Nimemnyang'anya 'beki tatu' simu, je nimekosea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimemnyang'anya 'beki tatu' simu, je nimekosea?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ndyoko, Nov 9, 2011.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Kuna katabia kasiko ka kawaida nilikaona kwa beki tatu wetu. Kuna wakati niliambiwa kuwa tukitoka home, baada ya muda mfupi kuna vivulana vilikuwa vikija. Kuna siku tulitega mtego na kweli ndege wakanasa. Tulitoka asubuhi kwenda kwenye mishemishe zetu, kumbe huku nyuma beki tatu akawasiliana na bf wake, kavulana kakaja home, ndani ya robo saa nikarudi kweli nikakuta mvulana wamekaa sitiing room wanachat kwa raha zao.

  Nilipoingia ndani waliduwaa, nadhani hawakutegemea, wasijue wafanye nini. Nilimkamata dogo nikampa vibao vya haja dogo akatoka mkuu akiugulia mambata niliochapa. Nikamgeukia beki tatu nikamnyang'anya simu nikamwambia nitampa atakapoenda likizo. Amenuna kishenzi lakini hana jinsi. Tangu siku ile, nimeambiwa sasa hivi hakuna hizo movement tofauti na awali alipokuwa na simu. Kuna siku moja nikaamua kuiwasha ile simu, walai, kuna kama vi boy friend vyake vitatu vinadai mbona siku hizi hawaambii waje home, kwani kuna nini au sisi waajiri wake tuko likizo kwa hiyo muda mwingi tuko home ndo maana hawaambii waje?

  Wakuu jaribuni kuwa makiini na hawa beki tatu, kwani wengi wao hatuwajui tabia zao. Tunapokuwa kazini ni mengi yanatokea huku majumbani mwetu, mweeeeeeee! Chukueni tahadhari, huenda nyumba zetu zinageuka madanguro ya muda tunapokuwa makazini. Huenda nimefanya kosa kumpora mobile yake, lakini uamuzi wangu nahisi ni wa heri na ntamrudishia tu atapoenda likizo kwao Makete.

  Mwenzenu nimefunguka akili, wewe je?
   
 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,970
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  umemkosea heshima.hebu fikilia wewe boss wako akunyang'anye simu utajiskiaje.kama umemchoka mrudishe kwao kuliko kumnyanyasa kwa vitu vodogo vidogo.kwani nyie ndo mtamuoa?.au hamtaki awe na malafiki.kwani yeye mfungwa?.acheni ukilitimba.mia
   
 3. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hongera kwa kutambua mabaya ambayo anayafanya beki tatu wako,kuna mambo yananitatiza kidogo na naomba uniweke sawa.
  1.Wakati unanchukua huyo beki tatu ulikuwa unajua kuwa ni mtu mzima na atakuwa anahitaji haki zake za msingi za kuwa na mahusiano?
  2.Ulipokuwa unamnunulia simu au kukubali awe na mawasiliano ulitaka awe anawasiliana na nani?
  3.Je siku hizi ukiwa na tatizo au nyumba yako ikiwa imevamiwa au kuugua ni nani atakupa taarifa?
  4.Ulishindwa nini kumwambia kuwa pale kwako hutaki waje wavulana na kumwachia simu?
  Ni hayo tu mkuu.
   
 4. S

  SMART1 Senior Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani mzee unataka upige kazi, sema nae taratibu kwa upole anaweza akakusaidia na wewe.
   
 5. bht

  bht JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  ana umri gani ?
   
 6. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Mkuu sasa kama una beki tatu si inamana una wako halisi,mbona kama unamyima uhuru wakati kwako ni kama beki tatu tu.
   
 7. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,478
  Trophy Points: 280
  simu umnyang'anye na makofi juu, looo wewe baba una nini
  siku yaja utakuta kakabanika hako katoto kako kwenye oven
  usiache kuyaleta hapa jamvini.
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  ndo awalete kwangu, we unataka aniharibie watoto wangu. Hujui hawa watu huwa wanamalizana humo humo ndani ya nyumba wanazoishi wakati mwingine na watoto wa mwenye nyumba wanaangalia movie inavyoendelea. Huwa kila wikiend anapata free time kwenda kutembea, binafsi nilitegemea angemaliza huko hizo hamu zake
   
 9. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mmh! sijapenda,!! unajua mkuu na yy ni mwanadamu kama walivyo wengine,umemnyanganya cm lakini si gengeni anaenda basi jiandae kupata shemeji muuza genge!! mkalishe chini sema nae taratibu MRUDISHIE SIMU YAKEEEEEE!! ALLAA!!
   
 10. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Simu ni kwa ajili ya mawasiliano ya kujenga na sio kubomoa. Au unadhani kwa kuwa Mungu amekupa hicho kinaniii chako basi ndo ukitumie tu hovyohovyo hata kwa matumizi yasiyo na maadili? Au tuseme ukimuweka mlinzi akulindie mali zako basi ni ruhusa yeye kukuibia?
   
 11. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Inabidi tu ukubali kuwa umefanya vibaya...mrudishie mtoto wa watu simu yake!
   
 12. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Nilishamuimbia nyimbo zote unazozijua wewe kuhusiana na hii kitu. Na ndiyo maana wikiend yeye huwa anapata off ya kwenda mjini kutembea nikiamini huko ndo angemalizia hizo hamu zake. Nadhani amenogewa au huenda hao bf wake hawana uwezo wa kwenda guest ndiyo maana wanakuja kumalizana naye kwangu. Unajua kwako wewe unaona sawa beki tatu akifanyia mapenzi ndani ya nyumba yako ila mimi nadhani hiyo si sawa kabisa, binadamu tuko tofauti na ktk hili tumetofautiana
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hivi mkuu huyo House girl umemfunga gerezani? Kiasi kwamba asiwasiliane na marafiki zake? Unavunja katiba bana.
  Kwani huyo beki tatu ana umri gani? Naona unawaonea wivu hao maB/F wake
   
 14. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #14
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  yuko kwa age ya 25yrs
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,217
  Trophy Points: 280
  sikubaliani na kitendo cha housegirl kuleta vivulana vyake nyumbani kwako, atakuharibia watoto, nakumbuka wakati nikiwa mdogo housegirl alikua anatufungia balcon yeye anajirusha ndani, kama hatujala mchana huo imekula kwetu!! tukianguka tukaumia imekula kwetu, ila nashukuru sikujua wakitufungia huko wao ndani wanafanya nini la sivyo mmmmmh.

  lakini pamoja na yote hayo mrudishie huyo binti simu yake, asije zidiwa mihemko akamwinda baba watoto wako. lakini kabla hujamrudishia ni vyema ukazungumza nae umwambie ukweli hutaki vivulana vyake hapo, na ukimfuma nao tena hiyo ajira ndo bye bye, mweleza madhara ya mapenzi bila kinga na ajue akinasa hana lake hapo, maana kama ana umri wa miaka 25 huyo ni mtu mzima kama ana akili atashika maneno yako, meanwhile uwe unarudi home mara kwa mara mida tofauti msuprise ucheki anafanya nini.
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Nov 9, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Haaaaaaaa huyu ana haki kabisa ya kuwa na B/F hata kumi ni uwezo wake.
  Na hisi wewe tajiri wake unammendea unataka umege mwenyewe wivu huo
   
 17. Kimolah

  Kimolah JF-Expert Member

  #17
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 327
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  poleee, huwa ni ujana tu unawasumbua wengi wao, especially kama ulimtoa bush huko kaja kujanjarukia town... mpe chake rudisha kwao tafuta mwingine (tena ikiwezekana muwe related japo kidogo) , ataona haya kufanya mambo ya ajabu ajabu at your place. cha msingi shukuru Mola hao viboy (sijui nao ni age mate wake au anasalandiwa na viserengeti) hawajafanya shambulio hapo kwako, either wizi au hata kumrubuni kukuibia au kuwamolest watoto wako.
   
 18. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #18
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Mkuu taratibuuuuuuuu, mi mwanaume aisee, hebu nitake radhi bwana!
   
 19. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #19
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145

  Mkuu nilikuuliza maswali 4 lakini hujayajibu,kama simu ni kwa mawasiliano ya kujenga basi ungemjenga kwanza beki tatu wako juu ya matumizi bora ya simu pasi na kumnyang'anya.
  Kwenye red:Inaonekana beki tatu wako kuchukuliwa inakuuma sana,kunani mwenzetu???
   
 20. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #20
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  na hiyo ndiyo concern yangu kubwa halafu watu wanaona hii kitu ni nyepesi. Yaani mtu mzima unakubali beki tatu afanyie mapenzi ndani kwako, mi sijapata sikia hii. lakini binadamu tuko tofauti sana
   
Loading...