Nimemfumania mke wangu, nimechanganyikiwa! Ushauri tafadhari...

the muter

JF-Expert Member
Oct 31, 2012
1,312
1,743
Wana JF nimeoa na nina mtoto mmoja ana miaka minne, nimemfunia mke wangu anafanya mambo na kijana fulani wa mtaani hapa hapa.

Nimemrudisha kwao ila naona kama adhabu haitoshi kuna muda natamani kama nimkatekate vipande vidogo vidogo vya nyama au hata niende kwa mganga amfanye chizi.

Bado wazazi wamekutana wanasema nimsamehe.

Naomba busara zenu wanaJF ila pia nawapeni somo msiwaamini wanawake anaweza kukugeuka siku yoyote, mimi mke wangu nimetoka nae shule ya msingi mpaka mwaka huu ni zaidi ya miaka 13
 
Duh kijana wa mtaa alikuwa anakukuruka kwa kitumbua cha mkeo duh noomaa, JE walitumia kinga...?
 
the muter

Ushauri wangu mimi ni kuwa usijilazimishe kumsamehe. Kama moyo wako unakataa kumsamehe, basi na iwe hivyo... usimsamehe eti tu kwa sababu ya kutaka kuwaridhisha watu fulani, utakuja kufanya mambo mabaya sana huko mbele ya safari
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa hilo.wewe toka umuoe hujawahi tembea nje ya ndoa?
Mkuu, tatizo ni kufumania au kufumaniwa. Wengi wanatembea nje ya ndoa lakini inakuwa kama siri hivi... tatizo linaanzia pale mtu anapokuwa na ushahidi wa asilimia zote kuwa kaibiwa
 
Jesus . . . . . .!!Wewe huwezi kusamehe kulingana na ulivyoonesha hasira zako.
"
Kaa mbali na mkeo,acha muda upite kisha ujikague upya.
"
Najihisi kama akili yangu haifanyi kazi vyema,sijui kwanini!Aaaaaggggrrr!!!!
 
Pole sana mkuu,tukio kama hilo linatia hasira sana,mi naomba ishu kama hii iendelee kuwa story
kwangu,maana ikinitokea live,i will die na hasira.
 
pole mkuu kwa sasa una hasira sana waweza kufanya baya na ukajiletea matatizo zaidi mwache huko kwao alipokwenda hasira zikishapungua utaweza kutoa maamuzi kama ni kumsamehe au kuachana nae
 
Kwanza nakupongeza kwa jinsi ulivyolishughulikia jambo hili. Maana kama ni kuharibu, mara nyingi watu huharibu siku ya kufumania. Hapo ushavuka na maisha lazima yasonge mbele bila ya huyo mwanamke! Be strong, talk to people, and if possible go for counselling na uwe wazi kuwa una-intertain mawazo ya kudedisha mtu. Utasaidiwa and before you know it, utakuwa ok!
 
Pole sana ndugu, kwa sasa usifanye maamuzi ya haraka, kuwa na subra Mwenyezi Mungu atakujaalia busara ya namna ya kuliweka sawa jambo hilo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom