Nimemfumania mke wangu, nimechanganyikiwa! Ushauri tafadhari...

pole kijana, pole sana wanasema is the greatest pain ever,
pongezi kwako- kwa uamuzi ulochukua baada ya kumfumania ndiyo uliko na hasira lakin hukumpiga hata mmoja wao,,
ulifanya pia vizuri kumpeleka kwa wazazi, ila ningependa uruhusu maongezi kati yako wewe nae kwanza,,
vipi mkeo anaonesha moyo wa kuomba msamaha au ilikuaje, ndugu hapo juu kauliza swali la msingi vipi walitumia kinga,,
ni vema mkazungumza wewe na mkeo kwa mapana na marefu, hivi ni kitu gani hasa ni tabia yake, kuna kitu kinakosekana katika mapenzi, au ni gani? je unamridhisha mkeo kimapenzi? mnafanya mara nyingi apendavyo, upendavyo mpendavyo?
psychologia ya mapenzi inasemaje? mwanaume anaweza kutoka ni kawaida kwa wanaume wengi, sasa ukiona hata mkeo nae anatoka labda anajua unatoka na ameshindwa kukuambia na amejichukulia maamuzi pekee? au anakosa kitu? anything is rit
kinachouma apa ni kumfumania sio? jiulize ni mazuri mangapi mnafanya pamoja. mnaenjoy mapenzi mara ngapi. mbona hili limekua kubwa kwako kiasi unataka kumkatakata
je? hakuna tatizo jingine lolote kati yako wewe na mpenzi wako, lililotokea karibuni? ambalo unaweza ukalihusianisha na hili jambo? naamini mara nying hii ni triger tu kuna mambo mengi ups and down
jambo jingine usione ati huu muda ni mwingi saana at 13yrs, wengine tuna 13yrs baada ya drs la saba na bado tunasoma ni kitambo kidogo tu,, LOVE LAST IT'S ETERNAL
kwa ufupi unamjua mkeo kuliko mtu mwingine, yafaa kumsikiliza pia bibie jugdement ya upande moja haifai,,
ila kama upo CLEAN, HUJAWAHI TENDA JAMBO LISILO BAYA KWA MKEO,, , MAANDIKO YASEMA KOSA LA KUMFUMANIA MKEO WAWEZA FANYA MAAMUZI KUMWACHA MAANA UMEMWACHA KWA UZINZI
 
Wana JF nimeoa na nina mtoto mmoja ana miaka minne,nimemfunia mke wangu anafanya mambo na kijana fulani wa mtaani hapa hapa.Nimemrudisha kwao ila naona kama adhabu haitoshi kuna muda natamani kama nimkatekate vipande vidogo vidogo vya nyama au hata niende kwa mganga amfanye chizi.Bado wazazi wamekutana wanasema nimsamehe.Naomba busara zenu wanaJF ila pia nawapeni somo msiwaamin wanawake anaweza kukugeuka siku yoyote,mm mke wangu nimetoka nae shule ya msingi mpaka mwaka huu ni zaidi ya miaka 13

Wapi shule ya msingi hata ukitoka nae wodini siku ya kuzaliwa.Haya hicho kibwagizo.
Pole sana kakangu kwa mkasa huu uliokupata.Jiulize wewe ulishacheat kwake mara ngapi?kama hujawahi hongera na rudi kwenye maandiko ya dini yana sema samehe mara ngapi?na note sikuladhimishi kusamehe ni jukumu lako waweza kusamehe na uka divorce pia kama utapenda maana hiyo kitu hata kanisani unaambiwa kabisa mutangenganishwa kwa ugoni.

Nakuomba musichukulie ngao ya watoto.maana waweza kupata matatizo zaidi kwa kutumia kinga ya watoto kutoa msamaha.
Huwo ujasiri wa kumurudisha kwao nakupongeza sana maana ingewezekana kutokea kwa jambo lolote baya zaidi.
Ilaa swahiba na wewe jiangalie na vijitabia vyako waweza kuwa una mkera ndo sababu kaamua kutoka na kijana.
japo nyie hampendi kusemwa na sie wake zenu.ila uwa kuna vimaudhi vya hapa na pale ni vyema kusikiliza wife anachokwambia jamani.
 
ila pia nawapeni somo msiwaamin wanawake anaweza kukugeuka siku yoyote,mm mke wangu nimetoka nae shule ya msingi mpaka mwaka huu ni zaidi ya miaka 13

Ndugu the muter,
Kwa kweli nakupa pole sana...sina ushauri hapo nitakuwa naongea hypothesis kama bw. Kiranga.
Ushauri wangu kwa wana JF: Kama ndoa yako haiko rooted in Christ then it is all in vain.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu pole sana. ni situation ngumu sana, Nakuombea hekima na Busara. Jitahidi kumsamehe mkuu, maana kumsamehe hakumaanishi utamrudisha kuwa wife tena, kusamehe ni kitu kingine na kumrudisha ni kitu kingine. ''amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati, naye akaoa au yule akaolewa afanya uzinzi'' so if ya a Christian, you are released.

Lakini mkuu ni nani huyo asiyeanguka hata awe wa kwanza kumpiga jiwe huyu aliyeonekana? nakusihi ujitahidi sana kuomba kwa Mungu wako, atakupa kusamehe. Naye wife akitubu kweli na kujutia kweli makosa yake, Mpokee tena mkaendeleze familia yenu, maana pia imeandikwa ''usimuache mke wa ujana wako''
 
Pole kwa yaliyokukuta,Pia pongezi kwa ujasiri ulonao.....kitu cha msingi ninachokiona ni wewe uchunguze ni nini kilichomfanya mkeo mpaka akangonoka na kidume kingine,Ukipata jibu waweza kuchukua uamuzi sahihi.
 
Kusamehe ni muhimu sana, ila kujilazimisha kusamehe ni Hatari zaidi ya kukutana na simba..usikimbilie kuoa mwingine, tulia na usifanye revenge. Pia kama wewe una dini inayoamini MUNGU(GOD THE ALMIGHTY) yupo, mwombe akuonyeshe njia sababu kila jaribu lina mlango wake wa kutokea.utafute huo mlango.
Pole sana.
 
Pole ila Chimbuvu amekupa swali poa sana, wewe toka umeoa umemsaliti mara ngapi? Pia kusema usiamini wanawake wanaweza kusaliti si sahihi. Tabia ni ya mtu si gender yake. Kama nawe unazini nje msamehe na mjirekebishe wote na hiyo dhambi.
 
Last edited by a moderator:
Pole brother! Huyo mwana mke hakufai, usariti upo ndani ya damu yake, hata mkiludiana ni kazi bure, ataludia madudu
 
Wala usimtangaze kwa watu na kuomba ushauri. Jipe nafasi, moyo ni kitu cha ajabu sana. Utamsamehe tu, usijikimbize. Be cool, angalia mwanao
 
pole sana, dah! hawa viumbe ni dhaifu sana, saa zingine unaweza usiamini macho yako, halafu anaweza akakuruka! dah so sad!
 
Mungu atusaidie sisi ambao hatumo ndani ya ndoa,mnatutisha sana,kila siku kisanga kipya,pole sana ndugu mfumaniaji.
 
pole kaka, msamehe bt usimrudishe kwa sasa, ishi mwenyewe ukiendelea kujitafakari na ye ajitafakari huko aliko, ningekua mimi ningekaa hata six months
 
Wana JF nimeoa na nina mtoto mmoja ana miaka minne,nimemfunia mke wangu anafanya mambo na kijana fulani wa mtaani hapa hapa.Nimemrudisha kwao ila naona kama adhabu haitoshi kuna muda natamani kama nimkatekate vipande vidogo vidogo vya nyama au hata niende kwa mganga amfanye chizi.Bado wazazi wamekutana wanasema nimsamehe.Naomba busara zenu wanaJF ila pia nawapeni somo msiwaamin wanawake anaweza kukugeuka siku yoyote,mm mke wangu nimetoka nae shule ya msingi mpaka mwaka huu ni zaidi ya miaka 13

kutokana na id yako inabidi uwe mute kweli kwanini unataka kumuua mtu wakati ushamkimbiza let her go and you will stay safe hata mungu atakusaidia kijana usifikirie hivyo sana.. pole sana mkuu...:A S angry:
 
Yani yani yani yaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, hili jambo bora kulisikia, yani yani my wife m2 anamndoa loooh! Hongera sana Mkuu kwani uvumilivu ulio nao ndio silaha ya maisha yako. Usingekuwa nao tungekusoma magazetini na kukuangalia runingani ukiwa umeshatenda...Upe moyo wako muda, kuhusu wazazi kuanza vikao vya kurudisha hilo haliwahusu saana kwani mlishawaacha mkaambatana, baada ya utulivu utapata jibu la moyo wako kati ya kumwacha au kumsamehe ila kama utaamua kusamehe yeye mwenyewe ajutie makosa yake na kuomba msamaha na sio wazazi au washenga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom