dagaa
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 290
- 382
Habari wapendwa wangu,
Mimi nipo hapa sihitaji ushauri ila nataka niwasimulie kidogo lililonitokee, sababu sijamwambia mtu imenibidi niwadokezee.
Mimi ni mama wa watoto 2 na nimeolewa na ndoa ya kanisani, nina kazi yangu nzuri mshahara ni mzuri, maisha yangu ni mazuri tuna nyumba 2 na mume wangu na kila mtu ana gari yake, ila hapa kisa kilichonikuta ni kama ifuatavyo.
Baada ya Zaidi ya miaka kumi na 4 nimekutana na my first boyfriend, mi nashukuru nyumbani tulikua mambo safi, huyu boyfriend wangu tulikua tunasoma wote S.Africa, mi nilikuja nikaama nikaenda kusoma Canada nikamwacha hapo ila tukawa tunawasiliana kwa ukaribu sana, mwisho wa siku tukapotezana, ila kiukweli nilikua nampenda na nina iman nae alikua ananipenda.
Sasa bwana mwezi uliopita nilikua nina meeting na kampuni moja nikakutana na rafiki yake, du tulifurahi sana, tukapiga story mbili tatu, akaniambia unajua F (jina la boyfriend wangu niliyepotezana nae) alikua anakutafuta sana, tukabadilishana namba, mi sikutaka kumwomba ata namba ya F sababu najua sasa nina familia yangu na nina Imani nae atakua na familia yake.
Mara nafika ofisini mida ya jioni naona namba ngeni inaita, kupokea mara ni mimi mume wako F, nikacheka na tabasamu la furaha. Akaniuliza uko wapi nikamwelekeza ofisi yangu, yeye anaishi Arusha ndo anakofanya kazi, nikamwambia ok , cha kwanza aliniuliza ushaolewa nikamwambia ndio na nina watoto 2, nikamwomba nitampigia baadae sababu nilikua biz kidogo, saa kumi na moja natoka ofisini akanipigia nikaongea nae kwenye gari mpaka nafika nyumbani, tukapiga story nyingi.
Ila siku zinavyozidi kwenda ndo anazidi kutaka kuwa karibu na mimi, mara nikapata parcel ya DHL ina zawadi iliyoambatanishwa na picha ipo katika frame tuliopiga mi na yeye enzi tupo S. Africa kwakweli nilikumbuka mbali, nilipiga simu na kumwambia asante na nimeiweka ofsini kwangu. Ila nami nampenda na alinitamkia nimekupata tena sitegemei kukupoteza tena.
Juzi nimemtumia SMS ndefu nikamweleza ukweli mimi siwezi kuendelea nae sababu mimi nina familia yangu nae ana familia yake, sasa kila mtu achukue time yake, kwakweli kanitumia SMS nyingi sana kaniomba nisifanye ivyo, nimeamua ni mblock kila mahala ila cha kushangaza kanunua laini nyingi kwa ajili yangu nayo nimeblock, anatumia line nyingine, kwa sababu kila navyoendelea kuchati nae namimi nazidi kumpenda.
Ili kuepusha imebidi nifanye hivyo. Sasa jana nimeamka nimewaza mengi sana juu yake na nina mpenda na nikiangalia upande wa mume wangu nae kanitenda sana ila mi sitaki kufanya hivyo sababu wakati wa kufunga ndoa niliungama pale mbele nikasema huyu ndo awe mume wangu mpaka kufa, kwakweli in short alikua chagua langu na nilikua nampenda ila wanavyosema ndoa upangwa na Mungu ndo maana tulipoteana.