Nimekutana na monitor wangu wa darasa amechoka, yaani amechakaa kinoma!

Poker

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
5,420
14,671
Milima haikutani ila binaadamu hukutana. Leo katika mishe zangu za hapa na pale nikabahatika kukutana na kiranja wangu wa darasa ametoka kufanya interview katika moja ya ofisi humu town.

Katika salamu za hapa na pale ikabidi nimkumbushe namna alivyokuwa kiherehere shule, kila siku kuniandika noise maker, mbaya zaidi nilishapewa adhabu ya kung'oa visiki kisa alinichongea nimemtukana. Mbaya zaidi alishanichongea kwa discipline master nimemchungulia mwalimu wa kike chooni, sitasahau siku hiyo hiyo walimu walinichangia staff room pale mpaka jasho linawatoka!

Yaani nilichezea kichapo mpaka kutembea siwezi najiburuta, darasani kwenye kiti ukikaa maumivu kama yote. Yaani kila nikimwangalia simpatii jawabu. Hakuchoka kali zaidi akaja nichoma nimeiba nyama jikoni nakumbuka ilikuwa siku ya graduu! Nikapelekwa staff tena mwalimu mmoja kanishika miguu mwingine mikono aisee nilichezea stiki za ujazo wote, nilipoachiwa na shule nikatoroka mpaka home kuulizwa kulikoni nikasimulia, kesho yake nikarudishwa shule nikalimwa suspension ya wiki 2.

Siku ya kuripoti likaitishwa parade pale shule kwahiyo nilikuwa nimekuja na rafiki wa mshua kama mzazi, dah akaambiwa anichape mbele ya wanafunzi wote na yeye alinipa stiki balaa. Siku ya kumaliza shule baada ya mtihani wa national form 2 nilipewa barua nipeleke home, nikaisoma kwanza kumbe ilikuwa ya kufukuzwa shule.

Ila one day yes, nimekutana naye ananiomba connection za town na kujidai ananisifia sana ila kila nikikumbuka madhila yake kule nyuma naona huyu ni snitch tuu! Nikaona isiwe tabu nikampa makavu asinijue tena nisije muitia mwizi hapa town!

NB: Mpatapo nafasi jamani jaribuni kuwa humble na kuishi na watu vizuri, siyo kuwachongea kwani life changes in a blink of an eye!
 
Wote mlikuwa na akili za kitoto ni kawaida mambo kama hayo

Acha ujinga mpe connection classmate wako. Haya maisha leo unamwona anahangaika kutafuta kazi kesho anaweza akawa chanzo cha msaada kwako au akawa hata mkuu wako.

Usijione umemaliza haya maisha tu mwanetu kuwa makini
 
Hii kwenye saikolojia huwa tunaiita Trauma. Unamkumbuka mtu aliyekufanyia mambo mabaya kwenye nyakati muhimu za maisha yako. Kiukweli, mtu afanyiwe ubaya wakati mwingine lakini siyo kipindi cha makuzi (Adolescence/Puberty), huwa hasahau kabisa kwasababu ndicho kipindi ambacho hutengeneza tabia atakazoenda nazo ukubwani. Kuna mambo mtu anaweza kuhisi kawaida, lakini kuchangiwa na ofisi nzima ya walimu kwa kosa hujafanya au kudhalilishwa mbele ya shule nzima ni vitu ambavyo mtu wa kawaida huwezi kuvisahau kabisa kwasababu vinaathiri afya ya akili ya mtu.

Japo sasa mkuu Poker , jambo kama hili unaliachia tu, litakutesa wewe zaidi kuliko yeye kwasababu unalikumbuka na linakuteletea uchungu. Halafu hapohapo linakupa furaha ya muda mfupi kuona yeye anateseka (Sadism). Wenzetu wazungu haya mambo huwa wanayatilia sana mkazo kwasababu yaanathiri afya ya akili ya mtu, kama hatakuwa makini.
 
Back
Top Bottom