Lol...acha kupekenyua simu ya mpenzi wako. Wanasema eti ukifanya hivyo utajipa jakamoyo.
Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kuficha kichwa chako mchangani na kujifanya kama hujui vile.
Acha kupekua pekua simu dogo
Eti nini? Umemchumbia na kuishi naye? Hivi unapochumbia ndio unapata uhalali wa kuishi na binti wa watu kweli? Dini gani hii inafundisha hivyo? Mi nilidhani ulimuoa na hivyo kukufanya wewe uwe na uhalali hata wa kuhoji kila kitu, kumbe bado unazini na kufanya uasherati? Ndio maana na yeye kaamua kuwa na wengine maana wewe na hao mahawara zake wa nje hamna tofauti, wote ni wazinzi tu!Niko katika mahusiano ya kimapenzi kwa muda sasa mpaka kumchumbia huyu niliye naye na kuishi naye.Juzi kuna message ya kimapenzi imeingia kwenye simu yake.Cha kushangaza amekuwa mkali baada ya mimi kuishika simu yake kwa kigezo kwamba hamjui huyo mtumaji ila atamfuatilia then anijulishe. Kumwambia afanye hilo zoezi hapo tukiwa pamoja akakataa.Nishaurini bandugu hiyo ni halali kweli mimi kusubiria mpaka amfuatilie mhusika ndio aniambie?asamteni kwa ushauri.
"We are always paid for our suspicion by finding what we suspect." Henry David Thoreau
achana na simu ya mwenzio
huna uhalali wa kuingilia privacy yake
kama wampenda utamwamini
Hii habari ya kusema sijui eti usiiguse simu ya mwenzi wako mimi huwa siielewi kabisa!.mmh, hivi kuna twisheni ya hili suala la kuheshimu gadget za wenzi wetu?
Mie siwezi mbona, nikinyimwa kushika nakosa usingizi hata mwezi.
"We are always paid for our suspicion by finding what we suspect." Henry David Thoreau
Hii habari ya kusema sijui eti usiiguse simu ya mwenzi wako mimi huwa siielewi kabisa!.
kumbe tuko wengi tusioelewa
mie naonaga ni 'uzinzi' tu