Nimemkamata mwizi wa Taa (balbu) usiku wa leo

Kweli hata mimi nilijua hilo ndio maana hata yeye hakujua nimejipangeje, cha kwanza nilimwambia NTAKUUA kwa ukali akaogopa asalimu amri,.
Siku nyingine ikijakutokea the same circumstance usiance na neno "NITAKUUA" coz litamfanya apanic na kufanya kitendo chochote ambacho labda hukujitaarisha nacho. Anza na neno "TULIA HIVYO HIVYO". Hii itamuondolea confidence ya kureact coz hajui umejizatiti kiasi gani.
 
Kumpeleka mtu Police ni sawa na kuwapelekea pesa ya ulaji police..Wewe ungekuwa na akili ungemwambia nigawie mpunga tumalizane.
sasa ulaji wamepewa police..Naamin kufika tu police amewachia 20,000 akachomoka zake..sasa mnaanza bifu ya mtaani isiyokuwa na sababu..mkimalizana na mchinjana huko Geita.
Jamaa alikua analia kama mtoto anatuomba tusipige yowe yaani tulimpiga mpaka huruma
 
Tukaamua tumpeleke police tukiwa njiani kuelekea huko njiani tukawekwa chini ya ulinzi na walinzi wa mitaani tukaelezea mwanzo mwisho wakatuelewa maana kidhibiti alikua nacho mwizi, tulirudi kulala walinzi tukawakabidhi mtu huyo ndio walimpeleka polisi.
Yaani Walinzi walishindwa kumkamata mwizi wanataka kuwakamata nyie tena? Huwa nalipa pesa ya Ulinzi Mtaani kwangu ila sijawahi kuona faida
 
Mkuu hujatuelezea kama ulipona tumbo.
Tumbo nilipona kabsa, kwa mshituko niliokuanao nilivyomuona anatoka kwa jirani kuelekea nyumbani kwangu

ndipo nilijihisi kusisimka mwili kama natembelewa na nyoka mgongoni tumbo likajawa hofu kama mtu amekoswa kugongwa na gari , tumbo sjui lilipona mda gani
 
Mmemkabidhi kwa walinzi wa mitaa ambao pamoja na uwepo wao bado jamaa alikuwa anajaza diaba na mitaa kuwa gizani?

Kwamba mnaamini watanfikisha kunakohusika kweli? Vipi wakiamua kuvuta chao na kumuachia huyo mwizi mtajuaje? Je mwizi wenu mlimtambua au ilikuwa sura ngeni? Maana kama mngemtambua angeogopa kuiba tena hapo mtaani lakini kama ni vinginevyo inakuwa ngumu kidogo kuamini kwamba mchezo mmeumaliza.
Sura ilikua ngeni nayeye alijitambulisha ametokea mtaa mwingne, kifupi usiku tulikua kama hatutumiii hakiri zetu asubuhi tumesimlia mengi yameibuka yaani tulifoji kwakwel
 
Mbona technique ya kutoa taa umeielezea kwa ufasaha sana?
Umeelewa hapo kwenye chupa kubwa ya dasani iliokatwa afu ikafungwa kwenye mti mlefu hakuna taa ya kuchomka hapo rabda taa ya fimbo
 
Umenikumbusha kisa kimoja, kuna siku tulikamata mwizi mtaani kwetu mishale ya usiku mkali sana kama saa nane hivi, tukaamua kumpeleka polisi kwa hatua zaidi za kisheria, ile tumemfikisha polisi tukaanza kushambuliwa na polisi wale kwa maneno eti wanaume tisa tunamleta mwizi kituoni hajavunjika hata miguu au mikono wakasema ni matumzi mabovu ya muda wa kulala bora tungemuachia tukalale.....
waumini waimbaji wa kwaya
 
Back
Top Bottom