Roho yangu inaanza kukaa mbali na huyu ndugu yangu, je nina makosa mimi kutopokea simu zake?

Balqior

JF-Expert Member
Jun 8, 2021
1,709
5,688
Ni ndugu yangu mtu mzima, namwita shangazi, sijawahi gombana nae, na binafsi namwona ni mtu mwema kwangu, na nimefahamiana naye toka utoto wangu hadi utu uzima huu, kipindi cha likizo nlikuwa nashinda kwake miezi mingi kabla ya kwenda home, ila kipindi cha hivi karibuni amekua na tabia ambazo zimefanya roho yangu ianze kumkataa.

Kila mwezi atanipigia simu, hili la kunipigia simu sina shida nalo, Maana hata mm huwa nampigiaga simu.

TATIZO LINAPOANZIA:
Kila nikiongea naye kwenye simu, ananiuliza maswali ambayo mara nyingi mm binafsi sipo huru (comfortable) Kuyajibu daaah..

1)Kila akinipigia simu lazima aniulize nipo wapi, nikikwepesha kumjibu atanisisitiza mpaka nimwambie niko wapi..
2)Nikimwambia napigaa mishe za kilimo, simu zitakazofuata ataniuliza mara nne nne kilimo kiliendaje.
3)Muda mwingine ananiuliza kama biashara nilizofungua bado zipo
4)Kila akinipigia ananiuliza kazi nlizo-apply zimeendaje

Kutokana na hayo maswali hapo juu, yani nimeanza kujitenga naye kimya kimya mpaka yeye Kuna siku aliniuliza mbona najitenga nae, ila nahic hajajua kwanini namkwepa, ila in general shangazi yangu tangu nimfahamu amekuwa ni mtu mkarimu Sana kwangu.

Huyu shangazi yangu Huwa anasema baadhi ya ndugu Zake wengine hawapokeagi simu zake, nahisi ni kwasababu ya hii tabia yake ya kuuliza maswali.

Labda mm ndio nina tatizo, Wenye uzoefu naombeni mnipe mawazo yenu kwenye hili, ili kama nina makosa nijirekebishe
 
Unataka upewe nini Wewe katika maisha yako?????? Yaani umepata mtu ambaye anakufatilia katika +ve way kujua mambo yako yanaendaje. Rudia kusoma point yako namba 2&3 kwa umakini wa hali ya juu Utapata majibu. ACHA U**NGE
 
Wewe ndio mwenye tatizo.Sijaona tatizo shangazi(ambaye ni kama baba)kuuliza kijana wake maisha yanavyoenda.Kwani ukimjibu vile yanavyokwenda kuna shida?Shida iliyoko kwako unaanza kuhusisha mambo ya ushirikina ilhali shangazi anahitaji kusikia mazuri kutoka kwako.
 
Kila kitu lazima kuwa na KIASI na binadamu yeyote mwenye kutaka kufika mbali lazima ajifunze kutunza SIRI na Kuheshimu sauti ya ndani.

Yaani kama kuna mambo nafsi yako inasita kuzungumza kwa mtu fulani, acha usizungumze.

Tofauti na hayo mtu mzima anayetafuta siyo busara kuhoji kila hatua anayopitia katika maisha yake binafsi na ya utafutaji kiujumla.

Mkuu huna tatizo ila sauti yako ya ndani ndiyo unayotakiwa kuisikiliza.

Unapotamka malengo yako yote kwa mtu unakuwa kama upo uchi na hata hamasa ya kupambania lile lengo inashuka.
 
Tabia hizo inaonyesha anapenda kuharibu maendeleo ya watu, atakuwa anajaribukukufatilia kwa njia za giza na akishindwa anakuuliza ili afanye yake. Usishangae kwanini wengine wanamkimbia, itakuwa wamegundua kitu juu yake.

Endelea kukaa nae mbali, muhimu usimueleze issue zako zozote. Watu kama hao wanapenda kusikia mtu ana matatizo tu. Usiongee yako hata kwa watu wa karibu nae asiyasikie, ndio maana wengi tunafanya yetu na kunyamaza baada yanaonekana tu kama wakiyaona. Usimruhusu akaja kwako leo hata mbeleni.

Sali pia
 
Mmmmh akili yangu haitaki kumuhukumu hivyo, sababu ni mtu mwema kwangu, na sina ushahidi Wowote dhidi yake, anyways Mungu anajua vyote Keenly
 
Unaandaa mazingira ya kumkataa au sio? Usisahau ulipotoka Mkuu.

Mxiieeeuuu nikajua labda amekukonyeza ama akakutupia kapicha ka ajabu .
 
Unaandaa mazingira ya kumkataa au sio? Usisahau ulipotoka Mkuu.

Mxiieeeuuu nikajua labda amekukonyeza ama akakutupia kapicha ka ajabu .
Sina mpango wa kumkataa, ila tu maswali yake nliotaja kwenye huu uzi yananipa ukakasi, in general hana shida, ni mama mwenye heshima zake Karucee
 
Back
Top Bottom