Nimempa mimba mdogo wa rafiki yangu

Nimempa mimba mdogo wa rafiki yangu

Kama huna mpango wa kumuoa achana naye.
Sio sio favor au huruma.
Cha muhimu omba msamaha, lea hiyo mimba.
Mtoto akizaliwa mchukue kaa naye.
 
Toa Posa kabla kaka yake ajajua make nyie wanaume mnakuwaga na hasira sana kujua best frnd anakulombea dada
 
Tabia za kishenzi kabisa ili kupoza machungu hapo wewe peleka posa tu ila urafiki ndio basi tena
 
Ulivyokuwa unamtawanya miguu hukuona aibu ila sasa hivi ndiyo unaiona?????

Wakuu,

Naomba mnisaidie kwa hili.

Nimempa mimba mdogo wa rafiki yangu kipenzi, namuambia aitoe hataki. sio kama sina uwezo wa kumuhudumia ila naogopa jinsi watu watakavyonichukulia kutokana na status yangu.

Naona aibu sana jamii inayonizunguuka ikija kufahamu hii habari. naombei mnisaidie wakuu nifanye nini kuondokana na aibu iliyo mbele yangu? Kuhusu kumpeda nampenda sana binti na nina mpago aje awe mama wa watoto wangu lakini sio kwa kuzaa nje ya ndoa.

Kijana mkimya heshima kwako!!!,Mimi ninakushauri kuwa uache mara moja mpango wako muovu wa kutaka kuua kiumbe kisichokuwa na hatia,Mkuu hiyo ni dhambi kubwa sana mbele ya Muumba wetu,mwenye Mamlaka na uweza wa kuondoa pumzi ni yeye aliyetuumba hivyo ni bora ukamwacha huyo binti azae kosa litakuwa dogo kuliko kutoa mimba,Usiogope aibu wewe ni mtoto wa Kiume kuwa kauzu zaidi ya Kaka kuona,Si ulitaka chai ukamvua chupi mtoto wa mwenzio kula bati hadi kiumbe kizaliwe;Halafu mtoto akishazaliwa nakushauri umuoe huyo binti Ndoa mtafunga baada ya kuweka mambo yote sawa;Nakuambia kinyume na hapo Mkong'oto utakaoupata kutoka kwa aliyekuumba ni babu kubwa kiasi ambacho utatamani Dunia hii ipasuke na wewe ujifukie humo.Chonde sana usifanye unyama huo nakuomba sana mkuu.
 
Wakuu,

Naomba mnisaidie kwa hili.

Nimempa mimba mdogo wa rafiki yangu kipenzi, namuambia aitoe hataki. sio kama sina uwezo wa kumuhudumia ila naogopa jinsi watu watakavyonichukulia kutokana na status yangu.

Naona aibu sana jamii inayonizunguuka ikija kufahamu hii habari. naombei mnisaidie wakuu nifanye nini kuondokana na aibu iliyo mbele yangu? Kuhusu kumpeda nampenda sana binti na nina mpago aje awe mama wa watoto wangu lakini sio kwa kuzaa nje ya ndoa.

Wakuu ebu nisaidieni katika hili, nimshauri vipi huyu mtoto akubaliane nami maana anakataa hataki kusikia kabisa habari hizo.

Rafiki habari ya uzima?
Nimesoma maelezo yako na kwakuwa umeomba ushauri basi nimeona ni vyema nikachangia. Kwanza kuna jambo naomba niliweke sawa, unaona aibu namna ambavyo watu watakutazama kiasi cha kumsahau Mungu?! Tunapenda dhambi kuhofia aibu?! Watu na Mungu ni nani umempa kipaumbele?! Kuna kitu kimoja huwa tunakosea, tunapenda kufanya jambo lenyewe lakini matokeo ya kulifanya jambo husika huwa hatupendi. Tunapenda ngono lakini matokeo ya ngono hatupendi. Yet unasema unapenda awe kuwa mama watoto wako kitu ambacho sidhani ukweli wake, unajua madhara ya kutoa mimba? Kifo ama kupoteza uwezo wa kuzaa, je ni kweli unampenda huyo binti kiasi cha kumtakia kifo ama kumsababishia uwezo wa kupata mtoto? Hebu kuwa muwazi. Status yako iumize wengine Kaka? Status mbona haikukuzuia kuwa na mahusiano nae na kufanya nae mapenzi?! Sikushambulii Ila nataka nikusaidie japo kwa njia ngumu (learn the hard way). Hakuna anayejua namna tulivyozaliwa. Jambo limekwishakutokea kubaliana na matokeo. Humtaki wewe mwache azae Mungu ndiye baba wa yatima na mume wa wajane. Unampenda muoe. Kuzaa kwake hakukuzuii wewe kuwa naye kama unampenda. Kila mtu ana status, hata huyo binti ana status Ila amekubaliana na hiyo hali why not u?! Aibu ya wanadamu na nafasi yako ktk jamii isikufanye ukamkosea Mungu. Damu hiyo itakulilia kama ya Abili. Nenda kaongee na wazee wafanye vikao kama wampenda, nenda katengeneze heshima yako kwa kuonyesha hekima ktk kukubali kuhudumia malenzi and the like. I'm a man Ila sikubaliani Kabisa na utoaji wa mimba kwa kukwepa majukumu au kwa ajili ya ubinafsi (status). Asante kwa kusoma ujumbe wangu.
 
"A man has to accept his fate or to be destroyed by it"-Quintus lentulus Batiatus.
 
Wakuu,

Naomba mnisaidie kwa hili.

Nimempa mimba mdogo wa rafiki yangu kipenzi, namuambia aitoe hataki. sio kama sina uwezo wa kumuhudumia ila naogopa jinsi watu watakavyonichukulia kutokana na status yangu.

Naona aibu sana jamii inayonizunguuka ikija kufahamu hii habari. naombei mnisaidie wakuu nifanye nini kuondokana na aibu iliyo mbele yangu? Kuhusu kumpeda nampenda sana binti na nina mpago aje awe mama wa watoto wangu lakini sio kwa kuzaa nje ya ndoa.

Wakuu ebu nisaidieni katika hili, nimshauri vipi huyu mtoto akubaliane nami maana anakataa hataki kusikia kabisa habari hizo.

nyie watu huwa mnanishangaza sana, mkiwa mnafanya mapenzi huwa hamuwaz mimba ikitokea itakuwaje ila ikitokea mnaanza kuleta tabu sijui ni kwanin,muogopeni mungu jaman, msiwe na roho ngumu kiasi hicho jaman daaah....
 
Mama watoto mtarajiwa halafu unataka atoe mimba!? Muulize Wema Sepetunga, atakupa majibu ya kuchoropoa....
 
''naogopa jinsi watu watakavyonichukulia kutokana na status yangu''

Ulipaswa kumuogopa Mungu kabla ya uzinifu

''naogopa jinsi watu watakavyonichukulia kutokana na status yangu''

Bado hujapevuka kiakili kama kila linalokupata unalipima kwa kuangalia watu watakavyokuchukulia. Status yako ni ipi?!

''naombeni mnisaidie wakuu nifanye nini kuondokana na aibu iliyo mbele yangu''

Unadhihirisha kutopevuka zaidi kwa kuona kuwa kumpa binti ujauzito ni aibu

''huyu mtoto akubaliane nami maana anakataa hataki kusikia kabisa habari hizo''

Unataka kuongeza kosa lingine kwa kuficha la kwanza? Kutoa mimba ni dhambi (aibu katika mtazamo wako)..
Kwanini unamuita mtoto wakati huyo ni mama mtarajiwa kwa sasa?

Wakuu,

Naomba mnisaidie kwa hili.

Nimempa mimba mdogo wa rafiki yangu kipenzi, namuambia aitoe hataki. sio kama sina uwezo wa kumuhudumia ila naogopa jinsi watu watakavyonichukulia kutokana na status yangu.

Naona aibu sana jamii inayonizunguuka ikija kufahamu hii habari. naombei mnisaidie wakuu nifanye nini kuondokana na aibu iliyo mbele yangu? Kuhusu kumpeda nampenda sana binti na nina mpago aje awe mama wa watoto wangu lakini sio kwa kuzaa nje ya ndoa.

Wakuu ebu nisaidieni katika hili, nimshauri vipi huyu mtoto akubaliane nami maana anakataa hataki kusikia kabisa habari hizo.
 
Hakuna watu wanaoudhi kama wanaolazimisha kutoa mimba!
Kama hutaki kumuoa ni bora ukapotea kabisa atajua mwenyewe cha kufanya. Hiyo status yako mbona haukuitizama kabla ya kummanua!!
 
Hivi hakuna uwezekano wa huyu ----- tukamripot tcra wamkamate ni kwanini anataka kuua kwa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu
 
Aibu gani sasa? Status yako ipi? Duuuh sifa nyingi unajipa ila akili KIDOGO.
 
Wewe una status gani au ndio hawa madiwani wateule wa Ukawa wanaotupa tabu huku mtaani...
Acha upumbavu wewe kwanini umnyime kiumbe mwenzako haki ya kuishi
 
Embu Jiulize Kwanza Ingekuaje Mama Yako Angeitoa Mimba Yako?..Je Ungekua Hapo Ulipo Au Lah?..Je Unafahamu Ni Jinsi Gani Ww Ulipatikana?..Jiulize Ndugu..Ukiitoa Usahau Kuipata Tena.
 
Lipi jema. Kutoa mimba au kurasimisha awe mke?
 
Back
Top Bottom