Nimemwambia mke wangu tuachane halafu turudiane

Nimemwambia mke wangu tuachane halafu turudiane

Nina muda kidogo kwenye ndoa, nina ndugu na mke wangu ana mawifi wa kutosha kiasi cha kwamba wakiamua kumrarua atararuka kweli ila hawawezi sababu ninamlinda na nilijifunza namna ya kuweka mipaka ya mke na dada zangu. Wote nawapenda.

Nimekulia kwenye familia ambayo mama yangu alizungukwa na mawifi na watoto wao walikulia nyumbani wakilelewa na kutunzwa na baba na mkewe ambaye kwangu ni mama. Tukio kidogo tu likitokea basi wote tunapata fundisho la madhara ya extended family kwa mke na familia yako.

YES ndugu wanaweza kuwa tatizo lakini ni ndugu, si wakati wote hawapo sahihi. Kuna mazingira ambayo ndugu huumia juu yako kuliko mkeo. Linaweza lisitokee kwako lakini mke pia anaweza akawa chanzo cha mateso yako na ndugu wakasimama kukupigania. Mwanzoni huwezi ona sababu ni kama umefungwa fulani hivi na penzi.

Ukitaka kufanikiwa kwenye maisha ya ndoa usichukue upande, mtunze mkeo na mpende ila jua mipaka ya mapenzi yako kwake na weka mipaka ya ndugu zako kwenye maisha yako kwa akili kubwa ukihakikisha kuwa na wao huwapotezi sababu una mwanamke.
 
Aliekushauri huo utopolo Ni mpumbavu.
Unamtengenezea mazingira ya kukusaliti mkeo.

Hakuna mwanamke Mwenye akili zake timamu anaweza kubali kuishi na mwanaume asiye na misimamo.

Umeonyesha udhaifu mkubwa Sana mkuu[emoji2955]
 
Kwanza nikuulize,
Uyo MKE unkwenda kuishi Naye wewe au hao ndugu zako?

Mtoa mada wee Ni KICHWA panzi, hukustahili kuoa kabisa[emoji3525]
 
Ila wanawake mna moyo, yani umekataliwa kwa ndugu wa mumeo bado tu unalazimisha [emoji23][emoji23] hiyo ndoa itapitia misukosuko mingi
Kama na mumewe wanaelewana Haina shida.
Wakishazaa watoto inakua imeisha iyo, watoto wanaunganisha familia[emoji4]
 
Wanaume wa ainayako hua wanaishi maisha magumu sana kwenye ndoa, na mwesho wenu hua mbaya sana maana mkeo ipo siku atachoka na maisha ya sanaa na atakuacha baada ya kugundua kwamba ndugu zako wana mamlaka na nafasi kubwa kwenye maisha yako kuliko yeye.
Kwakifupi huyo mama hana mume anae jielewa, na haujui jukumulako kama mwanaume aiseeeeee.....
Ivi ujue kwamba mke hufurahia pia mume atakae mlinda sikuzote haijalishi nini kimetokea, now kwako mkeo hana security
Mkewe ana hasara Sana, jamaa Ni kiazi kilichotukuka[emoji4]
 
Mleta mada bila shaka ana mtindio wa ubongo

Yaani mke wako wewe, suala la ndugu kumtaka au kitomtaka linahusiana nini na maisha yako mpaka uhangaike kufanya yote hayo?
Wanaume dhaifu Kama Hawa Sijui wanawake huwa wanawaokota wapi[emoji3525]
 
Sasa huyo ni mkeo au ni mke wa Familia?.

Mwenye mamuzi ni wewe muoaji. Mbinu uliyoitumia ni ya mzunguko sana, ni kama wewe unashindwa kutoa misimamo yako kwa ndugu zako.
We acha tu ndugu yangu hayajakukuta. Kuna koo zingine ndugu wanaweza kukutenga mpaka ukoana ulizaliwa kwa bahati mbaya ukoo huo. Yan ndugu wanaweza wakalazimisha jambo ulifanye hata kama wewe hautaki. M naona njia hiyo anayotumia mdau n sahihi
 
We acha tu ndugu yangu hayajakukuta. Kuna koo zingine ndugu wanaweza kukutenga mpaka ukoana ulizaliwa kwa bahati mbaya ukoo huo. Yan ndugu wanaweza wakalazimisha jambo ulifanye hata kama wewe hautaki. M naona njia hiyo anayotumia mdau n sahihi
Nitarudi kueleza zaidi kuna watu hawawezi nielewa...Asante sana kiongozi.
 
Tunatofautiana sana,mimi nikimpenda mwanamke na nikawa na uhakika kwamba hata matatizo hakuna kiumbe yeyote anayeweza kunishauri kuachana naye,na nikiamua kuachana na mwanamke hakuna kiumbe atashauri nimuelewe,hata vikao huwa sihudhurii maana mpaka nafikia kufanya maamzi huwa nina uhakika wa usahihi wa ninachokifanya.

Maisha yangu yapo mikononi mwangu.
 
Baada ya ndugu zangu kuonyesha wazi kuwa hawamtaki mke niliyemuoa nilikaa chini na mke wangu tukapanga jambo.

1. Tulikubaliana kujifanya tumegombana sana na kila mmoja ameridhia tuachane.

2. Tukaanza visa ili na ndugu waone sasa kuna mtoto wa shangazi yangu ambaye ni binamu wangu anakaa kwangu. Nikamwambia mke wangu amfukuze beki tatu na alafu awe hapiki wala kufanya kazi yoyote. Atafanya huyu ndugu yangu.

3. Nikamwambia wife aanze kuchelewa kurudi na kama akitaka ale huko anakofanya kazi na mimi ntajua la kufanya.

4. Wife akirudi asiongee na mtu na mm ntafanya hivyo yaan tuwe kama hatuongei kwa wiki tatu. Na mimi ntakuwa nalewa kila siku.

5. Baada ya izo wiki tatu Wife asafiri kwao Morogoro nibaki mwenyewe. Huyu ndugu yangu atawafikishia habari.

6. Sababu hawamtaki na mimi nampenda wiki mbili baada ya Wife kusafiri kwao nawaambia ndugu zangu wote kuwa nimeachana na Wife.

7.Niliomba Uamisho mkoani. Dodoma na nimepata kwa hiyo nampitia Wife Moro kimya kimya tunaenda Dodoma na hakuna pimbi atakaa afike kwangu.

8. Mambo ni mengi. Leo siku ya pili tangu tumeanza mchakato wa kuokoa ndoa yetu.

#Tairus #Bella Ciao

Safi Sana, baada ya kukutenga Na Ndugu zako atakuwa Na mission yake sasa ya kukutenga wewe Na Dunia!

Hivi Ni namna gani mwanaume unashindwa kusimamia msimamo wako in day light kwamba siachi mke wangu basi?

Mpaka uongo uongo Na ujitenge! Utakuja ku uwawa kimasihara, mke Ana nafasi ambayo kamwe haiondoi uitaji wa Ndugu! Utakuja kudebweda tu! Ngoja
 
Back
Top Bottom