Oscar Lyrics
JF-Expert Member
- Oct 8, 2022
- 3,004
- 5,174
Aliyempa paka mimba atafutwe akabidhiwe mkewe amtunze, yani ambebeshe mimba halafu amtelekeze, hiyo kisheria haikubaliki.
[emoji16][emoji16]Kwani inatakiwa wafanane mkuu
Imani potofu tu hizo mkuu.Huwezi kumuacha mtu Kwa sababu ya hayawani ambaye hujui chanzo wala asili yake. Pengine alikuwa anakusaidia kuiondoa tatizo kubwa sana huko mbeleni bila wewe kujua na pengine unafuga jini au pepo hatari bila wewe kujua.
Na hapa nikipima uwezo wako wa kufikiri na huyo mwanamke naona huyo mwanamke kakuzidi sana. Ulichotakiwa kufanya sio kukasirika ila kujua Kwa undani zaidi Kwa nini hapendi paka ,pengine kuna jambo kubwa ambalo ungelifahamu usingefanya uamuzi wa ovyo ila unaweza kujihisi umefanya uamuzi mgumu.
Ni nani amekupa taarifa za future wife wako kumtesa huyo paka, ni majirani I au unaokaa nao nyumbani? Kama ni majirani na wana moyo mzuri na wanampenda huyo paka Kwa nini hawakukusaidii kumhudumia? Stukq bro utafuga majini na mapepo
Wana zungumza sanaaa ila katika lugha ambayo wewe huielewi.Hata wanyama nao wanahisi maumivu, ni vile kuzungumza hawawezi.
Lakini siachi kula nyama.
Una kiwango gani Cha elimu. Jifunze tabia za wanyama Ili uwatambue na kuachana na Imani za kishirikina amabazo hazina ukweli wowoteHuwezi kumuacha mtu Kwa sababu ya hayawani ambaye hujui chanzo wala asili yake. Pengine alikuwa anakusaidia kuiondoa tatizo kubwa sana huko mbeleni bila wewe kujua na pengine unafuga jini au pepo hatari bila wewe kujua.
Na hapa nikipima uwezo wako wa kufikiri na huyo mwanamke naona huyo mwanamke kakuzidi sana. Ulichotakiwa kufanya sio kukasirika ila kujua Kwa undani zaidi Kwa nini hapendi paka ,pengine kuna jambo kubwa ambalo ungelifahamu usingefanya uamuzi wa ovyo ila unaweza kujihisi umefanya uamuzi mgumu.
Ni nani amekupa taarifa za future wife wako kumtesa huyo paka, ni majirani I au unaokaa nao nyumbani? Kama ni majirani na wana moyo mzuri na wanampenda huyo paka Kwa nini hawakukusaidii kumhudumia? Stukq bro utafuga majini na mapepo
Mpaka Karne hii hujui Dunia jinsi ilivyo pamoja na viumbe vyake . Achana na Imani zisizo kuwa na ukweli. Jitambue na wewe ni sehemu ya wanyama waliopo dunianiSikiliza vizuri song la Mzee wa busara la Sir Nature na Inspector Haroun.
Kuna kipande kinasema Mzee busara ana paka wake huyo akilia nyaauuu basi Nyumba ya Pili tunazika mtu na tunamsahau.
By the way paka wa Sasa hawana faida yoyote, hawakamati Panya, paka anataka nyama tu na shombo hali kitu kingine Sasa huyo paka wa nini.?
Huyo demu mlete kwangu Kwa Mkopo tutaelewana sana, sipendi kabisa haya mapaka hasa vile vilio vyao Vya kishirikina usiku.
Nakuunga mkono ndugu yangu huyo hafai. Kuna watu huwaga ni katili sana kwa wanyamaKuna wamanzi ni wakatili sana
Kuna demu nilikua naishi naye sasa ni siku kadhaa mwanzo alikuwa anakuja na kuondoka
Ila majuzi akalowea mazima kakaa kama siku nne hapa na nikajiset kichwan kwamba nitulie na huyu na ikifaa nije kumuoa siku za usoni maana tayari nishamlabel kama future wife
Sasa hapa jirani kuna paka ana mimba tena kubwa sana ni paka mstaarabu sana hana sifa ya udokozi wala nini ila sasa mwenye paka alihamia mkoani sasa alishindwa kuhama na Paka basi yule paka akawa kaachwa tu anashinda mazingila ya hapa hapa.
Alikua anateseka sana unakuta analia njaa tu maana hajazoea maisha ya maporini nikawa nikija nikila basi nitamwita na kumpa mabaki ya chakula
Siku zikaenda akanizoea sana mwisho akawa ni kama paka wangu tu akahamia kwangu akawa anashinda hapa.
Nikawa nampa chakula kila msosi lazima nimtengee kidogo hata kama hayupo nitamuwekea tu kwenye kisosi najaza vizuri sasa ana mimba kubwa sana mimi napenda sana paka wala hajaharibu chochote nilitoka nimerudi nakuta paka hayupo namuuliza mwenzangu hanipi majibu.
Kuambiwa kumbe nikitoka huwa anamfukuza yule paka na kumpiga sasa kaona haitoshi kaenda kununua sumu ya panya kachanganya kwenye kipolo cha mchuzi wa nyama kwenye kisosi anachoriaga paka narud nakuta ndo anakiweka kisos huko ndani ashachanganya ili paka akija ale kumbana ndiyo akasema alikua anamuwekea paka akasema hapendi paka kwahiyo bora amuue tu kwa sumu.
Nikamuuliza huyo paka kafanya nini mbona sio mdokozi jibu lake ni hapendi paka tu nimekasirika sana sikuwa na budi zaidi ya kumuambia achukuwe nguo zake aondoke.
Kama mwanamke anaweza kumuua paka kiumbe cha Mungu tena mwenye mimba kubwa huo si ukatili?Paka mwenyewe ukimuona utaona huruma mimba yake imekua kubwa analala sana muda mwingi na kachoka sana muda wowote anazaa
Sikutegemea kwakweli, nimemuambia afungashe akuongea akachukua vitu vyake akatoka sahizi anatuma msg za matusi tu hapa.
Kuna watu wana roho mbaya sana napenda paka sana kwenye maisha yangu huwa nakumbuka utotoni nilishuhudia paka wetu akipewa sumu halafu alikua na vitoto vichanga hadi leo naumiaga huwa nakumbuka najiskia hasira na uchungu sana
Nawe ni wale wale. Amwondoe ampeleke wapi? Aondoke yeye mgeniki ukweli naona sio sahihi kuna mtu hana mapenzi na paka kama mimi napendelea mbwa kuliko paka zaidi....
Paka anakuga na kero zake kama kulialia usiku na ata kila ukitaka kula anakua anasonga njee na kujiliza njaa na kama ashakuambia hapendelei paka muondoe unamng'ang'ani kama paka wa dawa.
Umeambiwa sababu wewe unatafuta ya kwakoHuyu alikuwa na sababu zake tuu...
Usikute Ishu hata sio huyo Paka
Mtoto wa watu ashamtumia akaamua kumtafutia sababu[emoji2]
Umenena kweli kabisaNakupongeza sana kwa maamuzi uliyofanya, viumbe vyote vimepewa pumzi na Muumba alietuumba, suala la binadamu kuchomoa uhai wa kiumbe ni pale tu kukiwa na sababu maalum aidha kujulinda, kuandaa kitoweo, kuzuia magonjwa, kulinda mifugo yake. Isiliwe , ama sababu ya maana. Kinyume na hapo mfano huyo kichaa alietaka kuchomoa uhai wa paka kisa tu anawachukia, sio sawa.
Niliwahi kuwa na mgeni wangu nakuta anamfukuza paka anamfokea Toka!! Nilimwambia "huyo paka namfuga mimi hapa ndio kwake muache apumzike" , siku nyingine nikamkuta anarudia nilimkata jicho kali sana mpaka akajistukia kuniomba msamaha, tangu siku hio hakurudia.
ukiona nafuga mbwa au paka jua kwamba huo sio wa porini, OLE WAKO nikukute unamtilia sumu kwenye chakula, utarudi ulikotokea !!
Mtu anaua mnyama bila sababu, je atasita kukuchomoa uhai wako akiwa na wivu, tamaa ya mali, kufosi muachane, n.k. ?
Kuna wale wapuuzi akikuta mbwa amekaa zake hana habari basi atachukua jiwe na kumpiga najiuliza WTF, amekukosea nini kwani? Tunatofautiana sana.Uzungupori wako mkuu,Mioyo tumetofautiana.....assume ungekuwa mbwa afu upigwe bila Makosa.
Sana mwamba...na inahuzunisha sanaKuna wale wapuuzi akikuta mbwa amekaa zake hana habari basi atachukua jiwe na kumpiga najiuliza WTF, amekukosea nini kwani? Tunatofautiana sana.