bongo-live
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 1,564
- 1,921
Mke wangu kadai talaka kimya kimya sasa hivi kaolewa na Mwanaume mwingine!
Mimi ni baba wa mtoto mmoja, miaka 3 iliyopita nilifunga ndoa na mke wangu, kutokana na ujana baada ya miezi 3 tu niliichoka ile ndoa na kumrudisha Kwakweli sikuwa na sababu yoyote ila niliona kama ana kisirani sana na kuninyima donati yakee..yaani nilikua sina uhuru wa kufanya mambo yangu kama nilivyokua sijaoa, nikirudi nyumbani nimechelewa analalamika, nikitoka out shida, nikaona nimuache kwanza.
Nilimfukuza na sikujali kama anaishi wapi, kipindi anaondoka alikuwa na ujauzito, hivyo mpaka anajifungua hata sikukumbuka kumtafuta. Yeye alikuwa ananitafuta kila siku ila nilikuwa namjibu vibaya, namwambia ukipata mwanaume mwingine mpe huyo mtoto, mimi nilikosea kuoa. Ukweli ni kwamba sikuwa na mpango wa kumuacha moja kwa moja ila nilikuwa nikimuambia vile ili tu asinichoshe. Alinisumbua sana mpaka mwaka jana mwezi wa 6 ndipo aliacha kabisa kunitafuta, mpaka leo sijawahi kumuona mtoto wangu kwani nilikuwa sitaki kumuona, nikiamini kuwa nikimuona nikambeba hisia zinaweza kunifanya nirudiane na mama yake, na mimi sikutaka!
Basi, niliingia kwenye mahusiano mengine nikiamini kuwa yatanipa amani. Mwezi wa 9 nilianza kuishi na huyu mwanamke mwingine, hajui kama nilishawahi kuoa kwani anakuja kwangu ananiona naishi mwenyewe. Nilijitambulisha kwao ili akubali kuishi na mimi na ana ujauzito sasa anakaribia kujifungua.
Changamoto ni kwamba nimekuja kugundua kuwa wanawake wote ni wale wale, huyu naye nimemchoka kwani tangu kuanza kuishi naye kisirani chake ni kilekile kama cha ex wangu, hivyo kwa kuwa tayari ni ndoa ya kanisani nikaamua kurudi kwa mke wangu. Wiki iliyopita niliamua kumtafuta na kumuomba kumuona mtoto, alinijibu vizuri tofauti na nilivyotegemea, akanambia nikitaka kumuona mtoto ruksa, nikamuulizia anaishi wapi.
Akaniambia yuko hapa hapa Dar lakini sasa hivi yeye ni mke wa mtu hivyo siwezi kwenda kwake. Kwakweli nilishangaa kwani tuna ndoa ya kanisani, nilipomwambia kuwa wewe ni mke wangu, akanitumia nakala ya talaka ya mahakamani kumbe alifungua kesi ya talaka bila kunishirikisha, ikawa kama mimi nililetewa samansi na nikasaini lakini sikufika mahakamani, hivyo talaka ikatoka upande mmoja. Nilifuatilia mpaka mahakamani nikakuta kweli talaka ilitoka mwaka jana. Kwakweli nimechanganyikiwa. Hivi ni kweli mtu anaweza kupewa talaka bila mimi kuwepo? Nataka kurudiana na mke wangu, nimejikuta nina hasira naumia, nalia kila siku, yaani hata kazi nimeshindwa, sijui nafanya nini? Najua nilikosea lakini nimejirudi nataka kuishi na mwanangu nifanye nini ili kumrudisha?