Kwa wale wawekezaji wa ndani na wenye viwanda (Mwijage) kama mie hasa kusaga nafaka naomba niwape ushauri kidogo.
Biashara hii ni nzuri kwa mtu mwenye shughuli nyingi kwani inahitaji minimum physical supervision.Unaweza kukaa nyumbani na ukajua mapato yako huku ukiangalia kiasi cha umeme kilichotumika na kujua mwenendo hasa wa biashara.
NIMELIZWA-Utaratibu wangu ulikuwa ku calculate shilling/unit of electricity na nilijiwekea kiwango ambacho niliona kina tija.Zilipoingia meter za Luku ndio nikafurahi zaidi kwani najua kiasi nilichonunua na kipato nilichopata.
Juzi juzi mfanyakazi wangu wa muda mrefu alifiwa na ikabidi nilete mtu mwingine na maajabu yakatokea,mtumishi mpya alileta mara tatu ya kipato cha mtumishi mzoefu.Hili lilinistua na kesho yake ikawa hivyo hivyo na ndipo nilipofanya upelelezi.
Nilichogundua ni kuwa mfanyakazi mzoefu alishajua ni kiwango gani nahitaji kwa kila unit na alichofanya yeye ni kunipatia kiwango hicho huku akinuua na kuweka umeme wake.
Nilipokwenda Tanesco kufuatilia records ndipo nikastuka zaidi kuwa kwa kutwa alikuwa akiweka unit zake kati ya kumi na 15-20.
Kagueni manunuzi ya umeme Tanesco kila wakati.