Nimempima UKIMWI nikakuta anao

P.hunter

Member
Nov 16, 2015
74
125
Habari za Muda Huu Waungwana,

Samahani kama nItakuwa nakosea kuwasilisha hii Mada lakini naombenii ushauri kwenye hili, Juzi Kati nilikamata mdada mmoja kutoka Bar fulani Maeneo ya Ubungo, Sasa nikampeleka kwangu usiku huku tukiwa tumelewa, Ilipofika muda wa kunjunjana nikataka kuvaa kondomu akasema anaogopa ataumia.

Nikamwambia basi nikupime kwanza maana vipimo ninavyo, akacheka akasema mimi ni mwanaume wa 4 kwake hana historia ndefu then akasema wiki mbili zilizopita aliumwa akaenda kuchek ngoma akakutwa hana, lakini akasema kama nataka kuhakikisha basi nimpime.

Akawa hana wasiwasi kabisaa, me nikampima then mzigo ukasoma positive, hapa nikatumia ujanja kumficha ili asijue, niliogopa angejisikia vibaya. Basi nikazuga zuga mpaka tukalala, asubuhi nikampa nauli akasepa.

Sasa Nachoomba mnisaidie ni Je nimueleze kuwa yeye ni HIV positive au nimpotezee maana nakutana nae sana mtaani huku.

Anafanya kazi katika bar ya mtaani.

Natamani kumueleza ukweli lakini nashindwa.

Je, nifanyeje?
 

Darius RR

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
306
1,000
Mweleze kwamba siku ile ulivyompima kipimo hakikosoma vizuri, au kipimo kime-expire kwa hiyo kinatoa inconclusive results, hivyo unamshauri akapime zahanati ambayo unajua atapata ushauri nasaha.

Usimwambie kama unajua majibu ila mpe tu ushauri wa kupima.
 

P.hunter

Member
Nov 16, 2015
74
125
Mweleze kwamba siku ile ulivyompima kipimo hakikosoma vizuri, au kipimo kime-expire kwa hiyo kinatoa inconclusive results, hivyo unamshauri akapime zahahanati ambayo unajua atapata ushauri nasaha.

Usimwambie kama unajua majibu ila mpe tu ushauri wa kupima.

Sidhani kama nikimwambia hvo ataenda zahanati kupima, nadhani atapuuzia maana anajiamini na tulipima ili anihakikishie mimi kuwa hana ili tupige mechi kavu
 

GEMBESON

JF-Expert Member
Apr 15, 2012
1,167
2,000
Yani umtoe damu mtu kwa lengo la kupima, halafu aondoke bila kuona wala kuulizia majibu yake? mbona sio rahisi.

Wakati unapima yeye alikuwa amelala?. Na inawezekanaje wewe umpime yeye halafu wewe mwenyewe usipime?.

Binafsi sijawahi kupata mtu wa hivyo, nikimpima mtu na mimi najipima na wote tunaona majibu yote.
 

Darius RR

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
306
1,000
Sidhani kama nikimwambia hvo ataenda zahanati kupima, nadhani atapuuzia maana anajiamini na tulipima ili anihakikishie mimi kuwa hana ili tupige mechi kavu

That is so tough, kama vipi mkaushie, usimweleze wala usieleze mtu yeyote anayemfahamu.
 

P.hunter

Member
Nov 16, 2015
74
125
Yani umtoe damu mtu kwa lengo la kupima, halafu aondoke bila kuona wala kuulizia majibu yake? mbona sio rahisi.

Wakati unapima yeye alikuwa amelala?. Na inawezekanaje wewe umpime yeye halafu wewe mwenyewe usipime?.

Binafsi sijawahi kupata mtu wa hivyo, nikimpima mtu na mimi najipima na wote tunaona majibu yote.

Kiongozii, Alipima akijiamini na alitakaa mm nimuamini, hakuwa anataka kujua majibu yake, yy anasema alipima wiki mbili zilizopita so alitaka mm niamini na mm nlivompimaa sikuonesha mshangao wwte nikmwambia uko sawaa ndomana hajahojii
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
42,594
2,000
Mhhhh hapo kuvaa ndomu na kuanza kumpima naona CD imeruka,sidhani kama kuna mwanamme rijali akavumilia kipindi hiko chote wakati yeye anataka kutoka wazungu!! Kama CD haijaruka basi itakuwa CHAI kasoro andazi.
 

P.hunter

Member
Nov 16, 2015
74
125
Ulimpima na kipimo gan kwani?

D5E898E0-153D-44E5-815C-055E839E60D5.jpg
 

Darius RR

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
306
1,000
Na mm nimewaza hv lakin naona nafsi inanisuta

Ndiyo maana huwa haishariwi kujipa majukumu ya madaktari.

Kama unajijua una kifua kaa na hiyo siri, kama huna kifua mjulishe, maana ikitokea ukamweleza yeyote ambaye siyo muhusika utakuwa umekosea sana.

Lakini je, una uhakika ataweza kuyapokea vizuri majibu?
 

dronedrake

JF-Expert Member
Dec 25, 2013
9,183
2,000
dah we jamaa, unaanzaje kula bar medi aisee, bora kupiga puli kwa kweli

anyway, mpe majibu ajijue
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom