Biashara ya Kusaga na Kukoboa: Uzoefu wangu wa miezi 15

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Ndugu zangu, mwaka jana July 2021 nilinunua mashine ya kusaga na kukoboa na kuifunga Tanga mwezi wa Septemba, 2021.

Mchanganuo wa Vifaa:-

1. Mashine ya Kusaga

Kinu size 75 - 1,200,000
Mortor 30hp - 1,300,000
Starter(On/Off)- 300,000
Pulleys 2 - 100,000
Mikanda 3 - 15,000

2. Kinu cha Kukoboa

Kinu rollers 3 - 1,200,000
Mortor 30hp - 1,300,000
Pulleys 2 - 100,000
Switch - 300,000
Mikanda 3 - 45,000

Vifaa vingine vya umeme:-
1. Main Switch 3Phase - 190,000
2. Socket braker 100A- 60,000
3. Wires, taa, earthrod,clamps, switches - 150,000

Vifaa vya usimikaji mashine
1. Channel/Chasis cha chini (2)- 250,000
2. Cement mifuko 2 - 29,000
3. Mchanga ndoo 30 - 15,000
4. Guta la Kokoto - 30,000
5. Usafiri Guta ( 2,3&4) - 10,000

Ufundi:-
1. Umeme - 200,000
2. Ujenzi/Mechanical - kufitisha vinu chini - 150,000

Gharama ya kufunga umeme 3 phase (jumla) - 1,200,000

Kodi ya frame - 50,000 kwa mwezi.

Ikumbukwe, umeme wa 10,000 unapata units 28.

MAPATO:
(Ukiwa huna mahindi)
Umeme wa 10,0000 = units 28= 28*1,000 = 28,000/=
(Faida 28,000-10,000=18,000)

Umeme wa 100,000, faida 180,000
etc etc.

Kwa kipindi cha miezi 15 niliyofanya kazi, nimetumia units 12,500 sawa na mapato ya sh 12,500,000/=

Hizi ni bei halisi na nimehusika fully mwenyewe kila hatua ya mradi huu mpaka sasa.

USHAURI:

Ukitaka kufungua mashine za kusaga na kukoboa, tafuta mtaji hata wa gunia 5 za kuanzia, maana wateja huenda mashine yenye mahindi, hivyo utauza MAHINDI, PUMBA na UNITS ZA UMEME kwa haraka.

Ikumbukwe, gunia 1 linatoa debe 3 za pumba, na kila debe ni 4, 000 ( bei ya sasa 2022 November)

Sina mtaji wa mahindi. Mahindi naletewa na watu/wateja, mm kwangu faida ni units za umeme zinavyopukutika.

Biashara sijaisajili, sina leseni bado.

Naombeni wazo la namna ya kuweza kukopesheka.
 
Hizi ni bei halisi na nimehusika fully mwenyewe kila hatua ya mradi huu mpaka sasa.

USHAURI:
Ukitaka kufungua mashine za kusaga na kukoboa, tafuta mtaji hata wa gunia 5 za kuanzia, maana wateja huenda mashine yenye mahindi, hivyo utauza MAHINDI, PUMBA na UNITS ZA UMEME kwa haraka.

Ikumbukwe, gunia 1 linatoa debe 3 za pumba, na kila debe ni 4, 000 ( bei ya sasa 2022 November).
 
Mkuu sijaelewa hapo kuwa na gunia za mahindi na kuhusu wateja wanaenda kwenye mashine yenye mahindi ebe fafanua
 
Hizo ndiyo mada nzuri kwa vijana kuchangia na kupata mawazo Chanya, sio Kila muda kuwaza ngono tu.

Kuna mwenye uzoefu na mashine za Dizeli kuhusu faida? Kwa changamoto hii ya Umeme iliyopo nafikiria kufunga mashine ya kutumia Mafuta/Dizeli
 
Nakushauri ufunge ya umeme.

Ya dizeli ni changamoto sana brother. Hasa kwenye moto ake juu ya mortor. Zinaunguza sana mortor.

Imagine unanunua mortor kwa 1.3m then iungue?! Japo una uwezo wa kuisuka upya kwa 500 hadi 700k
 
Back
Top Bottom