Kang
JF-Expert Member
- Jun 24, 2008
- 5,692
- 2,576
Nimefanikiwa kununua laptop kutoka Amazon.com kwa kutumia hatua zifuatazo natumaini itawasaidia wengine.
Amazon hawatumi bidhaa nyingi Tanzania hasa electronics so unahitaji kampuni ya shipping itakayokutumia vitu vyako kutoka US kuja bongo kuna kampuni nyingi zinafanya hili mimi nilitumia USGoBuy.com kwa kuwa ndo niliona ina bei ndogo na unaweza kutumia USPS (Posta ya Marekani) sio lazima utumie DHL/UPS ambazo zina gharama zaidi.
Utahitaji kadi ya Visa/MasterCard inayofanya kazi mtandaoni.
Hatua
Amazon hawatumi bidhaa nyingi Tanzania hasa electronics so unahitaji kampuni ya shipping itakayokutumia vitu vyako kutoka US kuja bongo kuna kampuni nyingi zinafanya hili mimi nilitumia USGoBuy.com kwa kuwa ndo niliona ina bei ndogo na unaweza kutumia USPS (Posta ya Marekani) sio lazima utumie DHL/UPS ambazo zina gharama zaidi.
Utahitaji kadi ya Visa/MasterCard inayofanya kazi mtandaoni.
Hatua
- Nenda USGOBuy.com na fungua account hauhitaji kulipa kwa sasa.
- Watakupa address ya marekani hii ndo utaitumia wakati unanunua Amazon.
- Nenda Amazon weka vitu unavyotaka kununua kwenye kikapu, lipia kwa kutumia kadi kisha wakati wa kuweka address weka address uliyopewa na USGoBuy ya marekani, shipping ni bure Amazon->USGoBuy.
- Unaweza kununua duka lolote sio Amazon tu kisha ukatuma vitu vyote address yako ya USGoBuy wao watavishika kwa hadi siku 60 bila gharama na wanaweza kuviunga kwenye mzigo mmoja na kupunguza size weight ya mzigo kwa kutupa mabox yasiyohitajika.
- Subiri vitu vyako vifike USGoBuy kutoka Amazon.
- Vitu vikifika utataarifiwa na utaweza kuona kupitia tovuti ya USGoBuy. Pia kuna huduma ya kupigiwa picha hii ina gharama $5.
- Ukiwa tayari kuvituma vitu kuja bongo utajaza anuani yako ya TZ pamoja na kampuni unayotaka kutumia kuna DHL, UPS, USPS.
- Watakuhesabia gharama kutokana na uzito na size ya mzigo.
- Unaweza kulipia kwa kadi au PayPal.
- USPS ndo posta ya Marekani na ndio inagharama nafuu na nadhani ndo pekee wanaokubali PO Box.
- Jihadhari na kampuni za DHL/UPS hawa wanakuwa na fee za ziada kuukomboa mzigo ukifika bongo juu ya kodi "Shiping and Handling charges".
- Ukichagua USPS Priority mzigo unakuja kwa EMS so una tracking all the way.
- USGoBuy watakuomba ujaze gharama ya mizigo yako, hii ndo itaandikwa juu ya boxi, watakuuliza kama unataka original invoice za amazon ziwekwe kwenye boxi au waitupe.
- Mzigo ukifika bongo utapigwa kwanza 1,500 gharama za posta.
- Halafu kuna VAT 18% na kodi ya reli 1.5%
- Kwa laptop ndo hizo tu kodi, kwa vitu vingine kuna kodi zaidi ambazo sizijui kwa bahati mbaya.
- Pale posta wanapokokotoa kodi wanataka ile original invoice ya Amazon otherwise wanazama mtandaoni wanaanza kutafuta bei wenyewe, maelewano juu yako.