StudentTeacher
JF-Expert Member
- Jan 30, 2019
- 6,928
- 8,337
Unakuta ndugu hawamtaki na sababu hawana. Ukiwauliza utasikia "basi tu". Hii ishu imenikuta pia. Nilisimama kama mume kumtetea alipokuwa anaonewa bure,ingawa alianza kuota pembe na kudhani kwamba kwake sifurukuti(BIG MISTAKE). Nikamuonya kwa miaka takribani mitatu mfululizo. Akaendelea kushupaza Shingo. Siku ya siku ananipigia akastaajabu napokelea "chekundu" badala ya "cha kijani". Sasa hivi nipo kwenye mchakato wa kuoa mwanamke mwingine. Haiwezekani kuna wanawake chungu mzima wanamlilia Mungu awape mume usiku na mchana halafu kuna kiumbe kinanichukulia poa.Baada ya ndugu zangu kuonyesha wazi kuwa hawamtaki mke niliyemuoa nilikaa chini na mke wangu tukapanga jambo.
1. Tulikubaliana kujifanya tumegombana sana na kila mmoja ameridhia tuachane.
2. Tukaanza visa ili na ndugu waone sasa kuna mtoto wa shangazi yangu ambaye ni binamu wangu anakaa kwangu. Nikamwambia mke wangu amfukuze beki tatu na alafu awe hapiki wala kufanya kazi yoyote. Atafanya huyu ndugu yangu.
3. Nikamwambia wife aanze kuchelewa kurudi na kama akitaka ale huko anakofanya kazi na mimi ntajua la kufanya.
4. Wife akirudi asiongee na mtu na mm ntafanya hivyo yaan tuwe kama hatuongei kwa wiki tatu. Na mimi ntakuwa nalewa kila siku.
5. Baada ya izo wiki tatu Wife asafiri kwao Morogoro nibaki mwenyewe. Huyu ndugu yangu atawafikishia habari.
6. Sababu hawamtaki na mimi nampenda wiki mbili baada ya Wife kusafiri kwao nawaambia ndugu zangu wote kuwa nimeachana na Wife.
7.Niliomba Uamisho mkoani. Dodoma na nimepata kwa hiyo nampitia Wife Moro kimya kimya tunaenda Dodoma na hakuna pimbi atakaa afike kwangu.
8. Mambo ni mengi. Leo siku ya pili tangu tumeanza mchakato wa kuokoa ndoa yetu.
#Tairus #Bella Ciao
Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app