Nimempenda Barmaid

RFP

Senior Member
Jun 15, 2016
171
194
Wadau,

Jumapili iliyopita niliamua niende bar moja hapa maeneo ya Kimara Korogwe, kwasababu situmii pombe, niliagiza grand malt ya baridi nikawa nainywa, katika bar hii kuna mfanyakazi mmoja mzuri anasura ya upole sijawahi ona, nimetokea kumpenda balaa.

Haiba yake haifanani na mazingira niliyompata yani ni mpole never meet before, mweupe, kaumbika ana zigo kiasi! Wiki lote linaisha lazima nipitie hii bar nikitoka kazini, naombeni ushauri nifanyeje,maana nampenda sana.
 
Mwambie tu ukweli kua unampenda ingawa anaweza asikuamini maana atadhani umemchukulia kama baa medi ambao watu huwachukulia kama ni easy prey kwamba wanapatikana muda wote na kwa bei chee.

Nilishawahi kumpata mmoja baa moja kinondoni alikua mzuri na mtamu sijawahi kuona hadi nikambadilishia kazi maana akivyokua mzuri na maeneo ya kinondoni nikaona watu watanishinda dau nikamhamisha fasta nikamtaftia kazi nyingine na kumsaidia mambo mengne.

Sio kila baa medi ni malaya wengine wanafanya kutokana na shida. Chukua baa medi huyo mkuu.

Ni baa gani hapo korogwe mkuu nitembelee jumamosi kupata chakula ya mchana nikiwa natokea maili moja kumuona jamaa yangu.
 
Wadau jumapili iliyopita niliamua niende bar moja hapa maeneo ya kimara korogwe, kwa sababu situmii pombe, niliagiza gland malt ya baridi nikawa nainywa..katika bar hii kuna mfanyakazi mmoja mzuri anasura ya upoleee...sijawahi ona, nimetokea kumpendaa balaa..haiba yake haifanani na mazingira niliyompata...yaani ni mpole never meet before,,mweupe, kaumbika...ana zigo kiasi! Wiki lote linaisha lazma nipitie hii bar nikitoka kazini, naombeni ushauri nifanyeje..maana nampenda sana

Hiyo bar inaitwaje

Tuanzie hapo kwanza
 
hata kama wewe unamuona mpole, mkimya na mtaratibu, Je wewe ndo wa kwanza kumuona? je kwa siku kuna wanaume wangapi ambao wanamfikiri kama unavyomfikiria wewe? je kwa saa moja anatongozwa na wanaume wangapi? je kila baada ya nusu saa anapokea tip ngapi baada ya kuhudumia wateja ili awape namba ya simu? je kila baada ya robo saa wanaume wangapi wanampigia simu ambao wengi amekutana nao hapo bar na wengine huenda njiani? Sina maana nataka kukukatisha tamaa, ila yafikirie yote haya halafu UAGANE NA NYONGA!
 
Sasa tatizo liko wapi mkuu? Next step hapo ni kumwambia ukweli wa moyoni. Au hujui jinsi ya kutongoza kwahiyo unataka tukufundishe?? Ila kuwa makini mkuu...Usipime kwa macho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom