Penzi la mwana wa bosi

Tamu3

Member
Feb 17, 2023
25
16
PENZI LA MWANA WA BOSI

(sehemu ya kwanza)
1

Nipomaliza la saba, litorokea mjini,
Mguuni nina raba, na kibegi mgongoni,
Nauli ninayo haba, nimeweka mfukoni,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

2

Gari zuri tukapanda, kuelekea mjini,
Shauku ilinipanda, kuondoka kijijini,
Nauli nikailinda, nisiibiwe mjini,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

3

Hatimaye tukafika, usiku huko mjini,
Hofu mie linishika, kiwa pale stendini,
Kule sikuwa na kaka, wala ndugu wa mjini,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

4

Niliishi stendini, karibia wiki zima,
Ni siku moja jioni, akaja mama mzima,
Shida nikamwelezeni, kanionea huruma,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

5

Kwake akanipeleka, gari lake zuri Sana,
Lipofika tukashuka, getini pakaachana,
Wandani walishituka, nguo zangu paukana,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

6

Yule mama sasa bosi, kazi amenipangia,
Kazi kushika mikasi, kusawazisha maua,
Kuni nakata vipisi, jikoni navitupia,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

7

Bosi na mabinti tatu, kiume hakujaliwa,
Mkubwa aitwa Atu, sura nzuri amepewa,
Avaa virefu vyatu, vinang'aa kwenye juwa,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

8

Kwa bosi pale nyumbani, bosi mtu wa safari,
Na mwaka jana mwishoni, alisafiri safari,
Atu nami libakini, nyumba tulinde vizuri,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

9

Toka kiwa kijijini, mapenzi kwangu ni Shari,
Sijawahi lifanyeni, natoboa hii Siri,
Atu kanizindueni, kuvunja hiyo amri ,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

10

Nakumbuka siku moja, Atu likuja chumbani,
Kwangu likuwa kioja, usiku meingieni,
Amevaa kanga moja, imemchora mwilini,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

11

Atu nikamuuliza, kwanini aje chumbani,
Akadai hatoweza, amepandwa na majini,
Mambo mengi linijuza, moja ni kuhusu chini,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

12

Pasipo kutarajia, kanga kule litupia,
Chuchu nikajionea, zimesimama sawia,
Akili ikazubaa, macho kodo nakodoa,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

Endelea kusoma sehemu ya pili,
Bonyeza hapa

View: https://www.facebook.com/107870673982860/posts/658604935576095/?app=fbl

Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa Mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi TANZANIA 5/9/2023

View: https://www.facebook.com/107870673982860/posts/pfbid02eNvfEfKKVPmKdtKQ41SKybNb8JsCZ5t2AavJgywyhzxvfgNfJ6G9eqb3sJL7qEW5l/?app=fbl
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom