Nimemliza mwanamke baada ya kumuuliza kama ameolewa

Nimemliza mwanamke baada ya kumuuliza kama ameolewa

flulanga

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2016
Posts
4,856
Reaction score
6,442
Ujue sisi tuliojiajiri mara nyingi tunatoka hadi jpili hata nusu siku inatutosha.

Kuna mdada alikuja kupata huduma, amejazia amevaa dira ila msambwanda kama upo upo tu unaonekana vizuri japokuwa upo kwenye dira, mtoto maji yakunde nakimuonekano anaafya nzuri sana.

Katika maongezi nikamchombeza, nikamuuliza umeolewa? akanijibu hapana..., nikamwambia kwanini ujaolewa nawewe wakati umri wako umekomaa?? Duh aiseee alichonijibu 'hayo tuyaache tuu' nikaona kainama kaanza kulia.... Akatoa lesso akaanza kujifuta machozi.....

Ikanibidi nimwambie anisamehe kwaswali langu kama nimemchoma pabaya.... Akanijibu nisijali. Nahadithi yangu ikawa imeishia hapo.

Hii imenitokea Leo jamani.
Dada zangu embu Leo niwaulize swali... Nikwanini nyinyi ndio wahitaji sana wandoa kuliko sisi? Kama wewe mwanamke uhitaji ndoa yaani wewe mmoja basi jua wapo wenzako laki moja nyuma yako wanahitaji ndoa.

Yaani kwanini nyinyi mnatuhitaji sana sisi kuliko sisi tunavyowahitaji nyinyi?? Au sisi ndio maswagi yenu?? Kwanini hamjisikii raha mkiwa nyinyi kama nyinyi tu? Au yule nyoka aliwaambia nini kuhusu sisi wanaume maana sio kwakulia kule kwayule binti aiseeee duh!!

USHAURI: jikubalini jamani, jitambueni ili janga liturudie nasisi wanaume. Ifikie hatua sisi wanaume ndio muanze kutunanga kwanini hatuoi kama vile sisi tunavyowanga kwanini hamuolewi, tuanze nasisi kuzitafuta ndoa kwa tochi.

Jumapili njema...
 
Wewe kuolewa kwake au kutokuolewa kuna kuhusu nini? alipokujibu hajaolewa ungeishia hapo kiistaarabu kabisa.
Kwani mkuu nilikuuliza wewe au dada zako wote hawajaolewa??
 
IMG_20191103_153907.jpg
Haya bhana
 
Back
Top Bottom