Dumelo
Senior Member
- Apr 23, 2015
- 139
- 235
Kuna Dada tunafanya nae kazi hapa katika kampuni moja ya vinywaji baridi. Kiukweli ni mwanamke niliyekua nampenda sana, lakini kila nikijaribu kumueleza hisia Zangu kwake, na kwamba nina mipango mizuri kwake, Lakini amekua akinizungusha na kuniletea Vikwazo kibao, mwisho nikaamua kuachana na nae nikaendelea na maisha yangu, Hivi karibuni nilipata Msichana tukaanzisha uhusiano, nimeshakwenda kujitambulisha kwao na hivi karibuni namtolea mahari. Sasa hiyu Dada kasikia hizi habari, jana kanipigia simu kuniuliza nikamwambia Yes! Naoa hivi karibuni. Amenuna sana, na ameniblock hata kwenye whatsap. Ofisini hanipi Hi tena. Hivi ni haki kweli katika hilo.