Fredinho
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 971
- 1,160
Siku moja nilienda kung'oa jino kwenye hospitali moja hapa town kwetu,kwa bahati kumbe anayehusika na shughuli hiyo ni dada mmoja wa kichina nikapewa huduma nakuondoka,baada ya shughuli ile tulikutana tena kwa bahati kwenye mgahawa mmoja hapa mjini hapo ndo mazungumzo yakaanza,mazungumzo yakaanzisha uhusiano,uhusiano ambao umekuwa kama kaa la moto kwangu, kwani mi nilikuwa napita tu kumbe binti wa kichina ndo kakolea,binti anadai ndoa keshawaambia wachina wenzie kama 15 hapa mjini na wengi wao wanacheza karate.Nashindwa nimkimbieje kwani mi nimeajiriwa ajira ya kudumu mahali fulani hapa mjini kuhama ghafla siwezi.Na nikiona mazoezi ya kung fu na karate ya wale jamaa zake ndo kijasho kidogo hakiniishi kwapani.....kwa kifupi nimekwama, kumuoa siwezi,kutoroka siwezi,kumuacha naogopa kichapo cha wenzie,yaani hata sijui nifanyeje!!!