Nimemshauri ampige chini

Fursakibao

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
6,676
11,110
Habari za usiku huu wadau.

Nina rafiki yangu tumeshibana sana, siri zaje zangu zangu zake.

Sasa huyu mshikaji wangu ana demu wake wako kwenye mahusiano mwezi wa 8 sasa. Mwanzoni mapenzi yalianza vizuri baadae mambo yakabadilika. Kutokana na long distance kati yao kila kukicha ugomvi hauishi.

Kama rafiki wa karibu nilijitoa kabisa maana sikutaka kuwa mpatanishi, ika nyuma ya pazia nilikuwa mshauri wa rafiki yangu.

Kwa kifupi mapenzi yao yalikuwa yanabadilika kila wiki, wanaweza kugomvana ukajua hawa basi tena, kesho yake mapenzi yananoga. Mwisho wa siku walikaa wakashauriana waishi pamoja kwa muda wa mwezi na nusu ili waweze kusomana tabia.

Ndani ya mwezi moja wa kuishi pamoja, demu aliugua sana kwa muda wa wiki na zaidi hivyo jamaa akawa ndio mpishi na kufanya kazi zingine.

Baada ya demu kupona alimshukuru sana jamaa na akasema huyo ndio Mume aliyekuwa akimuomba Mungu ampatie. Hivyo basi walikuwa wameamua wiki ijayo amvalishe Pete ya uchumba.

Leo asubuhi wameamka vizuri, jamaa akampeleka saloon akalipa kama laki, wakarudi nyumbani, walipofika nyumbani demu akamwambia jamaa akatupe takataka, jamaa akamwambia amechoka, basi demu ketema povu si la nchi hii.

Baada ya kutema povu demu kaingia jikoni kapika, baada ya kumaliza kapakua kala bika kumpa jamaa msosi.

Jamaa hakusema kitu akapiga kimya. Sasa anafikiria kuhairisha mipango ya pete ameniuliza mi nikamwambia huyo demu hafai.

Ungekuwa wewe ndio jamaa ungefanya je? Au kama wewe ndio mimi ungempa ushauri gani?
 
Kuwa makini sana na mambo ya wapenzi. Mwisho wa siku wewe ndiyo utaishia kuonekana mbaya kwa kutaka kuwatenganisha. Huyo rafikiyo utashangaa ndiyo anamwambia manzi wake huu ushauri wako wa "hovyo" mwishowe unajikuta unachukiwa na pande zote mbili.

Ya Ngoswe.....
 
Kuwa makini sana na mambo ya wapenzi. Mwisho wa siku wewe ndiyo utaishia kuonekana mbaya kwa kutaka kuwatenganisha. Huyo rafikiyo utashangaa ndiyo anamwambia manzi wake huu ushauri wako wa "hovyo" mwishowe unajikuta unachukiwa na pande zote mbili.

Ya Ngoswe.....
Kwahiyo ushauri wangu ni wa ovyo?
Ulitaka nimwambie je avumilie au?
 
Kuna kitu jamaa kamfanyia huyu mwanamke siyo bure.Kama ni demu kama ulivyomuita aache udemu awe mwanamke wanawake hawacharukagi bila sabubu kama mademu.Cha mwisho achana na issue zao za chumbani.
Ni mwanamke na wote wako 40s.
Rafiki yako wa damu akija kukyomba ushauri utamuuacha apogee kisa mambo ya chumbani?
 
Naomba uniambie umri wa jamaa yako na wewe then umri wa mwanamke? Pia mwanamke ana akili kubwa kuwazidi hasa jamaa yako kuna mazoea kamzoesha huyo mpenzi wake ila kwako ana pretend na kujikakamua kama sio dhaifu
 
Naomba uniambie umri wa jamaa yako na wewe then umri wa mwanamke? Pia mwanamke ana akili kubwa kuwazidi hasa jamaa yako kuna mazoea kamzoesha huyo mpenzi wake ila kwako ana pretend na kujikakamua kama sio dhaifu
Mwanamke ana 40, jamaa ana 38
 
Inawezekana wana mazoea flani na huyo jamaa yako, na wewe hujui wanaishije....Embu waache kwanza watayamaliza wenyewe hasira zikiwaisha

Very correct, mi nina stori ila si kama ya jamaa ila yataka kufanana nayo. Manzi angu niko naye kwenye mahusiano almost 8 months hadi sasa. Sasa kitu ambacho nimekuja kuki notice kwa wadada au wachumba hawa, ukimzoeza kuwa unaosha vyombo na yeye yupo kakaa kuna siku atakuja kufoka kwanini hujaosha vyombo, hata kufua na majukumu mengine ambayo tumegawana kama Mama na Baba kwenye jamii yetu kulingana na nafasi zetu.

Mie huwa na kiutamaduni cha kufua nguo zangu na zake kama kuna nguo aliacha ghetto chafu anakuta nimezifua., sasa kuna siku yeye alipofika ghetto ile night akakuta sijafua nguo zake kama alivyozoea kukuta kwa sababu ya ubize wa kazi. Basi mdada alichukua nguo zake pekee ake akafua nikamuuliza kwani ukifua na zangu utapungukiwa na nini!!? Basi hakukubali kunisaidia kufua hizo nguo daah ila baadae sijui akili ikamjia akaenda kabatini akachukua nguo zangu akazifua..!

Na hiyo ni baadae jioni kabisa mie sikutaka tuzozane kwa sababu ya kufua nguo
 
Back
Top Bottom