Nimenunua kitu ebay, nitakipata bila tracking number?

pozzyfaza

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
1,453
268
Samahani wakuu kuna bidhaa nimenunua ebay na nimeilipia. Jana ebay wamenitumia email. Kuwa bidhaa iko shipped to ....wakaweka namba yangu ya simu. Ila sijajua jinsi ya kuitrack na wala sijapata tracking number. Je huu mzigo nitaupata kweli
 
Utaupata kama address iliyowekwa ni sahihi. Sio bidhaa zote huwa wanatoa tracking number mkuu, inategemeana na seller. Kuwa na subira mzigo utafika mkuu
 
Angalia kwenye hiyo email yao wanaweza kuwa wameweka order number au tracking number, kama wameziweka, zichukue hizo namba kisha fungua website yao tafuta sehemu ya kutrack nadhani itakuwepo kisha ingiza hizo namba zitakuonyesha hatua za kufika kwa bidhaa yako. Hata hivyo watakutumia mzigo wako
 
Na pia sio items zote wanatoa tracking no#, bidhaa nyingi zinazoanzia $30 na kuendelea ndizo huwa wanatoa TN (uhakika).
 
Kwaiyo chini ya hapo hawatoi
Kwa uzoefu ni hivyo, nimeshaagiza vitu vingi tu, na zote nilizopatiwa TN zilikua above $30, na kuna moja ambayo ilikuwa below $30 nililipia kama $6 hivi kwa ajili ya TN.
 
Kwa uzoefu ni hivyo, nimeshaagiza vitu vingi tu, na zote nilizopatiwa TN zilikua above $30, na kuna moja ambayo ilikuwa below $30 nililipia kama $6 hivi kwa ajili ya TN.

Sio Rule of thumb hiyo!

Bidhaa za Kutoka China/HongKong nyingi wana ship bila track number

Last time nimenunua multimedia player kwa above 50$ hawajatoa Track number

Postal services nyingi za US au UK ndo naona wanatoa track number
 
Usiwe na wasi kama unatumia Box na mzigo watoka US/UK kacheki posta week ya tatu
Kama ni Uchina na nyinginezo fanya check baada ya 4 weeks

Ila kwa average unaitaji subiri 30days walau
Mkuu ukinunua electronic devices kutoka ebay wanakutumia moja kwa moja kwenye sanduku lako la posta? Na vipi bidhaa ikishafika je kuna kodi unayotakiwa kulipa tra?
 
kuna sehemu posta pa kupokelea mizigo isio na sanduku usiwe na wasiwasi ukifika watakutumia msg posta utaenda kuuchukua wanachaji 1,000 ya kuchukulia mzigo na haina kodi unless waamue tu wenyewe.
 
Unaweza Kupokea Mzigo wako bila Box provided utoe namba ya simu ukifika pale posta mpya wanakutumia meseji uufate.
 
Mkuu ukinunua electronic devices kutoka ebay wanakutumia moja kwa moja kwenye sanduku lako la posta? Na vipi bidhaa ikishafika je kuna kodi unayotakiwa kulipa tra?

Huu wimbo umeibwa sana
Unaposema Electronic device sijui umelenga nini?
Nikiagiza e.g Smart watch itashindwa vipi kufika kwa njia ya Posta?
Na kwa nini wanitoeze ushuru wa smart watch?
Kama unaagiza vitu ambavyo sio vya Kwenda kuuza e.g 1 device ni vigumu wakutoeze ushuru shida itakuja pale wewe umeagiza Simu 20 hamna nanmna utakwepa ushuru hapo labda wasijue kama ni simu,Au agiza kitu ila kisiwe kitu ambacho ni kikubwa sana e.g Ukinunu TV sioni namna utakwepa ushuru hapo.

Kwa kifupi ni kwamba Mambo ya Ushuru kwa njia ya posta sio kivile sababu nyingi ni parcel za kawaida tu
 
Electronic devices ninamaanisha kitu kama simu ya mkononi, nimeuliza kwasababu kuna mtu wa dhl aliniambia ukituma kitu mfano laptop kupitia dhl kuna ushuru utatozwa. Pamoja na yeye kuniambia hivyo nilimuona hana uhakika na anachoniambia. Lakini wewe nimekuelewa vizuri. Asante sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom