Mkuu
Kimox Kimokole na familia yako hongereni sana kwa baby boy. Kwa sisi watumishi hatutaacha hiii habari iende kimya kimya.Tafadhari soma vifungu vifuatavo viendelee kukufundisha na kukuelimisha kuhusiana na bibilia inasemaje kwa habari ya watoto wetu wadogo.
Imeandikwa katika
Mithali 22:6 "Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee." Mungu anatarajia nini kutoka kwa wazazi wanapo wakuza watoto wao Imeandikwa
Kumbukumbu la Torati 6:6-7. "Na maneno haya ninayokuamuru leo yata kuwa katika moyo wako nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii nakuyanena uketipo katika nyumba yako na utembeapo njiani na ulalapo na uondokapo."
Mungu anawatazamia wazazi wawe wavumilivu. Imeandikwa katika
Wakolosai 3:21 "Nanyi akina baba msiwachokoze watoto wenu wasije wakakata tamaa."
Nidhamu ni namna yakuonyesha upendo kwa mtoto. Imeandikwa katika
Mithali 13:24 "Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; bali ampendaye humrudi mapema."
Nidhamu njema humfunza mtoto imeandikwa
Mithali 29:15 "Fimbo na maonyo hutia hekima bali mwana aliyeachiliwa humuaibisha mamaye."
Sababu ya kumwathibu mtoto nikumfanya akuwe vema. Imeandikwa
Waefeso 6:4 "Nanyi akina baba msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana."