Nimepata ajira ya mshahara wa milioni 1.2, natafuta mke tuanze maisha

Ni aje makamanda, I hope mko poa.

Mwenzenu nilijaribu maisha baada ya kiajira changu cha kwanza lakini ikabidi nirudi home kwanza nikajipange upya, hatimae nimepata kazi ya mshahara ambayo kwa kuanzia maisha ya kifamilia sio mbaya (1.2M take home), pia nina dili kama 2 hivi zitakazonilipa mara 2 au 3 ya huu mshahara wa kazini baada ya miezi michache. Mpango wangu ni kuchukua double room ya self nzuri mwisho wa mwezi.

Kwahiyo natafuta mchumba/mke tuanze maisha from scratch, yaani kama ni chini tulale coz najua nikishachukua nyumba ntalala chini mwezi mmoja. Nataka mwanamke huyu aje kunisaidia kumanage mambo ya finance na kupangilia mji wetu vizuri, ambae atanisapoti wakati mimi naendelea na mishe zangu.

Sifa zake:
  • Apende kula vizuri. Jamani mimi napenda kula vizuri
  • Ajue kupangilia bajeti na kudili vizuri na pesa
  • Awe anaweza kunishauri
  • Mimi ni mkristo, yeye awe mkristo au muislamu mie fresh tu
  • Awe mweupe, kama sio mweupe basi awe na msambwanda/kalio mubashara, kama nalo hana basi angalau awe amesoma, kama hajasoma basi awe angalau na ajira, kama hana basi kwao wawe vizuri naamini Mungu hamnyimi mtu vyote.
Ni PM tuchat chat ndio tupeane namba, kisha tukutane eneo la wazi k.v. mgahawa n.k.
Niko tayal

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakupiga bao me sina elimu zaidi ya kujua kisoma na kuandika lakini nacheza kibati cha elfu 30 kwa siku kwa mwezi laki 9 sikatwi kodi afu apo nshawaachia hom elf 10 kla siku hacha kujisifia iyo sio hela

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahhaahhaa... meseji sent! Na promo uliojipigia naimani watakufuata inbox

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
 
Hizi ID mpya sio za kuamini, umetoswa ukituma meseji hazijibiwi umeamua uje na njia mbadala, na hapa umewashika

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
 
joseverest nimekulindia nafasi yako, uje ili tumshauri pamoja

dogo hiyo hela ndogo sana na sana..

gross ya 1.2m net yake ni kama laki 8 na nusu hivi..

tena hapo bodi ya mikopo kama hawakudai.

haya sas tuchekeche laki 8 hiyo ulipe kodi, nauli, msosi, umeme, maji etc..

hiyo hela hapo ni kama unaingiza elfu 27 kwa siku
ambapo hata muuza chips au muosha magari na kindoo tu anakuzidi..

nakushauri swala la kuoa au kuishi na mwanamke weka pembeni kabisa.. fanya saving kisha invest na kuinvest na kuinvest tena.. after 5 yrs ndio usake kimwana..

kipindi hiki tafuta girlfriend tu uwe mnakutana weekend..
Umetisha mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hicho kigezo cha chini kabisa naon weng ndo kinawapeleka chaka ila utapata boy subiria tu
 
Mzee gross ya 1.2M unatafuta mke? Next post tutasikia umepatwa na pressure tukuombee..
 
Ni aje makamanda, I hope mko poa.

Mwenzenu nilijaribu maisha baada ya kiajira changu cha kwanza lakini ikabidi nirudi home kwanza nikajipange upya, hatimae nimepata kazi ya mshahara ambayo kwa kuanzia maisha ya kifamilia sio mbaya (1.2M take home), pia nina dili kama 2 hivi zitakazonilipa mara 2 au 3 ya huu mshahara wa kazini baada ya miezi michache. Mpango wangu ni kuchukua double room ya self nzuri mwisho wa mwezi.

Kwahiyo natafuta mchumba/mke tuanze maisha from scratch, yaani kama ni chini tulale coz najua nikishachukua nyumba ntalala chini mwezi mmoja. Nataka mwanamke huyu aje kunisaidia kumanage mambo ya finance na kupangilia mji wetu vizuri, ambae atanisapoti wakati mimi naendelea na mishe zangu.

Sifa zake:
  • Apende kula vizuri. Jamani mimi napenda kula vizuri
  • Ajue kupangilia bajeti na kudili vizuri na pesa
  • Awe anaweza kunishauri
  • Mimi ni mkristo, yeye awe mkristo au muislamu mie fresh tu
  • Awe mweupe, kama sio mweupe basi awe na msambwanda/kalio mubashara, kama nalo hana basi angalau awe amesoma, kama hajasoma basi awe angalau na ajira, kama hana basi kwao wawe vizuri naamini Mungu hamnyimi mtu vyote.
Ni PM tuchat chat ndio tupeane namba, kisha tukutane eneo la wazi k.v. mgahawa n.k.
Wewe ni mtu wa ajabu sana yaani unaoa kwa sababu ya mshahara wa 1.2m jee mkataba wa kazi hiyo ukiisha utamuacha?
 
Dunia inaenda kasi sana, ambapo maana ya ndoa imebadilishwa kabisa! Unaweza kuona ni kwanini ndoa za vijana wengi hivi sasa zinavunja usiku wa honeymoon au siku ya birthday ya kwanza tangu mfunge ndoa.
Natamani vijana ambao hawajaingia kwenye ndoa wakatafakari vitu zaidi ya hivi. Upendo ni jambo kubwa na sio mali. Aisee tunajenga ndoa kwenye misingi ya mali ulizonazo, sasa hii ni ndoa au unatafuta business partner au unatafuta make/mume. Umewahi kujiuliza siku ukiondolewa job kwa kuwa na vyeti feki utaishije na huyu uliyemleta kwa sababu ya mshahara?
Umewahi kujiuliza ikitokea ukaugua kwa mwaka mzima bila kwenda kazini, je huyu unayemleta kwa sababu ya mshahara au makalio yake au kwa sababu ni handsome boy/man atakuwepo muda wote huo?
Umepata kilema na makalio hayaonekani je bado utakuwa na thamani kwa Hugo handsome boy wako?
Kama unatafuta mume/mke basi ni vyema sifa za makalio, weupe, hips, uhendisamu vikawa sio sehemu. Ndoa inaanza siku mnapotoka honeymoon, siku mkeo anaamka bila makeup, siku mkeo anaamka hajatengeneza makalio yake vzr, siku mumeo anarudi amefukuzwa kazi, siku mumeo amepata ulemavu wa kudumu, siku ambapo daktari anawaambia kuwa kwa hali ya mmoja wenu hamuwezi kupata mtoto.
Ndoa inaendelea siku ambapo unamfumania mkeo/mumeo, siku unakuja mama na mkeo kuna ugomvi n.k.
Tunapaswa kutibu mambo mengi kwenye vichwa vyetu vijana wa kike na kiume la sivyo kila siku itakuwa ni kuoa na kuachika mwisho wa siku hakuna unachofurahia katika maisha. Unabaki wewe ni wa kutimiwa tu na watu tofauti na tukichoka hakuna hata anayekuita hata kidate na kiben ten hakuna hata kama ni bure.
 
1.2m tu? Ni kama vile umeona hiyo hela ni kubwa sana. Wenzio wanapata mshahara 150,000 kwa mwenzi walishaoa wana watoto na maisha yanasonga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom