kombaME
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 2,115
- 2,822
Habarini za weekend, naamini mmejiandaa vyema kesho kuanza kazi.
Wapendwa jana katika pilika pilika za weekend nikapata call mpya, akajitambulisha ni rafiki yangu aliliwa kichwa miaka hiyo tukiwa chuo tunapiga hizi kozi za afya.
Amenikumbusha huzuni niliyopata siku ile, siku ambayo matokeo yalipotoka na jamaa akapata red card, ilikuwa siku ya huzuni sana, ilikuwa ni siku ya simanzi kwangu. Nilijaribu kutumia maneno mengi ya kumfariji lakini hayakuwa na msaada, tulipojaribu kwenda kukutana na chief labda amsaidie hata kurudia mwaka ndo ikawa kama tumeenda kuchukua machungu, nakumbuka jibu lake "kuitwa dokta sio lazima utibu watu, unaweza kutibu hata ng'ombe na bado ukaitwa dokta". Alipanda gari kuelekea mkoani huku akinisisitizia kukomaa maana huzuni anayopitia sasa ni kubwa na asingependa niipitie.
Tulikuwa tunawasiliana baadae akaniambia anahisi tupo kwenye status tofauti so kila anapoendelea kuwasiliana na mimi anakumbuka chuo na kuzidi kuumia akabadili namba ikawa ndo mwisho wa kuwasiliana.
Nimekutana naye tena, ni furaha sana maana nimemuona amenawiri vizuri na aliamua kuachana na kozi za afya na akasoma mambo ya kompyuta na ni mwajiriwa wa kampuni moja na yupo vizuri. Nimependa tu kushare nanyi jambo hili, usiku mwema.
UJUMBE WANGU, MSIKATE TAMAA