Nimemtafutia kazi sasa anakataa kutoa penzi kwa bosi, mimi nimfanyeje?

jean phillipe beyun

Senior Member
May 18, 2015
142
167
Wakuu habari zenu,


Nina mdogo wangu wa kike, ni wa mwisho kwetu kuzaliwa, amemaliza chuo miaka 2 iliyopita hakua amepata kazi, amekua nyumbani tu muda wote huo. Kwa kweli for the past two years nimetembea sana kwenye mashirika mbali mbali kumtafutia kazi bila mafanikio. Hadi ilipofika December mwaka Jana nilipomlilia hali bosi mmoja ambae tuna muingiliano wa kikazi katika mashirika yetu.

Mimi huenda kwenye shirika hilo kila mwisho wa mwezi kwa mambo yahusuyo hesabu za shirika za mzee huyu mwenye roho nzuri, akaongea na HR manager wa hapo na hatimae mdogo wangu akaingia kazini baada ya mchujo wa karibu watu 1500 katika mtihani wewe kuandika baadae oral kwa kweli ilikua muujiza.

Sasa amebakiza wiki moja amalize probation, miezi miwili iliyopita bosi wake alimwomba uhusiano na mdogo wangu akamkataa akamwambia yeye ana mtu wake, yule bwana hajakata tamaa ameendelea kumkumbushia jambo hilo binti hadi sasa yule bwana kuona hali imeshindikana akamuita na kumwambia wazi kwamba kama unakataa ombi langu basi sitalipeleka jina lako kwa ajili ya confirmation, akasema anayo sababu nyingine ya kisheria ya kutom confirm.

Hivyo kazi yake ipo hatarini, sasa amelileta rasmi kwangu kuona tunafanyaje kuokoa hii hali, mimi nikamwambia akubali tu kuwa nae haitampunguzia chochote, nikamshauri wazi tu kwamba maisha wakati mwingine ni lazima ujitoe sadaka mwenyewe, watu wote waliofanikiwa wamepita njia ngumu sana na hata wakikueleza huwezi amini ni siri ya mtu moyoni.

Nimejaribu kumpa mifano mingi ya wanawake waliofanikiwa na anaowaona wamekalia viti vikubwa asilimia tisini ni pichu
Lakini binti kasema yeye hawezi kufanya hivyo acha akose tu kazi kwamba ana mtu wake. Kwa kweli nimekasirika sana kwa kitendo hicho, yule mzee alienisaidia pia anaungana nami kwa hili, sasa basi nimemwambia binti kama akipoteza hiyo kazi kwa ujinga wake sitaki kumuona hata kwangu, arudi kijijini kabisa kwa wazazi, maana amewapigia simu kama vile kunisemea vibaya kwa ndugu mbali mbali.

Huyu mtu wake mwenyewe ni fake balaa, huwa tunakutana sana mjini humu akiwa na magumashi kibao sema tu namna gani vipi mambo ya kiume, ana faulo kibao tu. Yaani kwa kweli nimekasirika sana, mimi mwenyewe kazini kwangu nakimbilia hadi begi la bosi wangu kwenye gari asubuhi akifika kama mtoto, yote hiyo ni kujipendekeza ili mambo yaende. Mwaka juzi kuna bosi wangu mwanamke mbaya wa sura kama nini, mumewe alikua na kisukari, kila watu wakiondoka tunajifungia ofisini, lakini nilivumilia hadi alipohamishwa na sasa hivi naishi poa kazini, yote ni kulinda kazi.

Sasa najua wazi huyo bosi wake atatekeleza hicho kitisho anachotoa, hr siku zote wanapokea mapendekezo kutoka kwa line manager, akisema staff huyu ameshindwa probation HR hawezi kufosi, na hii mbinu inatumika sana hasa kwa new comers, huwezi kuruka, labda Mungu akusaidie usitongozwe na bosi yoyote.
 
Jamaa uko realistic sana....

It is morally wrong. Yes it is. Sasa she has a chance of choosing between her morals or dignity and material benefits - an employment opportunity.

Realistically wanawake wengi go for the latter when the situation isnt as harsh. Now that there are material consequences and they are blackmailed ndio wanatumiaga morals au dignity to their defence. Interesting creatures.

Achague kusuka ama kunyoa. It is a cruel world.
 
Hongera zake huyo binti kwa kukataa kutoa rushwa ya ngono. Mkuu, hufanyi vema kumshinikiza atoe rushwa ya jinsi hiyo.

Kuhusu huo uhusiano wake mwingine unachotakiwa kufanya ni kutoa ushauri na kutoa sababu - kama unaamini huyo mpenzi wake hafai. Vinginevyo subiri posa.
 
Dah, unajua inahitaji ujasiri sana mkuu kwa case kama hii yako.

Nashindwa kutoa ushauri juu ya hili ila kwa mtazamo wa juu juu kila mtu yuko sawa kati yenu ila nani yuko sawa zaidi kuliko mwenzake kwa hapo bado sjajua ila haya maisha haya, ACHA TU.
 
aisee, ulichomueleza bimdogo nisahihi kabisa, kwa ajira na mabosi wa kileo, sasa wewe ndugu yake unagawa kwanini yeye ashindwe ukizingatia haiweki alama.....???
 
Life is unfair..... uamuzi wake ni sahihi maana hauwezi jua.... ule ni mchuzi wa kuku wa kienyeji ... hauonjeki... atazama mazima humo... mwisho wa siku anaharibiwa na wewe ndo chanzo...

Kazi zipo tu utafika wakati wake atapata .... yeye hafanyi kwa sababu ana mtu tu.... yeye anafanya kwa kulinda heshima na utu wake pia
 
Inasikitisha kuona ndugu yako wa damu anashadidia ukangonoke kisa kazi, Hivi ni kweli kazi imekuwa na thamani kiasi hicho? nijuavo mimi Afya ni dili kuliko kazi, akipata ukimwi leo hiyo kazi utamfanyia wewe?

jaribu kumuelimisha nduguyo njia sahihi na zinazokubalika ata kwa dini zetu, hiki ulichokileta hapa na unakishabikia hivo kwakweli inasikitisha, maisha marefu wakati mwingine tunafupisha wenyewe, maana hapo ata baraka za mungu huwezi pata
 
Kakangu mimi,ehehhehehehe!
Angemvizia huyo boss amtegue kiuno hata kwa bunduki ya kumpora askari aliye lindo!

R.i.P kaka wangu mimi!
Ila nini kuna limtu huku limebore ujue!
Bas tu ndo silijui!ngelijua.kerbu moja tu nimshtue kuwa brothers dont andika this maujinga!
 
Nimetamani kukutukana ila nimekosa tusi jipya yote yalishasemwa, Inshort hutakiwi kumlazimisha amkubali huyo bosi mfano akampa penzi leo kesho boss akafa/kufukuzwa kazi atakua anawapa wangapi? na je ikitokea na wewe bosi wako wa kiume anapenda kuwaingilia waanaume akakuomba umpe iyo naniliu yako utampa kisa kazi? heshima ni bora kuliko fedheha ndugu yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom