Nimemwambia mke wangu tuachane halafu turudiane

Tairus

JF-Expert Member
Mar 13, 2013
676
1,055
Baada ya ndugu zangu kuonyesha wazi kuwa hawamtaki mke niliyemuoa nilikaa chini na mke wangu tukapanga jambo.

1. Tulikubaliana kujifanya tumegombana sana na kila mmoja ameridhia tuachane.

2. Tukaanza visa ili na ndugu waone sasa kuna mtoto wa shangazi yangu ambaye ni binamu wangu anakaa kwangu. Nikamwambia mke wangu amfukuze beki tatu na alafu awe hapiki wala kufanya kazi yoyote. Atafanya huyu ndugu yangu.

3. Nikamwambia wife aanze kuchelewa kurudi na kama akitaka ale huko anakofanya kazi na mimi ntajua la kufanya.

4. Wife akirudi asiongee na mtu na mm ntafanya hivyo yaan tuwe kama hatuongei kwa wiki tatu. Na mimi ntakuwa nalewa kila siku.

5. Baada ya izo wiki tatu Wife asafiri kwao Morogoro nibaki mwenyewe. Huyu ndugu yangu atawafikishia habari.

6. Sababu hawamtaki na mimi nampenda wiki mbili baada ya Wife kusafiri kwao nawaambia ndugu zangu wote kuwa nimeachana na Wife.

7.Niliomba Uamisho mkoani. Dodoma na nimepata kwa hiyo nampitia Wife Moro kimya kimya tunaenda Dodoma na hakuna pimbi atakaa afike kwangu.

8. Mambo ni mengi. Leo siku ya pili tangu tumeanza mchakato wa kuokoa ndoa yetu.

#Tairus #Bella Ciao
 
Kwa hiyo watoto nao umewatelekeza
 
Baada ya ndugu zangu kuonyesha wazi kuwa hawamtaki mke niliyemuoa nilikaa chini na mke wangu tukapanga jambo.

1. Tulikubaliana kujifanya tumegombana sana na kila mmoja ameridhia tuachane.
Adui ndugu zako.
Ndoa ni yako, hujaolea familia
 
Mambo ni mengi. Leo siku ya pili tangu tumeanza mchakato wa kuokoa ndoa yetu.

Unaweza upo sahihi na mbinu yako kwakuwa hakuna ajuaye kesho...

Lakini Kamwe usishirikiane na Mke/Mpenzi/Demu wako katika jambo linalohusu ndugu zako.. Ya kwenu myamalize wenyewe achana kumshirikisha Mkeo.. Be a Man

Utanishukuru baadae....
 
Baada ya ndugu zangu kuonyesha wazi kuwa hawamtaki mke niliyemuoa nilikaa chini na mke wangu tukapanga jambo.

1. Tulikubaliana kujifanya tumegombana sana na kila mmoja ameridhia tuachane.

2. Tukaanza visa ili na ndugu waone sasa kuna mtoto wa shangazi yangu ambaye ni binamu wangu anakaa kwangu. Nikamwambia mke wangu amfukuze beki tatu na alafu awe hapiki wala kufanya kazi yoyote. Atafanya huyu ndugu yangu.

3. Nikamwambia wife aanze kuchelewa kurudi na kama akitaka ale huko anakofanya kazi na mimi ntajua la kufanya.

4. Wife akirudi asiongee na mtu na mm ntafanya hivyo yaan tuwe kama hatuongei kwa wiki tatu. Na mimi ntakuwa nalewa kila siku.

5. Baada ya izo wiki tatu Wife asafiri kwao Morogoro nibaki mwenyewe. Huyu ndugu yangu atawafikishia habari.

6. Sababu hawamtaki na mimi nampenda wiki mbili baada ya Wife kusafiri kwao nawaambia ndugu zangu wote kuwa nimeachana na Wife.

7.Niliomba Uamisho mkoani. Dodoma na nimepata kwa hiyo nampitia Wife Moro kimya kimya tunaenda Dodoma na hakuna pimbi atakaa afike kwangu.

8. Mambo ni mengi. Leo siku ya pili tangu tumeanza mchakato wa kuokoa ndoa yetu.

#Tairus #Bella Ciao
Brother hii mbinu inaitwaje ila big up
 
Back
Top Bottom