Nimemaliza mkataba kazini,je,haki zangu ni zipi?

Mgimilamaganga

JF-Expert Member
Mar 31, 2019
266
257
Habari za muda huu wakuu,

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.Nilikuwa nafanya kazi ya Security kwenye kampuni moja hapa jijini Dar Es Salaam.Sasa jana ndio nimefikia mwisho wa mkataba wangu wa mwaka mmoja,na kwa taarifa nilizopewa ni kuwa mkataba hautahuishwa kwani kampuni imepungukiwa na vituo vya kazi.

Naomba msaada wa kujua haki za mfanyakazi aliyemaliza mkataba wake tafadhali.

Asante.
 
Kama ulipewa taarifa kabla ya mwezi mmoja kuwa hutasaini mkatana mpya, hapo huna chako ila kama hujaambiwa utalipwa notisi mshahara wa mwezi mmoja....
 
Haki zako zimo ndani ya mkataba uliosaini.
Ndio zimeainishwa pale lakini siyo guarantee kwamba zitafuatwa kwa sababu hata nakala ya mkataba sikupewa,walibaki nayo wao.Ninachokihitaji ni sheria ya kazi inasemaje juu ya mtu aliyemaliza mkataba?
 
Kuna nauli ya kukurudisha kwenu kama ulisema wewe ni wa Mikoani
Kuna likizo ya malipo kama hujawahi kwenda wa kulipwa likizo (basic salary) nk
 
Mimi niliambiwa jana wakati nafuatilia mkataba mpya.
Kuna nauli ya kukurudisha kwenu kama ulisema wewe ni wa Mikoani
Kuna likizo ya malipo kama hujawahi kwenda wa kulipwa likizo (basic salary) nk...
Kama uliambiwa ghafla una haki ya kulipwa notisi ya mwezi mmoja
 
Kama ulipewa taarifa kabla ya mwezi mmoja kuwa hutasaini mkatana mpya, hapo huna chako ila kama hujaambiwa utalipwa notisi mshahara wa mwezi mmoja....
Je,huo mshahara wa mwezi mmoja haujumuishi malipo ya likizo?

Kwa utaratibu uliopo nilitakiwa niende likizo baada ya kumaliza mkataba(likizo yenye malipo).
 
Kuna nauli ya kukurudisha kwenu kama ulisema wewe ni wa Mikoani
Kuna likizo ya malipo kama hujawahi kwenda wa kulipwa likizo (basic salary) nk...
Kama uliambiwa ghafla una haki ya kulipwa notisi ya mwezi mmoja
Notisi ya mwezi mmoja kwa mtu ambae mkataba unaisha??..nachojua mimi notisi anapewa mtu ambaye mkataba wake haujaisha but ngoja wadau wengine wazoefu waje walete experience yao humu
 
Kuna nauli ya kukurudisha kwenu kama ulisema wewe ni wa Mikoani
Kuna likizo ya malipo kama hujawahi kwenda wa kulipwa likizo (basic salary) nk...
Kama uliambiwa ghafla una haki ya kulipwa notisi ya mwezi mmoja
Nimeshakuelewa hapa.

Kwa hiyo nastahili kulipwa basic salary na fidia ya mshahara wa mwezi mmoja kwa kutokupewa notisi kuwa mkataba hautaongezwa.

Sasa hapa ndio patakuwa na ugumu,huyu mhindi hataelewa.
 
Kwisha kwa mkataba hakunaga notice. Hapi ni kudai kulipwa likizo tu. Chukua bRua uende NSSF kufuatilia mafao.
 
Habari za muda huu wakuu,

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.Nilikuwa nafanya kazi ya Security kwenye kampuni moja hapa jijini Dar Es Salaam.Sasa jana ndio nimefikia mwisho wa mkataba wangu wa mwaka mmoja,na kwa taarifa nilizopewa ni kuwa mkataba hautahuishwa kwani kampuni imepungukiwa na vituo vya kazi.

Naomba msaada wa kujua haki za mfanyakazi aliyemaliza mkataba wake tafadhali.

Asante.
Zimeandikwa kwenye mkataba wako
 
Kwisha kwa mkataba hakunaga notice. Hapi ni kudai kulipwa likizo tu. Chukua bRua uende NSSF kufuatilia mafao.
Kuisha kwa mkataba mfanyakazi ni lazima apewe taarifa mwezi mmoja kabla ya kuisha kwa mkataba.
Mwajiri akikaa kimya maana yake amekubali kuongeza mkataba au alipe mshahara wa mwezi mmoja.
 
Back
Top Bottom