa mambo.....unafanya tuwe tayari kumtetea......kusimama nae kwa gharama yoyote.........bila unafiki wala kusita.....kwa maslahi ya nchi yetu tukufu.......Tanzania......
 
Wakishirikiana RICHMOND,Caspian,Dowans na IPTL ?

mkuu uchaguzi utakuwa mgumu
kwaaoni yangu ni kuwa iwepo kampeni ya watu kujiandikisha na kupiga kura.Kusema Richmond Epa n so on tutakuwa tunajidanganya wenyewe
 
ndoto hazitoi rais, ni information, critical thinking, options analysis na kujiandikisha na kupiga kura na kisha kuzilinda ndiko kunatoa rais
 
kila ndotp ina maana. hiyo yako inaonyesha ni jinsi gani dr. anaigiza kuingia ikulu. sio rahisi
 
Wewe ni nani ?

Mkuu mi ni raia tu wa tanzania,mtu mdogo tu lakini nina maono makali sana. Kwenye ukweli huwa nasema ukweli na huwa sina mihemuko ya kisiasa. Tuombe Mungu tuwepo baada ya uchaguzi 2015,tutakumbushana tu hayo niliyo comment hapo juu.
 
ndoto haiwezi kutuletea rais wa tanganyika cha msingi kujiandikisha na kurinda kura kila kituo nchi nzima
 
Back
Top Bottom