ndandawamalenja
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 548
- 664
Naishi Dar. Wakati flani nilienda A-town kikazi, demu wangu akanifuata. Kwa mara ya kwanza kwenye uhusiano wetu (wa mwaka mmoja) tuka-sex kavukavu. Wiki moja baadae demu akaniambia ana mimba. Nilikuwa nataka sana mtoto nikamwambia haina shida tulee tu. Nikamhamisha kwa ndugu yake alikokuwa anakaa nikampangishia chumba. Mtoto alipozaliwa nilipomwangalia tu machale yakaanza kunicheza kuwa nimepewa mtoto wa mtu. Sasa miaka miwili baadae, siku moja nimekaa hivi na mshikaji (ambaye hajui mahusiano yetu) tunapiga stori akapita huyu mzazi mwenzangu feki. Hakuniona, ile nataka kumwita jamaa akaniuliza unamfahamu huyo demu? Nikamwambia amewahi kuishi jirani na mimi, namfahamu. Akaniambia, huyu si amezaa na mzee fulani? (Simtaji). Kidogo nizimie. Mtoto amefanana sana na huyo mzee, namfahamu vizuri na huwa naongea naye mara kwa mara. Nikashangaa siku zote nimeshindwa vipi kujua hilo? Hapo anapoishi huyo mzazi mwenzangu feki (najua mimi ndio feki, ila ngoja nimwite yeye hivo) huwa naenda mara mojamoja. Siku chache baada ya tukio lile nikatia timu kwa mema tu, nikitaka kumuuliza. Lakini nikapatwa na hasira, nikaona si busara kuuliza. Nikaondoka zangu. Kesho yake asubuhi nikapata msg kutoka namba nisiyoijua. Mwenye namba hiyo akajitambulisha kama jirani wa mzazi mwenzangu. Akanitaarifu kuwa ananionea huruma na ameshindwa kujizuia, eti watu wananichora ninavoenda pale nikiamini mimi ndio baba wa mtoto wakati wao wanajua kuwa mtoto siyo wangu baba ake wa kweli huwa anaenda pale na anafanana sana na mtoto. Kama siamini niende siku hiyo mchana nitamkuta sehemu fulani ambako wataenda na huyo mama mtoto. Sikwenda kwa sababu ya maumivu.(ya roho). Nilipomuuliza huyo mama mtoto kwa kumpa ushahidi akanipa stori ambayo ikanithibitishia kuwa huyo mtoto siyo wangu. Japo yeye anakomaa kuwa mtoto ni wangu, lakini alikubali kuwa aliwahi kutembea na hiyo mzee mara moja mwezi uleule alioshika mimba, eti mazingira ndio yaliyomlazimisha. Sasa namwonea huruma sana kwa sababu huyo mzee hamsaidii chochote, kwa sababu nikimwachaga muda mrefu bila hela huwa namkuta ana hali mbaya mno. Na yeye huwa ananiambia nikisitisha huduma itabidi arudi bush. Halafu kitu kingine nakapenda sana katoto japo si kangu. Na tatu nina hasira sana na demu kwa kunidanganya kwa miaka miwili mizima. Nalipa kodi (tena nikichelewa kidogo mwenye nyumba anawakaga), nampa mshiko wa matumizi, na vitu vingine halafu kumbe alinifanya *****? Nimfanyeje jamani? Hata sasa hivi kanipigia simu kunibembeleza!