Nimempa mimba mdogo wa rafiki yangu

Nimempa mimba mdogo wa rafiki yangu

Wakuu,

Naomba mnisaidie kwa hili.

Nimempa mimba mdogo wa rafiki yangu kipenzi, namuambia aitoe hataki. sio kama sina uwezo wa kumuhudumia ila naogopa jinsi watu watakavyonichukulia kutokana na status yangu.

Naona aibu sana jamii inayonizunguuka ikija kufahamu hii habari. naombei mnisaidie wakuu nifanye nini kuondokana na aibu iliyo mbele yangu? Kuhusu kumpeda nampenda sana binti na nina mpago aje awe mama wa watoto wangu lakini sio kwa kuzaa nje ya ndoa.

Wakuu ebu nisaidieni katika hili, nimshauri vipi huyu mtoto akubaliane nami maana anakataa hataki kusikia kabisa habari hizo.

Hivi wewe mpuuzi huyo bint kwa sisi waafrika ni mdogo wako kabisa ukamdanganya na visenti uchwara vyako, ukamvulia nguo bila haya umemmimba, unaonaje aibu kwa jamii, hukuona aibu kumvulia nguo Leo unaionea aibu jamii!!? Wewe wewe Subiri huyo rafiki yako ajue, au mtoe kabla hajafa awe ameacha meseji ndio utaijua hiyo familia ikoje. Sina ushauri zaidi ya kuwaza kwa hasira kwamba ungekuwa jirani yangu ningekusagia hata chupa ufe.
 
shukran sana wakuu kwa mawazo yenu. wengi mmenishauri nioe haraka. nafanyia kazi ushauri huu haraka iwezekanavyo maana no way!!
 
Kajitambulishe kwao kama Mpenzi wake. Ulitegemea uoe bila kujulikana kwao kuwa yeye ni zaidi ya "mdogo" wako?
 
SWALI 1:wakati unamtongoza na kumla hukujua kama ni mdogo was rafiki yko na kama kuna watu, SWALI 2:status yako ni ipi?SWALI 3:endapo utampeleka kuitoa binti akafa utafanya nn? SWALI 4:vipi binti yeye hana Status hadi analea mimba?? SWALI 5:watu watakuchukulia vipi na binti unahisi watamchukulia vipi kwa kubeba ujauzito kabla ya ndoa??? SWALI 6:Baadae ya saa ngapi au lini aje kua mama wa watoto wako?je,akiitoa hiyo ukija kumuoa asipozaa na ww utatoa kizazi ili wote msizae???
 
Wakuu,

Naomba mnisaidie kwa hili.

Nimempa mimba mdogo wa rafiki yangu kipenzi, namuambia aitoe hataki. sio kama sina uwezo wa kumuhudumia ila naogopa jinsi watu watakavyonichukulia kutokana na status yangu.

Naona aibu sana jamii inayonizunguuka ikija kufahamu hii habari. naombei mnisaidie wakuu nifanye nini kuondokana na aibu iliyo mbele yangu? Kuhusu kumpeda nampenda sana binti na nina mpago aje awe mama wa watoto wangu lakini sio kwa kuzaa nje ya ndoa.

Wakuu ebu nisaidieni katika hili, nimshauri vipi huyu mtoto akubaliane nami maana anakataa hataki kusikia kabisa habari hizo.

KWANI NYIE FORM TWO SI MKO KWENYE PEPA NYIe??
 
Unaona aibu kutoka na status yako mbona hujaona aibu wakati wa kutia mimba.......ndio wale kesho asipozaa mnawasimanga
 
Kuna watu hamnaga aibu kabisa. Yani unajielezea kabisa??
 
Umesema "unampenda na unataka aje kuwa mama wa watoto wako". Shida nini tena, kwa hiyo unataka kuua binadam sio ee. Acha utoto, kuzaa nje ya ndoa unamaanisha nini hasa? Kwani kufanya mapenzi na mwanamke usiyefunga naye ndoa nani kakuambia sio dhambi? Mungu hupenda kuyaonesha mambo ambayo mtu hufanya sirini na kuweka wazi. Kuwa makini usijaribu kuua maana huwezi jua utaumbuka kiasi gani baada ya hapo. Ndio ukubwa huo embu komaa kiume. Yaani ubetuke na sister wa mtu halafu unataka pia kuhatarisha uhai wake. Embu fikiri rafiki ako akikuta sista ake unakufa na ww ndo mhusika ipi ni nouma zaidi.
 
Kakuona uko naBright future,.muache kuwahondomola watoto wa familia duni kavukavu,.
Wakizinasa hawazichukulii kama ni mimba bali ni Fursa.
Pole mdau
 
Kwani mlivyokuwa mnafanya matusi ulikuwa huoni aibu...

Leo mtoto huyo, baba kijacho... status kitu gani...
 
Wewe sio kijana mkimya,Ni kijana muharibifu....hongera kwa kutia mimba..
 
Eti aibu!!! Aibu kwa nani?ulitaka upande tu usivune, kubali ujauzito huo na ulee, tutakuandalia jina tu LA mtoto
 
Huyu nae atataka aje kuitwa baba nae huyu huyu na akili zake kama kajaza choo kichwani, yaani dunia hii … Mungu tu atunusuru aisee daah!
 
Wakuu,

Naomba mnisaidie kwa hili.

Nimempa mimba mdogo wa rafiki yangu kipenzi, namuambia aitoe hataki. sio kama sina uwezo wa kumuhudumia ila naogopa jinsi watu watakavyonichukulia kutokana na status yangu.

Naona aibu sana jamii inayonizunguuka ikija kufahamu hii habari. naombei mnisaidie wakuu nifanye nini kuondokana na aibu iliyo mbele yangu? Kuhusu kumpeda nampenda sana binti na nina mpago aje awe mama wa watoto wangu lakini sio kwa kuzaa nje ya ndoa.

Wakuu ebu nisaidieni katika hili, nimshauri vipi huyu mtoto akubaliane nami maana anakataa hataki kusikia kabisa habari hizo.
Rafiko yako lazima akule takl
 
Back
Top Bottom